Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2014

ZITTO KABWE KUMALIZA TOFAUTI ZA ALI KIBA, DIAMOND PLUTINUMZ

Picha
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amejitosa kusuluhisha ugomvi wa muda mrefu wa wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba na Nasibu Abdul 'Diamond'. Zitto alitoa kauli hiyo juzi wakati akihojiwa katika Kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha EATV baada ya kuulizwa kuwa ni jitihada gani amezifanya kusuluhisha ugomvi wa wasanii hao akiwa kama mlezi wa wasanii wanaotoka mkoani Kigoma.

DI MARIA RASMI MANCHESTER UNITED

Picha
Manchester United wamemsajili winga wa Real Madrid Angel Di Maria kwa kitita cha pauni milioni 59.7, ambayo ni rekodi ya uhamisho Uingereza. Winga huyo kutoka Argentina, amefanya vipimo vya afya siku ya Jumanne asubuhi na kusaini mkataba wa miaka mitano. Di Maria huenda akacheza mechi yake ya kwanza siku ya Jumamosi dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. Ada hiyo ya uhamisho inazidi ada ya pauni milioni 50 iliyotolewa na Chelsea kumsajili Fernando Torres kutoka Liverpool mwaka 2011. Di Maria aliishuhudia timu yake mpya ikizabwa mabao 4-0 na kitimu cha daraja la nne katika michuano ya Capital One hivyo Mna United imetupwa nje kabisa, ujio wa nyota huyo kunaweza kuifanya ibadili matokeo na kuanza kufufua matumaini yake mapya baada ya kuendelea kusuasua, Man United imeanza ligi ya premia ambapo imepoteza mechi moja na kutoka sare mojana ina pointi moja tu.

ETO'O ATUA EVERTON

Picha
Everton wamemsajili Samuel Eto'o kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuondoka Chelsea msimu uliopita.

SIMBA KUSHUKA TENA DIMBANI LEO NA MAFUNZO

Picha
Wakati Simba ikitarajia kucheza mechi ya kirafiki leo dhidi ya timu ya Mafunzo ya Zanzibar, kocha Patrick Phiri amesema anatarajia kupata kikosi cha kwanza baada ya Raphael Kiongera kuungana na wachezaji wenzake. Hii itakuwa ni mechi ya pili ya kirafiki kwa kikosi hicho cha Phiri, baada ya ile ya awali dhidi ya Kilimani City ambayo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Akizungumza jana kwa njia ya simu mara baada ya mazoezi ya timu hiyo, Phiri alisema Kiongera anatarajia kuwasili mwishoni mwa wiki, huku kikosi cha kwanza ambacho kitaanza kucheza katika michuano ya Ligi Kuu ya Bara kitajulikana wiki moja kabla ya michuano hiyo kuanza.

NGASSA AWAFUNIKA MBWANA SAMATTA, ULIMWENGU

Picha
MSHAMBULIAJI wa Yanga SC ya Dar es Salaam, Mrisho Khalfan Ngassa anaweza akawa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, michuano hiyo ikiwa imefikia hatua ya Nusu Fainali. Taarifa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imesema kwamba, Ngassa hadi sasa anaongoza kwa mabao yake sita baada ya hatua ya awali na ya makundi ya michuano hiyo.Ngassa alicheza mechi nne tu za Raundi mbili za awali za michuano hiyo, dhidi ya Komorozine ya Comoro nyumbani na ugenini, akifunga mabao matatu kila mechi. Baada ya hapo akacheza vizuri katika mechi zote mbili dhidi ya Al Ahly ya Misri, Yanga SC ikitolewa kwa penalti baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake. Lakini tangu hapo, wachezaji waliofanikiwa kumkaribia Ngassa kwa mabao msimu huu kwenye michuano hiyo ni watano, Haithem Jouini wa Esperance ya Tunisia, Edward Takarinda Sadomba wa Al Ahli Benghazi ya Libya, Iajour Mouhssine wa Raja Club Athletic ya Morocco na Knowledge Musona wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, a

SAMUEL ETO'O FILLS SASA KUTUA EVERTON

Picha
Everton inataka kumsajili mshambulizi nyota kutoka Cameroon Samuel Eto'o kwa mkataba wa miaka 2 Everton inataka kumsajili mshambulizi nyota kutoka Cameroon Samuel Eto'o kwa mkataba wa miaka 2 . Mshambulizi huyo aliruhusiwa kuondoka Chelsea mwisho wa msimu uliopita.

