Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2017

Stars yaitwanga Burundi 2-1, Mavugo aendelea kumtungua Dida

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo imefanikiwa kuitwanga Burundi mabao 2-1 mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Huu ni mchezo wa pili mfululizo Stars ikipata ushindi, Jumamosi ya juma lililopita Stars iliilaza Botswana mabao 2-0 katika Uwanja wa Taifa, Stars inayonolewa na Salum Mayanga inaonekana kuimarika na kutia matumaini. Ilijipatia bao la kuongoza lililofungwa na winga Simon Happygod Msuva, hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa bao hilo, Burundi ilisawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake Laudit Mavugo ambaye anaichezea Simba ya Tanzania. Bao hilo la Mavugo ni kama mwendelezo wake wa kumtungua kipa Deogratus Munishi "Dida" anayeichezea Yanga pia ya Tanzania, bao la pili na la ushindi la Stars lilifungwa na Mbaraka Yusuph

Nay wa Mitego akamatwa na polisi

Picha
Na Ikram Khamees. Morogoro Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Emmanuel Elibarik maarufu Nay wa Mitego amekamatwa na jeshi la polisi mjini hapa akiwa kwenye shoo zake za kimuziki. Taarifa iliyopatikana inasema Nay wa Mitego amekamatwa na polisi Mvomero lakini bado haijawekwa wazi kipi kilichopelekea kukamatwa kwake. Lakini chanzo chetu kimabaini kuwa msanii huyo amekamatwa na polisi kwa sababu ya kuachia wimbo wake mpya uitwao 'Wapo' ambao ndani yake una maneno yenye ukakasi, wimbo huo umemdisi waziwazi rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ukimwambia kuwa amezuia uhuru wa habari na serikali yake inaendeshwa kwa kiki

Nape afunika Taifa, mashabiki waimba "Nape.....Nape....Nape

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Hivyo ndivyo ilivyokuwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilipocheza na Botswana mchezo wa kirafiki. Waziri wa zamani wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii, Nape Moses Nnauye alikuwa gumzo mara baada ya kuwasili uwanjani hapo kushuhudia mtanange huo. Nape alizoa mashabiki lukuki ambao walimzonga huku wengine wakitaka kupiga naye picha, Waziri huyo aliyedumu kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenye serikali ya JPM alikuwa kivutio kikubwa. Baadaye Nape aliungana na waziri aliywmrithi kwenye wizara hiyo Mhe Dkt Harrison Mwakyembe na kukaa naye jukwaa moja kisha baadaye meneja wa zamani wa Yanga, Mohamed Bhinda aliwafuata wote na kuwakumbatia

Banda mchezaji bora Simba

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Kiungo Abdi Hassan Banda amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Klabu ya Simba wa mwezi Februali. Banda ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza tangu arejee kwenye kikosi cha kwanza, kiungo huyo mrefu anayemudu kucheza nafasi zote za ulinzi amecheza vizuri mwezi Februali na kuiwezesha klabu hiyo kuendelea kukaa kileleni. Kwa maana hiyo Banda atazawadiwa kitita cha shilingi Laki tano za Kitanzania ambazo hutolewa kwa mchezaji bora wa mwezi, Banda ameshinda tuzo hiyo wakati Laudit Mavugo alishinda pia tuzo kama hiyo Januari

Samatta aing' arisha Stars, apiga zote mbili

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa na nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jioni ya leo ameing' arisha Taifa Stars baada ya kuifungia goli moja kila kipindi na kuifanya Stars iibuke na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Botswana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Huo ni ushindi wa kwanza kwa kocha mzalendo Salum Mayanga aliyerithi mikoba ya mzalendo mwenzake Charles Boniface Mkwasa, Samatta aliifungia Stars bao la mapema la kuongoza katika kipindi cha kwanza. Nahodha huyo leo aling' ara vilivyo akicheza vizuri licha ya kukosa mtu wa kuelewana naye kwani Stars ingeweza kuibuka na ushindi mkubwa zaidi, Samatta alifunga bao la pili na la ushindi. Baada ya mchezo wa leo, Stars sasa inajiandaa kwa mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Burundi, katika mchezo wa leo winga Simon Msuva alipoteza nafasi nyingi za wazi

