Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2024

Kibwana Shomari kumrithi Kapombe, Simba

Picha
Klabu ya Simba imeonyesha uhitaji wa kuipata huduma ya mlinzi wa kulia Kibwana Shomari ambaye anamaliza kandarasi yake mwisho wa msimu huu na waajiri wake Yanga SC ila hawajafikia mahitaji anayohitaji mlinzi huyo, Simba SC kuihitaji huduma ya mlinzi huyo ila wameweka dau dogo sana kwenye ada ya usajili japo imefahamika Simba SC wamepanga kuongeza dau.

FIFA kuifungia Israel kisa Palestina

Picha
Rais wa Shrikisho la soka duniani FIFA ,Gianni Infantino amesema kutakuwa na mkutano usiokuwa wa kawaida wa Baraza kuu, Julai 20 kutathmini ombi la Palestine na kuchukua maamuzi huru kuhusu kuifungia Israeli kujihusisha kwenye masuala ya soka kutokana na vita vinavyoendelea kwenye ukanda wa Gaza .

Mastaa wanne waomba kuondoka Azam FC

Picha
Wachezaji kadhaa wa Azam FC wameuomba uongozi wa klabu kusikiliza ofa zilizotumwa/zitakazotumwa kwa ajili yao msimu ujao. Baadhi ya majina yaliyoomba kusikilizwa ni James Akaminko, Feisal Salum, Cheikh Sidibe, Malickou Ndoye, Kipre Jnr... Hata hivyo uongozi wa Azam FC umekiri kupokea ofa za wachezaji hao na umedai hauna mpango wa kumzuia mchezaji yoyote atakayepata nafasi ya kuondoka

HUSSEIN KAZI KUMPISHA LAMECK LAWI SIMBA

Picha
Mlinzi wa kati wa Klabu Simba SC Husein Kazi anatajwa kuwa ni sehemu ya kukamilisha dili la Usajili la Mlinzi wa kati wa klabu ya Coastal Union Lameck Lawi Simba SC imetoa Kiasi cha pesa pamoja na Hussein kazi ili kukamilisha dili hilo ambalo lilikuwa la wengi kuelekea soko la usajili Haikuwa rahisi kwa Klabu ya Coastal Union kutupilia mbali ofa za Vilabu vya Ihefu na Azam FC ambao nao walituma ofa ya kumtaka Lameck Lawi Hussein Kazi amesajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu huu, ambapo alitazamiwa kutoa ushindani kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza kwenye timu hiyo hali ambayo ni kama imeshindikanika Simba wanatazamia kufanya maboresho makubwa ya kikosi chao kuelekea msimu ujao haswa mara baada ya kufanya vibaya msimu huu Inataarifiwa kuwa moja ya maeneo ambayo Simba SC wanaweza kufanya vyema ni pamoja na usajili wa beki, kiungo na mshambuliaji huku eneo la ufundi wakitazamia kuleta kocha mwenye rekodi kubwa kuja kufanya kazi na Mgunda.

AZAM YATANGULIA FAINALI CRDB BANK

Picha
Timu ya Azam FC imefanikiwq kuingia fainali ya kombe la CRDB Bank Federation Cup, maarufu kombe la FA baada ya jioni ya leo kuichapa Coastal Union mwbao 3-0 katika uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Abdul Sopu alikuwa wa kwanza kuiliza timu yake ya zamani baada ya dakika ya 41 kufunga kwa mkwaju wa penalti kabla ya Feisal Salum "Feitoto" dakika ya 70 kufunga la pili. Sopu kwa mara nyingine aliandika bao la tatu dakika 79 na kuipeleka fainali ikisubiri mshindi kati ya Ihefu SC na Yanga SC zitazochuana kesho Azam wametangulia fainali

FREDDIE AENDELEA KUFUNGA, SIMBA IKISHINDA 1-0

Picha
Bado Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wanaendelea kukamata nafasi ya tatu licha kwamba inapata ushindi, jioni ya leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mchezo wa Ligi Kuu bara. Kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi 60 lakini ikishikilia nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 60 isipokuwa ina uwiano mkubwa wa mabao ya kufunga. Yanga tayari imeshatwaa ubingwa ikiwa na pointi 71 bado ikiwa na mechi tatu mkononi, bao pekee la Simba limefungwa na mshambuliaji wake Freddie Michael dakika ya 7