TANZANIA KUANDAA MATAIFA AFRIKA MWAKA 2017

Picha
Tanzania imeomba kuandaa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017, baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuiondoa Libya, iliyokuwa imepangwa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo. CAF ilitangaza kuiondoa Libya kutokana na kukumbwa na machafuko ya kisiasa nchini humo yaliyosababisha kutokuwa na serikali imara. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa (TFF), Selestine Mwesigwa, alisema wametumia nafasi hiyo kuomba kuwa wenyeji wa Afcon 2017.

JESHI KAMILI LA NOOIJ TAYARI KUIVAA MOROCCO

Picha
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Morocco iliyopangwa kufanyika Septemba 5, mwaka huu nchini humo. Wachezaji walioitwa kwa ajili ya mechi hiyo ambayo ipo katika Kalenda ya Fifa ni makipa Deogratius Munishi (Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni Said Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari Kapombe (Azam), Nadir Haroub 'Cannavaro' (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Joram Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).

SUGE KNIGHT ANUSURIKA KUUAWA

Picha
Mkurugenzi wa zamani wa kampuni ya muziki ya Deathrow ya Marekani, Suge Knight anaripotiwa kufanyiwa upasuaji hospitali kufuatia kupigwa risasi katika sherehe isiyo rasmi ya tuzo za video bora za MTV. Suge Knight inadaiwa alipigwa risasi kadhaa mapema siku ya Jumapili (Agosti 24), akiwa West Hollywood nightspot 1 Oak. Knight aliweza kuondoka huku akitembea mwenyewe katika sherehe hiyo iliyoandaliwa na Chris Brown, kabla ya polisi kumsaidia, kwa mujibu wa tovuti ya TMZ.

BALOTELLI RASMI LIVERPOOL

Picha
Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli, 24, amekamilisha uhamisho wake kutoka AC Milan kwenda Liverpool kwa pauni milioni 16. Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City, amekubali mkataba wa muda mrefu, ingawa hatoweza kucheza dhidi ya timu yake ya zamani Jumatatu usiku (Jana).

MANENO YA DIAMOND YAMLIZA AUNT EZEKIEL

Picha
Star wa filamu nchini Aunty Ezekiel anadaiwa kuchomwa vilivyo na maneno ya Diamond kwa Wema Sepetu yanayodaiwa kumgusa yeye pia moja kwa moja kama rafiki wa Wema, Diamond juzi alisema  kuwa Wema anapenda sana starehe na mashoga wapenda kujirusha badala ya kufanya kazi ili kujiletea maendeleo kwa kutumia fursa aliyonayo sasa. Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Aunty kikizungumza  jana kwa masharti ya kutotajwa jina kilisema kuwa baada ya Aunty kuona alichoandika Diamond aliachia msonyo wa kufa mtu kuonyesha hakupendezwa hata kidogo huku akibaki kuumia. "Aunty alipoona alichoandika Diamond alichia msonyo huo ! unajua maneno ya Diamond yamejaa ukweli mtupu, yalikuwa kama mkuki kwa Aunty, Aunty ni mtu wa starehe sana si umeona hata ndoa yake haina uhai, ukweli unauma, yeye na Wema wanapaswa kujiangalia upya Diamond amempa Wema ushauri mzuri sababu anampenda"

MESSI ATIKISA, SUAREZ AANZA KAZI BARCELONA IKIUA 6-0

Picha
Luis Suarez Luis Suarez alichezea Barcelona mechi yake ya kwanza baada ya kuhamia huko kutoka Liverpool kwa €95 milioni huku klabu hiyo ya Catalona ikikomoa Club Leon ya Mexico 6-0 mechi ya kirafiki Jumatatu. Straika huyo wa Uruguay, ambaye hataweza kuchezea Barca mechi ya ushindani hadi Oktoba baada ya rufaa yake dhidi ya marufuku ya miezi minne kutokana na kumng’ata difenda wa Italia Giorgio Chiellini wakati wa Kombe la Dunia kukataliwa wiki iliyopita, alitolewa na nafasi yake kujazwa na Rafinha Alcantara dakika 14 kabla ya mechi kumalizika. Barca walikuwa tayari wanaongoza 4-0 kutokana na mabao ya Lionel Messi, Munir El Haddadi na mawili kutoka kwa Neymar kabla ya Munir na Sandro kukamilisha ufungaji mabao yao.