Sunche na Kapeto madansa waliotikisa

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Ni miongoni mwa madansa waliojipatia umaarufu mkubwa katika miaka ya 2000 hasa kutokana na aina ya mtindo waliouanzisha. Sunche na Kapeto (Pichani) ndio ninaowazungumzia leo, nimewamisi sana, ni jamaa zangu wa karibu wote wawili. Wenyewe wamenigeuza ndugu yao, mara nyingi nimekuwa nao karibu, walianza kucheza kwenye kumbi za starehe na wikiendi hufanya shoo ya nguvu, miaka iliyopita wakati tasnia hiyo ilipokuwa na mashindano yake kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa hadi Taifa, madansa hao ndio walipoibukia. Walishiriki mashindano hayo kwa kutumia majina ya Big Cut (Kapeto) ambaye ni Kurwa na Small Cut (Sunche) ambaye ni Dotto. Walifanya vizuri ingawa hawakuwa kuwa mabingwa wa taifa, baadaye waliamua kuachana na majina hayo na kujiita Sunche na Kapeto, walijipatia umaarufu mkubwa. Baada ya fani ya udansa ilipoanza kudorola, Sunche na Kapeto wakajiunga na Tanzania One Theatle (TOT) iliyokuwa ikiongozwa na marehemu John Komba, TOT Plus Band ilitamba mno hasa

Bocco apelekwa Afrika Kusini

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Nahodha na mshambuliaji wa Azam FC John Bocco "Adebayor" anapelekwa nchini Afrika Kusini kutibiwa goti linalomsumbua kwa muda mrefu baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba SC. Bocco aliumia katika mchezo huo licha ya Azam kushinda bao 1-0 goli ambalo lilifungwa naye, Afisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd Maganga amesema Bocco atapelekwa Afrika Kusini kufanyiwa matibabu. Maganga pia amesema mbali na Bocco, Azam ina majeruhi wengine ambao ni Agrey Morris na Mcameroon Stephen Kingue, Azam imetolewa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuchapwa jumla ya mabao 3-1

Jeuri ya Manji kurejea upya Jangwani

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Baada ya Mahakama kuu ya Tanzania kumrejesha uraiani mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji na kutakiwa kuendelea na shughuri zake za kawaida, imebainika kuwa kibopa huyo wa Quality Group anarejesha tena jeuri Jangwani. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimesema kwa sasa Manji bado mgonjwa na anaendelea na matibabu katika hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam lakini bosi huyo amepanga kumwaga noti za maana Jangwani ili kurudisha morali kwa wachezaji. Manji ameumizwa sana na suala la kuhusishwa na matumizi ya unga na alikasirishwa zaidi kwa kitendo cha kuendelea kushikiliwa na serikali muda wote mpaka pale mahakama ilipotoa mwongozo kuwa yuko huru na hapaswi kushikiliwa. Akaunti za kibopa huyo zimeachiwa ina maana fedha sasa zitaanza kumiminika Jangwani kama ilivyokuwa nyuma, Manji anataka kuona ubingwa wa bara unaendelea kubaki Jangwani, kilisema chanzo hicho

YANGA NA WAARABU TENA

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Dar Young Africans maarufu Yanga SC wamepangwa tena na timu za Afrika ya Kaskazini katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga imepangwa na Moulodia Club Alger ya Algeria katika mchujo wa kufuzu hatua ya makundi inayishirikisha timu 16, Yanga imejikuta ikiangukia michuano hiyo baada ya kutolewa kwenye Ligi ya mabingwa Afrika na Zanaco ya Zambia kwa goli la ugenini. Yanga imekuwa na bahati mbaya hasa inapokutana na timu za Kiarabu na mara zote imekuwa ikitolewa, kwa maana hiyo Yanga inaweza kuishia hapo kwani matumaini finyu ya kuwang' oa Waarabu

Jerry Muro amtilia shaka Lwandamina

Picha
Na Shafih Matuwa. Dar es Salaam Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga SC ambaye amesimamishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jerry Colnery Muro amefunguka juu ya uwezo wa kocha Mzambia George Lwandamina. Muro ambaye adhabu yake inamalizika Mei mwaka huu, amedai hakuna dhambi kubwa itakayowatafuna Wanayanga ni kuondoka kwa Mholanzi Hans Van der Pluijm aliyeipa mafanikio timu hiyo. Msemaji huyo mwenye maneno ya kejeli hasa kwa mahasimu wao Simba, amedai kuna tofauti kubwa kati ya Hans na Lwandamina ambapo amedai Lwandamina ni kocha mzuri lakini hawezi kuisaidia Yanga kwa mfumo wake. "Mfumo wa Lwandamina haueleweki kabisa, Yanga hawachezi, angalia timu imeshindwa kuzifunga Azam, Simba na Mtibwa ambazo ndio washindani wa Yanga, pia Yanga imeshindwa kwenye michuano ya kimataifa, Yanga itamkumbuka sana Hans", amesema Muro huku akichukizwa na matokeo mabaya ya timu