Kaizer Chief kumtoa Djigui Diarra Jangwani

Picha
Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini inalenga kumsainisha kipa wa Yanga SC, Djigui Diarra raia wa Mali kwenye dirisha kubwa la usajili mwaka huu. Inaelezwa kuwa Amakhosi wameaandaa dau nono litakalowashawishi viongozi wa Yanga SC wamuachie nyota huyo wa timu ya taifa ya Mali na wanamuona kama mtu sahihi wa kwenda kuchukua nafasi ya kipa wao wa muda mrefu Itumeleng Khune. Licha wa uwepo wa mlinda Bruce Bvuma ambae ametoa Cleensheet 7 kwenye mechi 16 ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini PSL bado wanaona kuna haja ya kuongeza mlinda lango mwingine mwenye ubora kama Djigui Diarra.

RONALDO HATAKI KUPOKEA SIMU SAA 4 USIKU

Picha
Mshambuliaji nyota Cristiano Ronaldo na utaratibu wake wa usiku, mipaka ya muda wa kupokea na kuzungumza na simu. "Kitu muhimu, sizungumzi baada ya saa 4 au 5 usiku. Sipokei simu. Sipendi kuzungumza usiku kwa sababu ya afya ya akili yangu. Kwa hiyo, baada ya saa 4 usiku, tafadhali usinipigie simu".

Vinara wa mabao kwenye kombe la CRDB Bank

Picha
Wakati mtifuano wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB Bank Federation Cup ikianza kesho kwa Coastal Union na Azam FC huku Ijefu SC na Yanga zikifuata, Orodha ya wafungaji bora wanaowania tuzo imetoka na mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize anaongoza kwa mabao akiwa amefunga magoli matano. Edward Songo wa JKT Tanzania yeye anafuatua akiwa amefunga mabao matano na Yohana Nkomola wa Tabora United mwenye mabao matatu akilingana na Joseph Guede wa Yanga na Sadio Kanoute wa Simba wenye mabao matatu kila mmoja 

Singida Black Stars watua Arusha kucheza na Yanga FA Cup

Picha
Singida Black Stars zamani (Ihefu Sc) wameshafika Arusha kwaajili ya mechi ya nusu fainali ya CRDB BANK Federation Cup dhidi ya Yanga SC Jumapili hii. Singida wamefikia Themi Suites hotel Njiro na maandalizi yao wanafanyia katika uwanja wa UWC Kisongo zamani ISM. Mchezo kati ya Singida Black Stars na Yanga unatarajia kuwa mkali kwani timu zote zinawania kombe, lakini Singida wanaitaka nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa hapo mwakani

Yanga yamalizana na Prince Dube

Picha
Klabu ya Yanga SC imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Prince Dube kwa kandarasi ya miaka miwili akitokea Azam. Yanga itamtangaza rasmi mshambuliaji Prince Dube baada ya msimu kumalizika na itahusika kwenye masuala yote yanayomuhusu mchezaji huyo kwa mujibu wa kimkataba. Kutokana na hilo Prince Dube atamalizia pesa zilizobaki kutokana na kutoutumikia mkataba na fidia ya mkataba binafsi na Azam na almost 98% kumalizana na klabu ya Azam .

NGOMA NA WENZAKE WATEMWA

Picha
Klabu ya As Vita Club imevunja mikataba ya wachezaji watatu kufuatia Utovu wa nidhamu waliouonyesha kwenye Klabu pamoja na kwa viongozi wa benchi la Ufundi la Klabu hiyo, wachezaji hao ni, ▪️ Patrick Banza ▪️Nissi Ngoma ▪️Mike Dombo Patrick Banza yeye alimtukana Kocha Mkuu wa Klabu hiyo na kusema kwamba chanzo cha matokeo mabovu ya AS Vita Club ni Kocha Mkuu.