CHELSEA YAISHUSHIA MVUA YA MABAO BUNRLEY

Picha
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho Chelsea ilipeleka kilio kwa Burnley usiku wa jumatatu katika mchuano wa ligi kuu ya England ambapo Chelsea iliitandika Burnley mabao 3-1.

AZAM FC FULL KUIVAA EL MERREIKH KESHO

Picha
BEKI Shomary Kapombe na mshambuliaji Lionel Saint- Preux kutoka Haiti wote wamefanya mazoezi kikamilifu jana na leo kuelekea mchezo wa kesho wa Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Azam FC ikimenyana na El Marreikh ya Sudan, Uwanja wa Nyamirambo, Kigali, Rwanda. Wawili hao waliokuwa wanasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja, walikosa mchezo wa mwisho wa Kundi A dhidi ya Adama City ya Ethiopia, Azam FC ikishinda 4-1.

ARSENAL, BASIKTAS USO KWA USO LEO

Picha
Kocha wa Arenal, Arsene Wenger Beki wa kushoto wa Arsenal, Kieran Gibbs atakosa mechi zote za ligi ya mabingwa dhidi ya Besiktas baada ya kuumia eneo la uvungu wa goti. Gibbs atakaa benchi kwa takriban majuma matatu baada ya kuumia wakati wa mchuano kati ya Arsenal na Crystal Palace siku ya jumamosi. Pia mshambualiaji Yaya Sanogo hajasafiri kwenda uturuki kwa ajili ya mpambano wa leo

MIMI SIYO FREEMASON- HOZA

Picha
MTENDAJI mkuu wa mtandao wa Mambo Uwanjani blogspot, Prince Hoza amekanusha vikali kuwa yeye si muumini wa dini ya kishetani ya Freemason tofauti inavyoelezwa kuwa anashiriki kuunganisha watu katika imani hiyo. Hoza amedai watu wengi wamekua wakimpigia simu ili awaunganishe katika imani hiyo inayodaiwa ni ya kishetani na inayowapa watu utajiri, akizungumza na Mtandao huu, Hoza amesema yeye si freemason isipokuwa ameshiriki kuandika habari za freemason hivyo asihusishwe  kabisa na imani hiyo. 'Unajua watu si waelewa, niliandika habari moja ambayo nilifanya mahojiano na msanii mmoja ambaye anadai yeye ni memba wa freemason, hivyo niliitoa katika mtandao huu na kuweka jina langu kama mwandishi, nashangaa baada ya hapo watu wengi wamekuwa wakinipigia simu wakitaka niwaunganishe', alisema na kuongeza.

PHIRI AAHIDI UBINGWA MSIMBAZI, MAXIMO AMTUNISHIA MISULI

Picha
Wakati Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia Patrick Phiri akidai ubingwa bila kuifunga Yanga hauna raha, Marcio Maximo ametamba kutumia kikosi mseto cha wakongwe na chipukizi kwenye Ligi Kuu Bara iliyopangwa kuanza Septemba 20, mwaka huu. Akizungumza na gazeti hili kabla ya kuondoka kuelekea visiwani Zanzibar mwishoni mwa wiki ambako Simba imeweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya, Phiri alisema moja ya mikakati aliyojiwekea ni kuhakikisha anatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara lakini hautanoga bila kuifunga Yanga. "Moja ya mikakati niliyojiwekea ni kuhakikisha Simba inatwaa ubingwa wa ligi ikiwa chini yangu, lakini nitafurahi zaidi nikitwaa ubingwa na kuifunga Yanga," alisema Phiri.

CHELSEA KUMENYANA NA BURNLEY

Picha
Mourinho ana kibarua kwa kuwa wachezaji kadhaa wamejeruhiwa Ligi kuu ya England ambayo imeanza jumamosi iliyopita itaendelea jumatatu hii ambapo Burnley watawakaribisha Chelsea kwenye uwanja wa Turf Moor. Burnley huenda wakawatumia wachezaji wake mahiri akiwemo Lukas Yukiviz ambaye amesajiliwa msimu huu wa majira ya joto akiungana na Danny Ings kuunda safu bora ya ushambuliaji kama ambavyo wamejidhihirisha ubora wao katika michezo ya majaribio kabla ya ligi. Mlinda mlango wao pia sasa yupo salama na timamu kuikabili Chelsea baada ya kukosa michezo kadhaa ya majaribio kutokana na majeraha ya hapa na pale.