Azam FC yatupwa nje kombe la Shirikisho, yapigwa 3-0

Picha
Na Mrisho Hassan. Mbabane Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika (CC) Azam FC jioni ya leo imetupwa nje ya michuano hiyo baada ya kubutuliwa mabao 3-0 na wenyeji wao Mbabane Swallors ya Swaziland. Matokeo hayo yanaifanya Azam FC itolewe kwa jumla ya mabao 3-1 kufuatia ushindi wa 1-0 ilioupata jijini Dar es Salaam, katika mchezo wa leo Azam walicheza vizuri na kwa maelewano lakini wakajikuta wakipotea mchezoni baada ya kufungwa bao la kwanza. Mabingwa hao wa kombe la Mapinduzi sasa watahamishia nguvu zao kwenye Ligi Kuu Bara na michuano ya Azam Sports Federation Cup ambao wameingia robo fainali

Simba yaifuata Mbao nusu fainali

Picha
Na David Pasko. Arusha Goli lililofungwa katika kipindi cha pili na mshambuliaji wa kimataifa raia wa Burundi Laudit Mavugo limeipa Simba ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Madini FC ya Arusha na kufanikiwa kuingia nusu fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup. Mechi hiyo ilipigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta ikiudhuriwa na maelfu ya watazamaji waliotokea mikoa jirani ikiwemo Dar es Salaam. Vijana wa Madini walucheza vizuri na kuelewana vema na kufanikiwa kuidhibiti Simba katika kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana, kipindi cha pili Simba iliamua kufanya mabadiliko ambayo yalileta nguvu mpya na kupata bao la ushindi. Simba sasa imeingia nusu fainali na inakuwa timu ya pili kufanya hivyo kwani jana timu ya Mbao FC iliingia nusu fainali baada ya kuilaza Kagera Sugar mabao 2-1, Yanga itacheza na Prisons hatua ya robo fainali ili kuungana na Mbao na Simba

Yanga waondoshwa kwa bao la ugenini

Picha
Na Mshamu Hassan. Lusaka Yanga SC imeondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kutoka sare ya 0-0 na wenyeji wao Zanaco mchezo wa marudiano uliopigwa katika uwanja wa Mashujaa. Kwa maana hiyo Yanga inaangukia kombe la Shirikisho ikianzia kucheza mechi mbili kabla ya kufuzu hatua ya makundi inayoshirikisha timu 16. Washambuliaji wa Yanga Simon Msuva na Obrey Chirwa walishindwa kuwatoka mabeki wa Zanaco ambao walikuwa wakiitafuta sare hiyo tasa ili wasonge mbele, Yanga inayonolewa na Mzambia George Lwandamina imeshindwa kuweka rekodi ya kuvuka makundi kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Mholanzi Hans Van der Pluijm

Yanga kuanza kwa mashambulizi

Picha
Na Msham Hassan. LUSAKA Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Dar Young Africans maarufu Yanga SC jioni ya leo inashuka Uwanja wa Mashujaa mjini Lusaka kurudiana na Zanaco mchezo wa hatua ya 32 bora ya Ligi ya mabingwa barani Afrika. Katika mchezo huo Yanga itaanza kwa kushambulia mwanzo mwisho ili angalau kupata bao la ugenini na ikiwezekana kushinda mchezo huo, katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam, Zanaco iliilazimisha sare ya kufungana 1-1 Yanga. Hivyo katika mchezo wa leo Yanga inahitaji ushindi wa aina yoyote kitendo ambacho kinaifanya mechi hiyo ionekane kali na ya kusisimua, Yanga huenda ikaanza na Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Geofrey Mwashiuya na Obrey Chirwa ambao watacheza kwa kushambulia zaidi ingawa wapinzani wao wanaonekana ni wazuri mno wakiwa nyumbani

Jeshi la Azam mguu sawa Swaziland

Picha
Na Mrisho Hassan. Mbabane Kikosi cha Azam FC kesho kinajitupa uwanjani kurudiana na Mbabane Swallors ya Swaziland mchezo wa hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Azam FC inaingia uwanjani ikiwa na mtaji wa bao moja ililolipata Uwanja wa Azam Complex zilipokutana katika mchezo wa mkondo wa kwanza. Mchezo wa kesho Azam inahitaji sare ya aina yoyote na ikivuka kigingi hicho itaumana na moja kati ya timu zilizoondolewa kwenye Ligi ya mabingwa Barani Afrika, Azam itamtegwmea zaidi winga Ramadhan Singano ambaye ndiye aliyefunga bao katika mchezo wa kwanza