RATIBA YA MWISHO ZA YANGA, AZAM NA SIMBA

Picha
Mechi tatu za mwisho kwa Yanga na Azam wakati mechi nne za Simba ambazo zitaamua nafasi ya pili na ya tatu kwa miamba Azam na Simba wakati Yanga ikishatwaa ubingwa wa bara. 𝗬𝗼𝘂𝗻𝗴 𝗔𝗳𝗿𝗶𝗰𝗮𝗻𝘀 𝗦𝗖 : 🔰 22 - Dodoma Jiji » Ugenini. 🔰 25 - Tabora United » Nyumbani. 🔰 28 - Prisons » Nyumbani. Gamondi kocha wa Yanga 𝗔𝘇𝗮𝗺 𝗙𝗼𝗼𝘁𝗯𝗮𝗹𝗹 𝗖𝗹𝘂𝗯 : 🔵 20 - JKT Tanzania » Ugenini. 🔵 25 - Kagera sugar » Nyumbani. 🔵 28 - Geita gold » Ugenini. Dabo kocha wa Azam FC 𝗦𝗶𝗺𝗯𝗮 𝗦𝗽𝗼𝗿𝘁𝘀 𝗖𝗹𝘂𝗯 : 🔴 16 — Dodoma Jiji » Ugenini. 🔴 21 — Geita Gold » Nyumbani. 🔴 25 — KMC » Nyumbani. 🔴 28 — JKT Tanzania » Nyumbani. Mgunda kocha wa Simba SC

Ahmed Ally achekelea Kramo kubaki Simba

Picha
Na Shafih Matuwa Mpaka Kesho itaaminika kuwa Usajili bora wa Simba kwa msimu uliopita ni Huu wa Aubin Kramo. Kwa bahati mbaya majeraha yamewanyima Watanzania buradani tamu kutoka kwenye miguu ya mwamba wa Ivory Coast. Pongezi kwa viongozi wa Simba kwa kumbakisha na kumpatia Muda wa kupumzika na kupona kwa usahihi. Binafsi nadhani huu ni kama usajili mpya kwa Simba kuelekea msimu ujao na Kama Kramo atakuwa fit enough basi Tanzania itaimba jina lake. Kramo ni mtu haswaaa…..Sema başı majeraha ni kitu kibaya sana

SIO TP MAZEMBE TU, HATA SIMBA WAKAJIFUNZE KWA YANGA

Picha
Na Prince Hoza UONGOZI wa klabu ya TP Mazembe ya Lubumbashi, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, (DRC) wamefanya ziara nchini Tanzania na kufikia jijini Dar es Salaam yalipo makao makuu ya klabu ya Yanga SC. TP Mazembe chini ya bilionea na mwanasiasa wa DRC aliyepata kugombea urais misimu miwili na kuangukia pua, Moitse Katumbi imeamua kuja nchini kujifunza kitu kwa mabingwa wa Tanzania bara Yanga SC. Ni ngumu kuamini iweje kwa timu kubwa barani Afrika kama TP Mazembe kuja kujifunza kwa timu ambayo haijawahi kutwaa hata taji moja la CAF wakati wao wametwaa mataji matano ya Ligi ya mabingwa Afrika na moja la kombe la Shirikisho Afrika. Wanahabari nchini Tanzania wenyewe wanashangaa TP Mazembe kufunga safari na orodha ya viongozi wake na wakipatiwa mafunzo kutoka kwa Rais wa Yanga Injinia Hersi Said na wasaidizi wake akiwemo msemaji wa klabu hiyo Alikamwe. Afisa wa TP Mazembe akisikiliza kwa makini mafunzo ya Wanayanga Afisa wa TP Mazembe akiwa mafunzoni Sio TP Mazembe peke yako ambao wame

Sitaki mtoto wa nje ya ndoa- Jux

Picha
Mwanamziki wa RNB Juma Jux amevunja ukimya baada ya watu wengi kumjia juu kuhoji kwanini Mwanamziki huyo anabadili sana wanawake ila hapati kabisa mtoto kwa wanawake wote anaokuwa nao. Kupitia mahojiano hayo Juma Jux ameweka wazi kuwa hayupo tayari kupata mtoto na mwanamke yoyote ambaye hajafunga nae Ndoa, Kwa muktadha huo Juma Jux inaonesha hayupo tayari Kabisa Kupata Mtoto akiwa nje ya ndoa. Ikumbukwe hadi Sasa Juma Jux amekuwa kwenye Mahusiano na Jacklin Cliff, Vannesa Mdee, Jacqueline Wolper, na Kalen Bujulu hao ni wa Hapa Nchini tuu ila Wote hao wamepita salama Kwa Juma Jux bila kula ndimu na Udongo.