LIVERPOOL NOMA SANA, YAIGONGA SOUTHMPTON 2-1

Picha
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers alikuwa na kila sababu ya kutabasamu alipoingia uwanjani Anfield na kuwasikia mashabiki wa klabu hiyo wakishangilia na kuimba nyimbo za kumsifu kwa kuiokoa klabu hiyo msimu uliopita alipoiongoza kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Manchester City. Lakini wapinzani wao Southampton licha ya kuwa walikuwa wamewapoteza wachezaji watatu kwa mahasimu wao Liverpool hawakuwa wepesi wa kupisha mpira .

ROBO FAINALI KOMBE LA KAGAME NI KUSUKA AU KUNYOA

Picha
KAMA refa Israel Mujuni angekuwa sahihi, bila shaka Gor Mahia ingekuwa moja ya timu zilizofuzu Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mwaka huu mjini Kigali, Rwanda. Lakini kwa makosa ya kibinadamu, akakataa bao safi la tatu la Gor katika mchezo wa Kundi B dhidi ya APR na mwisho wa mchezo, timu hizo zikatoka sare ya 2-2. Gor ilihitaji kushinda mechi mbili za mwisho za kundi lake dhidi ya APR na Telecom ya Djibouti, baada ya kufungwa mechi mbili za awali na KCC ya Uganda na Atletico ya Burundi ili iende Nane Bora, lakini ikaambulia pointi mbili katika mechi hizo kwa sare ya 2-2 kila mchezo. Gor iliingia katika mchezo dhidi ta Telecom ikiwa tayari inajua KQ inawasubiri Uwanja wa Ndege wa Kigali kuwarejesha Nairobi- hivyo walikuwa hawana cha kupigania.

WASANII KILI MUSIC TOUR WAENDA KUMFARIJI AFANDE SELE MORO

Picha
BAADHI  ya picha zikionesha wasanii waliofanya Tamasha la Kili Music Music Tour Dodoma wakiwa nyumbani kwa Afande Sele katika kumpa pole ya kuondokewa na aliyekuwa mkewe marehemu Asha au mama Tunda kama anavyofahamika. Wasanii hao baada ya kjukamua katika tamasha la Kill waliamua kumtembelea msanii mwenzao aliyepata kuchukua ufalme wa muziki nchini. Afande Sele yuko katika majonzi mazito kufuatia msiba huo hivyo ni vema wasanii wenzake wakachukua fulsa hiyo kwenda kumfariji, Tunawapongeza wasanii hao kwa kumuonamzwenzao na kumpa pole.

MARADONA AMPIGA MAKOFI MWANAHABARI

Picha
Diego Maradona Mstaafu wa soka nchini Argentina, Diego Maradona, amenaswa kwa kanda ya picha akichapa mwanahabari Jumamosi kulingana na runinga ya Sky Sports. Makabiliano hayo walitokea wakati gwiji huyo, 53, alikuwa akiondoka kutoka ukumbi wa maonyesho ya sanaa na mwanaye ambaye alikuwa ameenda kutizama tamthilia ya Siku ya Watoto ya Argentina. Imeripotiwa kuwa mwanahabari mhusika alikunjia jicho mamake mwana huyo ambaye ni mpezi wa kitambo wa Maradona, Veronica Ojeda. Maradona, ambaye alishinda Kombe la Dunia kama mchezaji 1986 na kuongoza taifa lake kama kocha kutoka 2008 hadi 2010, ana uzoefu wa kuzozana na wanahabari.

KROOS, RODRIGUEZ KUANZA DHIDI YA SEVILLA

Picha
Toni Kroos Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, amedhibitisha ataachilia mizinga yake mizito ikiwemo nyota wapya Toni Kroos na James Rodriguez kwenye kombe la Uefa Super dhidi ya Sevilla Jumanne. Viungo hao wa kati walianza mazoezi Agostu 5 baada ya kuibuka mashujaa katika Kombe la Dunia, Rodriguez kwa Colombia na Kroos kwa mabingwa wa dunia, Ujerumani lakini Ancelotti alisema wote wataanza kivumbi hicho kitakacho toa vumbi jijini Cardiff. “Ndio, wote watakuwa kwenye orodha ya watakaoanza,” alijibu alipoulizwa ikiwa atawatumia nyota hao. Kroos anatarajiwa kushirikiana na Luka Modric kati kati mwa kiwanja huku Rodriguez akicheza nambari 10. Ancelloti alitangaza kwamba nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo, atashiriki kutoka kipenga cha mwanzo licha ya kusumbuka na jeraha sugu la goti katika Kombe la Dunia.