Serengeti Boys wapangwa na Mali, Angola na Niger, Afcon

Picha
Na Mwandishi Wetu Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 maarufu Serengeti Boys imepangwa kundi B katika fainali za mataifa ya Afrika KWA vijana wa umri huo yanayotarajia kuanza huko Gabon. Serengeti Boys imeoangwa pamoja na Angola, Niger na Mali ambayo huenda isishiriki fainali hizo kwakuwa imefungiwa na Shirikisho la mpira wa miguu Barani Afrika (CAF). Kufungiwa kwa Mali kunaweza kuipa ahueni Serengeti Boys ambapo sasa itahitaji kushinda mechi zake mbili tu ili ijihakikishie kushiriki fainali za kombe la Dunia kwa vijana zitakazofanyika India baadaye

Hayatou atupwa nje CAF

Picha
Hatimaye aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika, Issa Hayatou raia Cameroon ameangushwa na mpinzani wake Ahmed Ahmed wa Madagascar katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho hilo. Hayatou amdhudumu CAF kwa miongo kadhaa iliyopita amejikuta akiondoshwa kwenye madaraka hayo baada ya kupigiwa kura 20 huku mshindani wake mkuu Ahmad Ahmad akipata kura 34 zilizomwezesha kushinda kiti hicho. Ahmad Ahmad mara baada ya kutangazwa kama mshindi wa uchaguzi huo ameahidi kuendeleza soka barani Afrika kama alivyokuwa akifanya mtangulizi wake, haya ni mabadiliko makubwa kabisa kufanywa katika medani ya uongozi na yameshitua

Singida United yampa mikoba Pluijm naye aanza kazi rasmi

Picha
Na Paskal Beatus. Dar es Salaam Aliyekuwa kocha na mkurugenzi wa ufundi wa Yanga SC, Hans Van der Pluijm amejiunga na timu iliyopanda Ligi Kuu ya Singida United ya mkoani Singida ambayo inahudumiwa kwa ukaribu zaidi na Waziri wa mambo ya ndani Mhe Mwigulu Nchemba (MB). Pluijm ameteuliwa kukinoa kikosi hicho kinachovaa uzi wa njano kama Yanga, ambapo pia ameanza kufanya usajili wa wachezaji akiwaandaa kwa msimu ujao, Singida United imepanda Ligi Kuu sambamba na Njombe Mji na Lipuli ya Iringa, kocha huyo wa zamani wa Berekum Chelsea ya Ghana anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili

Zanzibar yapata uanachama Caf

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika, Caf limeipa uanachama wa kudumu Zanzibar leo katika mkutano wake unaoendelea. Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Alfred Lucas Mapunda amesema Zanzibar imepewa uanachama na Caf hivyo sasa Tanzania itawakilishwa na timu mbili za taifa katika michuano ya Afrika. "Zanzibar itashiriki michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON) kwa wakubwa na pia kwa vijana, kwa maana hiyo uteuzi wa timu ya taifa, Taifa Stars itakayoshiriki michezo ya Afrika haitahusisha wachezaji wa Zanzibar", alisema Lucas. Awali Zanzibar ilikuwa mwanachama wa muda wa Caf ambapo uliwezesha vilabu vyake kushiriki michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika (Cal) na kombe la Shirikisho Afrika (CC)

TRA yafunga ofisi za TFF kisa deni la mamilioni

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Mamlaka ya kukusanya mapato Tanzania (TRA) imezifunga ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) ikidai mamilioni ya shilingi yanayosemekana tangu enzi za utawala wa aliyekuwa Rais Leodegar Tenga na sasa Jamal Malinzi. Madalali wa kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart walivamia ofisi za Tff na kuwatoa nje maofisa wote na wafanyakazi wa Tff nje ya ofisi hizo na kufunga, TRA inaidai TFF mamilioni ya shilingi ikidaiwa ni ya kodi. Fedha hizo zinasemekana ni makato ya kodi za makocha wa timu ya taifa, Taifa Stars ikianzia na Mbrazil Marcio Maximo, Jan Poulsen, Kim Poulsen na Mart Nooij, kufungwa kwa ofisi hizo za Tff zinaweza kuathili soka la Tanzania