Nathaniel Chilambo aongeza mkataba Azam FC

Picha
Beki wa kulia wa Azam Fc Nathaniel Chilambo ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mwaka 2026. Chilambo amekuwa kwenye kiwango bora na kupelekea waajiri wake kumuongeza mkataba

YANGA HATIHATI KUSHIRIKI LIGI YA MABINGWA MSIMU UJAO

Picha
Kwa mujibu wa mwandishi Micky Jr ni kuwa timu zote ambazo zimekumbana na kadhia ya kufungiwa usajili kutokana na madai mbalimbali zipo katika hatari ya kunyimwa leseni ya ushiriki wa mashindano ya kimataifa msimu ujao kama tu, hawatamalizana na wadai wao mpaka kufikia Mei 31, mwaka huu. Kwa Tanzania miongoni mwa timu ambazo zimekutana na rungu la kufungiwa ni Mabingwa mara 30 wa Ligi Kuu Bara, Yanga.

MISRI HAKUNA KUSIFIWA- MAYELE

Picha
"MISRI Hakuna Kusifiwa Hakuna Kupostiwa, Huku Mechi Imeisha Umefunga Ume-assist, unarudi nyumbani kula wali unalala." "Kuna ukweli Waarabu wana ubaguzi, ukija uwe umejiandaa "Niliwahi kuongea na viongozi sijaja hapa kukaa benchi, tofauti na hapo December naondoka, mmetoa pesa lazima nicheze." "December tulienda Uarabuni, tukafungwa, kocha akaandika ripoti nitolewe kwa mkopo, president akakataa, kilichofuata huyo kocha akafukuzwa." "Pyramids hakuna bonus, niliuliza wachezaji wakasema hakuna, nakumbuka ni mechi na TP ndio president aliahidi pesa, lakini kitu kizuri wanalipa mshahara mkubwa." Fiston Mayele

AISHA MASAKA AREJEA UWANJANI SWEDEN

Picha
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya BK Hacken W ya Sweden, Aisha Masaka amerejea rasmi kwenye majukumu ya kuitumikia klabu yake baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha. Masaka katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu nchini Sweden, ameingia uwanjani dakika ya 72 wakati timu yake ikiwa imeshatanguliwa magoli 2-0. Mpaka mwisho wa mchezo huo, Hacken W wamekubali kudondosha alama kwa kupoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 2-0.

INONGA ATOROKA SIMBA

Picha
Inasemekana hali si shwari ndani ya klabu ya Simba SC inayopigania nafasi ya pili na mshindani wake Azam FC kwani inadaiwa baadhi ya wachezaji wake tegemeo kutoroka kambini. Mambo Uwanjani Blog imeupata ukweli kwamba beki wa kati wa klabu hiyo Mkongomani Henock Inonga "Backer'" kutoroka kambini akiwaiga wenzake Clatous Chama na Luis Miquissone. Inonga tayari ameuandikia barua uongozi wa klabu hiyo akitaka kuondoka na inadaiwa amesaini mkataba wa awali FAR Rabat inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga Nasreddine Nabi

NAJIM MUSA MIKONONI KWA YANGA

Picha
Baada ya Azam FC na Simba SC kubisha hodi kwa kungo fundi maestro kutoka Tabora United Najim Kusa, sasa rasmi klabu ya Yanga SC imeonesha nia ya kumhitaji kiungo huyo. Tayari Yanga imetuma ofa ikimuhitaji kwa ajili ya msimu ujao, Yanga imeridhishwa na kiwango chake na hivyo inaamini ikimpata itafanikiwa zaidi. Mpaka sasa Najim Musq hajasaini klabu yoyote ile sio Simba wala Azam hivyo nafasi iko wazi kwa Yanga kumsainisha