MANGALA SASA NDIYE BEKI GHALI ENGLAND

Picha
KLABU ya Manchester City imemfanya Eliaquim Mangala kuwa beki ghali zaidi kwa sasa katika historia ya soka ya Uingereza, baada ya kumnunua kwa Pauni Milioni 31.9 beki huyo wa akti wa Ufaransa kutoka FC Porto.   Ndoto za Mangala kuhamia Ligi Kuu ya England hatimaye zilitimia jana baada ya kuupiku uhamisho wa Pauni Milioni 30 uliomtoa Rio Ferdinand Leeds kuhamia Manchester United mwaka 2002.

PATRICK PHIRI KOCHA MPYA SIMBA

Picha
KOCHA bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2009/2010, Patrick Phiri anatarajiwa kutua Dar es Salaam wiki hii kwa ajili ya kusaini Mkataba wa kuifundisha klabu yake ya zamani, Simba SC. Mzaliwa huyo wa Mei 3 mwaka 1956, alifanya kazi kwa awamu tatu tofauti akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi kati ya mwaka 2004 na 2010 na kwa mafanikio makubwa- na sasa anataka kurejesha enzi. Mzambia huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC, misimu ya 2004/2005 na 2009/2010 na pia alishinda Makombe ya Tusker mwaka 2005 la Tanzania na Kenya. Kiboko ya Yanga anarudi; Patrick Phiri anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Ijumaa kusaini Simba SC

HARUNA NIYONZIMA AISHANGAA YANGA

Picha
Kiungo wa kimataifa wa timu ya Yanga ya Tanzania Bara, Haruna Niyonzima, amesema kitendo cha timu yake kutoshiriki mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) kwenye ardhi ya kwao, Rwanda kimemuumiza sana. Yanga iliondolewa kushiriki mashindano ya Kombe la Kagame baada ya kutaka kuleta kikosi cha pili chini ya kocha msaidizi, Mbrazil, Leonardo Neiva, hivyo nafasi yao kuchukuliwa na Azam. Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Dar es Salaam, Niyonzima, alisema alitamani sana kushiriki mashindano hayo na anaamini Yanga ingechukua kombe la michuano hiyo.

LIVERPOOL YAICHAKAZA DORTMUND 4-0, COUTINHO ANG'ARA

Picha
Mshambulizi wa Liverpool Dejan Lovren aliifungia the Reds bao lake la kwanza katika mechi yake ya kwanza Liverpool ilipoilaza Borussia Dortmund mabao 4-0 katika mechi ya kirafiki. Daniel Sturridge ndiye aliyeifungua kivuno hicho cha mabao baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Phillippe Coutinho.

ARSENAL MABINGWA NGAO YA COMMUNITY

Picha
Arsenal ndio mabingwa wa mwaka huu wa ngao ya Community. Arsenal ndio mabingwa wa mwaka huu wa ngao ya Community. Vijana wa Arsene Wenger waliwanyuka mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza Manchester City mabao 3-0 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Wembley.

NI SAHIHI KWELI LOGARUSIC KUTUPIWA VIRAGO SIMBA!

Picha
Na Prince Hoza Masaa yanayoyoma nilipeni changu kabisa niondoke: ndivyo ishara ya picha hii inavyojionyesha, Loga amefutwa kazi jana HATIMAYE Klabu ya Simba imemtimua kazi Kocha Mkuu wao, Mcroatia Zdravko Logarusic kwa madai ya kukiuka taratibu na miiko ya klabu hiyo. Hatua hiyo imefikiwa ikiwa ni siku moja baada ya Loga kuiongoza timu hiyo kupokea kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Zesco ya Zambia kwenye mechi ya Tamasha la Simba maarufu kama 'Simba Day' lililofanyika Uwanja wa Taifa Jumamosi. Klabu ya Yanga, Desemba mwaka jana ilimtimua Kocha wake Mkuu, Mholanzi Ernie Brandts ikiwa ni siku mbili baada ya kufungwa 3-1 na watani zao, Simba katika mechi ya ndondo ya 'Nani Mtani Jembe' iliyoandaliwa na wadhamini wao wakuu Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro. Ingawa Simba haikuwa tayari kueleza kwa kina miiko na taratibu alizokiuka kocha huyo, lakini habari za ndani kutoka chanzo chetu ndani ya klabu hiyo zinadai kuwa kiwango kibovu kilichoonyeshwa