MWAKINYO, ALLOTEY KUZICHAPA MEI 31

Picha
Na Kione Hamisi Mahuruku Bondia Hassan Mwakinyo, usiku wa Mei 31, 2024 atapanda ulingoni kuzichapa na Mghana, Patrick Allotey kuwania mkanda wa Middle-WBO raundi 10. Pambano hili litasindikizwa na mapambano mengine tisa ya utangulizi. Usiku huu wa vitasa utaruka mbashara kupitia Azam Sports3HD

NABI AIPONGEZA YANGA

Picha
Kocha wa AS FAR Rabat ya Morocco ambaye aliipatia Yanga SC, ubingwa wa NBC Premier League, mara mbili Nasreddine Nabi, amewapongeza vijana hao wa mitaa ya Jangwani kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu jana baada ya kuichapa Mtibwa Sugar magoli 3-1. Nabi katika wakati wakati wake akikinoa kikosi cha Yanga, aliiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa NBC Premier League mara mbili mfululizo kwenye msimu wa 2021/22 na 2022/23.

ALGERIA KUOMBA UANACHAMA ASIA

Picha
Shirikisho la Soka Nchini Algeria limepanga kujivua Uanachama katika Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF na kujiunga na Shirikisho la Soka Barani Asia(AFC). Shirikisho hilo limedai kutotendewa haki na CAF hasa hata hivi karibuni katika mchezo wa timu yao ya USM Alger dhidi ya RS Berkane. Shirikisho hilo la A lgeria ni miongoni mwa mashirikisho makongwe kabisa barani Afrika lilianzishwa mwaka 1954.

MANULA HAJAWAHI KUMFIKIA DIARRA- JEMEDARI

Picha
Mchambuzi wa soka Jemedari Said Kazumari amesema mlinda mlango wa Simba SC na timu ya taifa, Taifa Stars, Aishi Manula "Tanzania One" hajawahi kuufikia uwezo wa kipa wa Yanga SC Djgui Diarra raia wa Mali. "Katika kipindi cha miaka 10 sijawahi kuona mlinda mlango mwenye ubora kama wa Djiguu Diarra. Unapaswa kuwa mkweli kwenye jambo linalotaka ukweli, Diarra amekuwa kipa bora mbele ya Aishi. Watu wajue nikisema hiki sicho sio kwa sababu nakuchukia bali namaanisha", alisema Jemedari Djigui Diarra

ALIKIBA HANA UNAFIKI- CHIDI BENZI

Picha
Mwanamuziki, Chidi Benz amesema miongini mwa wasanii ambao hawana tabia za kinafiki Ali Kiba ni mmoja wao. Akizungumza kupitia Manara TV, Chidi Benz amesema Ali Kiba amekuwa akimuweka sikio mara kwa mara pindi anaposikia Habari mbaya kuhusu yeye Chid Benzi "Alikiba amekuwa akinichana ukweli pindi ninapokosea au ninapomkosea siyo kama wasanii wengine wanaongea chinichini jamaa amenyooka sana " alisema Chid Benz

YANGA YAICHAKAZA MTIBWA NA KUTWAA UBINGWA WA NBC MARA TATU MFULULIZO

Picha
Klabu ya Yanga SC imetawazwa kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara #LigiKuu Kwa Msimu wa 2023/24 baada ya kufikisha Pointi nyingi (71) ambazo haziwezi kufikiwa na Klabu yoyote ya Ligi Kuu Msimu huu (Wakiwemo watani zao Simba) Huu ni Ubingwa wa 30 Kwa Klabu hiyo ikiendeleza REKODI ya kuwa Wababe wa Soka la Tanzania ambapo ndio Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi ya Tanzania huku pia wakibeba Back to Back mara ya tatu na ikiwa ni mara yao ya tano kutwaa mara 3+ na huku ikiwa timu pekee iliyotwaa Nusu ya MAKOMBE (30) ya Ligi Kuu Tanzania Bara tangu ilipoanzishwa Mwaka 1964. Yanga imetawazwa mabingwa wa NBC jioni ya leo baada ya kuilaza Mtibwa Sugar mabao 3-1, Mtibwa walikuwa wa Kwanza kupata bao dakika ya 32 likifungwa na Charles Ilanfya. Yanga wakasawazisha kupitia kwa Kennedy Musonda dakika ya 62 kwbla ya Nassoro Chombo dakika ya 65 na Clement Mzize dakika ya 82.

ALIYEKATAA GOLI LA GUEDE AONDOLEWA LIGI KUU

Picha
Na Shafih Matuwa Mwamuzi Shaban Mussa ameondolewa kwenye ratiba kwa mizunguko mitano baada ya kukataa goli la Joseph Guede. Kocha wa Yanga Miguel Gamondi ametozwa faini ya Tshs Milioni 2 kwa kuleta vurugu. Mchezo namba 201 ya Ligi Kuu ya NBC Yanga na Kagera Sugar

SUED MWINYI AFARIKI DUNIA

Picha
Mtangazaji maarufu wa mpira wa miguu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),Sued Mwinyi amefariki dunia. Sued Mwinyi amefariki dunia Mei 12, 2024 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila iliyopo Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Pumzika kwa amani Legend

MFANYABIASHARA TANGA AINUNUA MWADUI

Picha
Timu ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga ambayo ilitamba miaka ya hivi karibuni kwenye Ligi kuu Tanzania Bara, Rasmi imenunuliwa na Mfanyabiashara maarufu wa Madini Wilayani Korogwe mkoani Tanga na Mkoa wa Shinyanga Ahmed Waziri Gao na sasa makao yake makuu yatakuwa mkoani Tanga. Ikumbukwe kuwa Mwadui kwasasa imetinga hatua ya Nusu Fainali ya ligi Daraja la pili maarufu kama First League na endapo itafanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya ligi hiyo basi itakuwa imejihakikishia kupanda ligi Daraja la Kwanza maarufu kama 'Championship' kwa msimu ujao 2024/25. Mkurugenzi wa Timu hiyo Ahmed Waziri ‘Gao’ amewaeleza Waandishi wa Habari Kuwa, timu hiyo kwasasa imenunuliwa kutoka kwa wamiliki wa awali na sasa imehamia Wilayani Korogwe, "Tumeamua kuweka nguvu kubwa ya fedha ili tuipandishe timu yetu Ligi Kuu, hivyo wadau wa soka hasa mkoani Tanga tunawaomba waisapoti, hii ni timu yao." amesema Gao Kuhusu kubadilisha jina la Timu hiyo, Gao amesema wapo kwenye mchakato kama wat

AZAM JINO KWA JINO NA YANGA KILELENI

Picha
Mabao mawili ya kiungo mkabaji Yanick Bangala dakika ya 11 na Gibril Sillah dakika ya 15 na lile moja la KMC lililofungwa na Waziri Junior limetosha kuipa ushindi wa mabao 2-1 Azam FC katika uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu bara. Kwa ushindi huo Azam FC inaendelea kushika nafasi ya pili ikiwa jino kwa jino na vinara wa ligi hiyo Yanga SC ambao kesho wanatelemka dimbani kuwania pointi tatu muhimu. Simba jioni ya leo imeshindwa kuing' oa Azam kwenye nafasi ya pili baada ya sare ya kufungana 1-1 na Kagera Sugar

SERGE POKOU AOMBA KUONDOKA ASEC KISA SIMBA

Picha
Kiungo mshambuliaji wa Asec Mimosas, Serge Pokou ameomba rasmi kuondoka klabuni hapo huku akihusishwa na Simba inayoelezwa inampigia hesabu kali. Fundi huyo wa mguu wa kushoto ambaye aliwahi kuifunga Simba hapa nchini wakati timu hizo zilipokutana Ligi ya Mabingwa alisema ingawa ana ofa nyingi lakini amevutiwa na ofa ya Tanzania. “Nina ofa nyingi ikiwemo moja ya hapo Tanzania, lakini bado sijajua wapi nitakwenda ingawa napenda kuja kufanya kazi Tanzania, kuna marafiki zangu hapo wananiambia namna ligi ya huko ilivyo na ushindani,” alisema Pokou. “Nimewaomba viongozi wa klabu wasiniwekee ngumu katika kuondoka, nafahamu hii ni timu ambayo inapenda kuuza wachezaji wake Ulaya, napenda kwenda huko lakini nani anajua ni lini ofa kama hiyo itakuja?” Wakati Pokou akiyasema hayo, kocha wake Jullie Chevalier alisema kiungo huyo uamuzi wa kuondoka kwake unategemea na uongozi wa klabu yao endapo timu inayomtaka itawafuata kwa kuwa bado amesalia na mwaka mmoja.