SPIDER- SIJAACHA MUZIKI

Picha
Mwanamuziki tokea kitambo aliyekuwa akiunda kundi la Mambo Poa Rashid Mustapha 'Spider' (Pichani)  ambaye kwa sasa ni mtangazaji wa Chuchu Fm Zanzibar amesema ajaacha muziki licha ya kubanwa na kazi. Akizungumza na Mwanasoka, Spider aliyekuja jijini katika msiba wa dada yake amesema muziki huko kwenye damu yake na kamwe awezi kuacha, 'Mimi na muziki ni sawa na uji namgonjwa siwezi kuacha licha ya kubanwa na kazi', aliongeza.

AZAM YAIFUMUA KMKM 4-0

Picha
AZAM FC jana walitoa ujumbe mzito kwa wapinzani wao katika Kombe la Kagame la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati wakati walipoifunga timu ya KMKM ya Zanzibar kwa magoli 4-0 katika mechi yao ya pili ya Kundi A kwenye Uwanja wa Amahoro hapa Rwanda.

WENGER ASHANGAZWA NA MTANDAO WA KLABU YA MAN CITY

Picha
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger Jumapili alieleza kushangazwa kwake na mpangilio ambao umewezesha kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea Frank Lampard kujiunga na klabu ya Manchester City kwa mkopo kutoka kwa ‘klabu-dada’ ya New York City. Pamoja na kuhamia kwa Lampard uwanja wa Etihad, New York pia wamemkopesha straika wa Uhispania David Villa kwa Melbourne City. Klabu zote tatu zinamilikiwa na City Football Group, kampuni inayomilikiwa na wamiliki wa City, Abu Dhabi United Group. Wenger, ambaye timu yake itakabiliana na City wikendi ijayo kupigania Community Shield, alidokeza kwamba ushirika huo huenda ukawapa mabingwa hao wa Ligi ya Premia nafuu wasiyofaa.

NISHA, MBOTO WAJIWEKA JUU NA FILAMU YAO YA KIDUME

Picha
Mastaa wa filamu nchini Salma Jabu Nisha na Mboto wamekuja na filamu mpya inayoitwa Kidume ambayo tayari ipo sokoni tangu juzi. Nae Nisha ameandika"Si muda mrefu tangu ZENA NA BETINA itoke,..ila linapokuja swala la jamii yangu huwa nasitisha lolote ili niweze kujitoa, pengine hutojitoa kwa pesa,ila unaweza kufanya kitu ukatengeneza pesa kwa ajili ya kusaidia kitu hiko, wenye imani (wakristo safi/Islam safi) huwa tunaamini ukitoa mkono wa kulia wa kushoto usione, nilijifunza hilo mwanzoni mwa mwaka huu moja ya comment ya shabiki yng humu humu instagram,. Kwa kuwa huwa napenda sana kusikiliza ushauri bora basi na huo ni kati ya shauri bora nililolifanyia kazi,nirudi kwenye mada ‪#‎KIDUME‬ "KIDUME " ni filamu ambayo imenifanya niandike yote haya sababu tulijitoa kwa ajili kufanya watu fulani wanaolia wapate afueni, wenye mateso ya muda mrefu

MART NOOIJ ALIA NA REFA MGANDA KUKATAA BAO HALALI LA STARS JANA DHIDI YA MAMBAS

Picha
KOCHA wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema kwamba refa Mganda, Dennis Batte alikataa bao halali lililofungwa na John Bocco ‘Adebayor’ jana katika mchezo dhidi ya wenyeji Msumbiji, Uwanja wa Zimpeto mjini hapa. Akizungumzia baada ya mchezo huo ulioisha kwa Mambas kushinda 2-1 jana, Mholanzi huyo alilalamikia bao ambalo Taifa Stars ilifunga dakika ya 17 kupitia kwa John Bocco lakini likakataliwa na mwamuzi Dennis Bate kutoka Uganda. Aidha, Nooij amesema moja ya sababu za kikosi chake kupoteza mechi dhidi ya Mambas jana ni wachezaji wake kucheza kwa wasiwasi katika kipindi cha kwanza. Taifa Stars iliruhusu bao la kwanza sekunde chache kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza katika mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kucheza hatua ya makundi iliyochezwa leo (Agosti 3 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Zimpeto hapa Maputo.

TANZANIA, KENYA ZOTE MAJANGA AFCON

Picha
Kenya na Tanzania zimeshindwa kufanya vizuri katika michuano ya kufuzu kombe la taifa bingwa Afrika mwaka 2015 huku Uganda ikifanikiwa katika hatua ya Makundi Lesotho ilitoka sare ya kutofungana na Kenya mwishoni mwa juma jijini Nairobi, matokeo yaliyofanya Lesotho isonge mbele kwa ushindi wa goli la kufunga na kufungwa. Kutokana na kupoteza mchezo huo, Shirikisho la Soka nchini Kenya limefuta kazi kitengo cha ufundi cha Harambee Stars , ikiwemo kumsimamisha kazi Kocha Mbelgiji Adel Amrouche. Kikosi cha Harambee Stars kilikua chini ya usimamizi wa James Nandwa siku ya jumapili lakini naye alisimamishwa kazi sambamba na wahusika wa idara ya ufundi.

DROGBA ARUDI NA MGUU MBAYA CHELSEA, ASHINDWA KUNG'ARA

Picha
MKONGWE Didier Drogba ameshindwa kung'ara akiichezea Chelsea kwa mara ya kwanza tangu arejee msimu baada ya kuchapwa mabao 3-0 Werder Bremen nchini Ujerumani katika mchezo wa kujiandaa na msimu.

NINGEPENDA KUCHEZA FILAMU NA CHRIS TUCKER NA ROSE NDAUKA- FRANK MWIKONGI

Picha
Star mkubwa wa filamu nchini ambaye hana skendo za hovyo hovyo Frank Mohamed Mwikongi amesema kuwa ana ndoto ya kuja kufanya filamu na star wa Hollywood Chris Tucker kwa kuwa anamkubakli sana, na kwa upande wa hapa nchini anataka kufanya kazi na Rose Ndauka kwasababu anaukubali uwezo wake licha ya kuwa tayari wamefanya pamoja filamu ya Waiting Soul lakini yupo mbioni kucheza nae tena filamu mpya.

TAIFA STARS YAKWEPA HUJUMA ZA MAMBAS

Picha
Kikosi cha timu ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), kinatarajiwa kuwasili leo jioni mjini Maputo tayari kwa mechi yao ya marudiano dhidi ya wenyeji Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Jumapili Agosti 3, mwaka huu, huku kikiwa kimejipanga vema kukwepa 'fitna' za ugenini. Katika kuhakikisha kikosi cha Taifa Stars kinakuwa kwenye mazingira yenye usalama na kuepuka 'hujuma' ya aina yoyote kutoka kwa wenyeji, Shirikisho la Soka nchini (TFF) limetanguliza ujumbe maalumu ili kuweka mipango ya mapokezi vizuri. Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya TFF, Wilfred Kidao, alisema Stars itawasili jioni Maputo na kila kitu wamekiandaa wao ili kuhakikisha kikosi kinakuwa kwenye mazingira salama.

SERIKALI YAINGILIA KATI UJIO WA REAL MADRID, FIGO ATHIBITISHA KUTUA

Picha
KAMATI ya Maandalizi ya ziara ya kikosi cha magwiji wa Real Madrid ya Hispania, jana imemtembelea Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara kumjulisha rasmi juu ya tukio hilo na mwanamama huyo kwa niaba ya Serikali, ameahidi kutoa ushirikiano.

RUDISHA AAMBULIA MEDALI YA FEDHA GLASGOW

Picha
Rudisha alikuwa bingwa wa Olimpiki mjini London mwaka 2012 Bingwa wa Olimpiki na ambaye pia anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 800 mkenya David Rudisha aliambulia medali ya fedhakatika mashindano ya Jumuiya ya madola.

PAUL SCHOLES AMPA USHAURI WA BURE VAN GAAL MAN UNITED

Picha
GWIJI wa Manchester United, Paul Scholes amemuagiza kocha Louis van Gaal kununua mabeki wawili kwa kuwa kuna udhaifu kwenye safu ya ulinzi.   Labda enzi za utawala wao zimepita, lakini wakati United inawatema Nemanja Vidic, Rio Ferdinand na Patrice Evra msimu huu, imepoteza wachezaji watatu ambao wameshinda mataji 16 ya Ligi Kuu ya England baina yao.