CHIRWA AISOGEZEA UBINGWA YANGA

Picha
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC na Kagera Sugar wamegawana pointi moja moja baada ya jioni ya leo kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu bara katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Bao la Simba limefungwa kipindi cha kwanza na kiungo mshambuliaji chipukizi Ladack Chasambi ksbls ya Obrey Chirwa kusawazisha Kagera Sugar kipindi cha pili. Kwa matokeo hayo Simba ishika nafasi ya pili ikiishusha Azam hadi nafasi ya tatu lakini Azam inaweza kurejea nafasi yake baadae itakapochuana na Namungo Simba inayonolewa na kaimu kocha Juma Mgunda, imekuwa kwenye mwendelezo mzuri wa kushinda kwani huu ni mchezo wake wa nne ikishinda miwili, sare pia miwili. Kwa sare hiyo sasa ni rahisi kwa Yanga kwani inahitaji alama moja tu ili iweze kutangaza ubingwa kwani Simba haitaweza kufikisha pointi 69

BREKING NEWS/ MWAMNYETO ASAINI SIMBA

Picha
Taarifa zilizotufikia muda huu kwamba klabu ya Simba SC imempa kandarasi beki kisiki na nahodha wa Yanga SC Bakari Nondo Mwamnyeto ikiwa na maana msimu ujao ataitumikia klabu hiyo. Chanzo cha habari hizi bila shaka zimesema kwamba Mwamnyeto amesaini mkataba wa miaka miwili, beki huyo amemaliza mkataba wake wa miaka miwili na alikuwa kwenye mazungumzo wa kuongeza mkataba mpya. Mtoa taarifa huyo amedai kwamba Mwamnyeto ana mapenzi na Simba na ndio maana imekuwa rahisi kusaini klabu hiyo

AYOUB LAKRED HUYOOO WYDAD

Picha
Golikipa wa Simba ambaye ni raia wa Morocco, Ayoub Lakred yupo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha dili lake la kusaini Wydad AC kuelekea msimu ujao lakini bado hajasaini karatasi zozote mpaka sasa. Lakred ameshaipa taarifa klabu ya Simba kuwa ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu, huku klabu ya Raja AC ikituma ofa rasmi kwenye Menejiment yake ikihitaji kupata ya golikipa huyo ambaye amekuwa na msimu bora sana. Vilabu vya Wydad AC na Raja AC vinapambana kukamilisha dili hili kwa wakati

SIMBA YAMWEKEA NGUMU INONGA

Picha
Hennock Inonga "Backer' Simba imemuweka njiapanda beki wake Henock Inonga kwa kumpa nafasi beki huyo kuleta ofa ambayo atataka kwenda baada ya beki huyo kubakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake. “Inonga ishu yake iko tofauti kuna mambo ambayo hatuyafurahii, ni beki mzuri ila tunataka kufanya maamuzi magumu kwa kuwa amebakiza mwaka mmoja wa mkataba wake kama atakuwa na ofa ya kutakiwa na klabu yoyote tutaikaribisha mezani na tutafanya maamuzi ya kumuachia.”

MTANZANIA ASHINDA UBINGWA WA LIGI KUU UKRAINE

Picha
Beki wa Kimataifa wa Tanzania,Novatus Dismas ametwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Nchini Ukraine akiwa na Klabu yake ya Shakhtar Donetsk. Huu ni Ubingwa wa 15 kwa Klabu yake kwenye Ligi hiyo huku ukiwa ni Ubingwa wake wa kwanza wa Ligi Kuu. Hongera Novatus Dismas

YANGA KULAMBA BIL 1 FEITOTO AKIUZWA SIMBA

Picha
Inasemekana kuwa,Azam FC ikitaka kumuuza Feitoto kwa Simba ni lazima waipe Yanga kiasi cha pesa shilingi bilioni moja Akizungumza kwa code kwenye Sport Arena,mtaalamu wa za ndaani Ricardo Momo, amesema wanaomtaka Fei hawawezi kutoa hiyo pesa zaidi watasubiri amalize mkataba "Kuna mchezaji tumemwona hapa,alikuwa kwa mpinzani katoka kwa mpinzani kaenda kwa team kubwa ya tatu katika nchi yetu Sasa kuna tetesi watu wamezivumisha kuwa anaweza akaenda kwa wapinzani wengine si alikuwa kwa wapinzani,wale wazee wa Dabi, alikuwa upande mmoja kwa wazee wa Dabi na mpaka kuondoka kwake kulikuwa kwa kishindo mpaka ikabidi watu waingilie kati e bwana kaeni mzungumze ili mambo yaishe Sasa hizi za ndaani kabisa,mkataba wa yule mchezaji wa mauziano baina ya yule giant mmoja ambae alikuwepo mchezaji na huyu giant wa tatu Endapo wakitaka kumuuza kwenye Klabu ya humu ndani basi wao wanatakiwa wapate kiasi cha shilingi bilioni moja Giant wa kwanza si huyu alikuwa mchezaji wake,ikatokea tafrani wakamuu

KIPA TZ PRISONS ACHUKUA NAFASI YA METACHA, YANGA

Picha
Moja ya eneo ambalo Yanga itaingiza ingizo jipya msimu ujao ni katika nafasi ya kipa na hesabu zao zimeenda kwa kipa namba moja wa timu ya Tanzania Prisons, Yona Amos ambaye msimu huu alikuwa na dakika 90 bora alipowatibulia Simba wakati Tanzania Prisons waliposhinda 2-1 ugenini kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. . Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba kipa huyo anapigiwa hesabu kuwa mrithi wa Metacha Mnata ambaye mwisho wa msimu huu ataachwa. Metacha mkataba wake na Yanga unafikia mwisho wa msimu huu akirejea klabuni hapo kwa mara ya pili lakini kinachoelezwa kumng’oa ni nidhamu yake ambayo haiwavutii mabosi wa klabu hiyo. . Yona akiwa chaguo namba moja pale kwa Wanajeshi wa Magereza amefikisha jumla ya klinshiti sabaa msimu huu. Ana footwork nzuri Yuko vizuri sana kwenye CATCHING, Mipira ya kona, faulo anaicheza vizuri bila kutema, hili ni eneo lake la kujidai. ◉ Kwenye SAVES yuko superb

JOHN NOBLE MRITHI WA LAKRED SIMBA

Picha
Klabu ya Simba iko katika mazungumzo na golikipa wa Tabora United, John Noble ili kuchukua nafasi ya kipa wao anayetajwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu. Ayoub Lakred amekuwa kwenye kiwango bora sana kwa sasa huku akiwabeba wekundu hao wa msimbazi lakini ameshitua Kwa kuwaambia kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu huu mkataba wake utakapomalizika. Simba wanamuona Noble kuwa kipa sahihi wa kuidakia timu hiyo kwani ni golikipa mwenye uwezo wa juu akiwahi kuichezea klabu ya Enyimba na timu ya Taifa ya Nigeria. Kabla ya kumsajili Lakred, klabu ya Simba ilikuwa ikimuwinda kipa huyo kabla ya kuzidiwa kete na Tabora United. Hata alipotua nchini, Simba walijaribu kumsajili ili kuipiku Tabora jambo ambalo liliwazindua viongozi wa Tabora na kumsainisha mkataba haraka. John Noble alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Tabora United hivyo haitakuwa shida Kwa Simba kumpata na pia mchezaji huyo hawezi kukataa fursa ya kuitumikia klabu hiyo inayoshiriki michuano ya vilabu barani Afrika mara kwa mara.