Blagnon arejea Simba baada ya kudunda Oman

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba SC raia wa Ivory Coast Fredrick Blagnon hatimaye amerejea kwenye Klabu yake ya Simba baada ya kukataliwa Fanja FC ya Oman aliyojiunga nayo kwa mkopo. Taarifa zilizoifikia Mambo Uwanjani zinasema kuwa Blagnon amerejea Simba baada ya kushindwa kuwaridhisha Fanja ambao walimchukua kwa mkopo wa miezi sita. "Ni kweli Blagnon amerejea Simba na ataungana na wenzake kumalizia mechi za msimu", ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na uongozi wa Simba

Madini waapa kufa na Simba

Picha
Na David Pasko. Arusha Kocha mkuu wa timu ya Madini FC, Abdallah Juma amesema vijana wake wako fiti kuikabili Simba na wameapa kufia uwanjani siku ya Jumamosi. Simba inakutana na Madini mchezo wa robo fainali ya kombe la TFF maarufu Azam Sports Federation Cup, na Juma amedai vijana wake hawana mchecheto na wataendeleza kile walichokifanya kwa Panone, JKT Oljoro na JKT Ruvu. Kikosi hicho cha Madini ambacho kinashiriki Ligi Daraja la kwanza Tanzania Bara kimepania kushinda mchezo huo na kimedai Simba si tishio kwao ni timu ya kawaida kama zilivyo nyingine

Rais Magufuli ampa tano Diamond Platinum

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli jana alimpigia simu mwanamuziki nyota nchini Naseeb Abdul "Diamond Platinumz" na kumpongeza alipokuwa live katika kipindi cha Tv Clouds. Mheshimiwa rais Magufuli alilazimika kupiga simu na kumpongeza Diamond kutokana na jitihada zake kwenye muziki na kuitangaza Tanzania kimataifa, Magufuli amedai Diamond amekuwa balozi mzuri kwa taifa letu nje mipaka na atashikamana naye bega kwa bega. Naye msanii Diamond amemuomba Rais Magufuli kuisaidia tasnia ya muziki ili waendelee na shughuri hiyo kwani imekuwa ikiwapatia kipato na kuendesha maisha yao ya kila siku, Diamond amekuwa akifanya vizuri kwenye muziki na akishirikiana na wanamuziki wakubwa duniani

Simba waitisha Madini, wapiga tizi kali

Picha
Na David Pasko. Arusha Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba SC kimetua salama jijini Arusha jana na kupata mapokezi makubwa ambapo mashabiki wengi walijitokeza kwenda kuilaki, na jana hiyo hiyo walianza mazoezi mepesi na leo wakaendelea kupiga tizi. Simba SC watashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta kuchuana na Madini FC ya hapa Arusha mchezo wa Robo fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup, mechi itachezwa Jumamosi. Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange Hiliki "Kaburu" amesema kikosi chake kimepania kupata ushindi katika mchezo huo kwani sasa hawataidharau timu yoyote watakayokutana nayo hasa kwa zile zinazozaniwa ni ndogo. "Kwenye Football hakuna timu ndogo wala changa, timu zote ni sawa isipokuwa kuna zile zenye mashabiki wengi na zisizo na mashabiki, ila Madini hatutaidharau kwani imeweza kuingia hatua kubwa kama hii, tutawapiga kama Polisi Dodoma". Alisema Kaburu

HASSAN KABUNDA MCHEZAJI BORA VPL FEBRUALI

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Kiungo mshambuliaji wa Mwadui FV ya Shinyanga, Hassan Salum Kabunda amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mwezi Februali mwaka huu. Kabunda ambaye ni mtoto wa beki wa zamani wa Yanga SC, Salum Kabunda "Ninja" au Msudan anechaguliwa kuwa mwanasoka bora wa mwezi Februali baada ya kuwashinda Mrundi Laudit Mavugo na mzalendo Ibrahim Ajibu wote wa Simba. Kabunda ameisaidia Mwadui kushinda mechi mbili mfululizo huku yeye akifunga mabao manne katika mechi tatu alizocheza kwa mwezi huo Februali, kiungo ambaye jana alijumuhishwa kwenye kikosi cha Taifa Stars na kocha mzalendo Salum Mayanga. Kabunda sasa atakabidhiwa kitita cha shilingi Milioni moja na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi Vodacom, Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas ndiye aliyetoa taarifa hizi kupitia mahojiano yake na waandishi wa habari leo

Taifa Stars mpya yatangazwa, Kessy ndani

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza kikosi chake kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki. Stars inaweza kucheza na kati ya Zambia au Rwanda ama timu nyingine yoyote kwakuwa kumekuwa na taarifa tofauti. Lakini kikosi cha Mayanga kitaongozwa na nahodha wake Mbwana Ally Samatta anayekipiga nchini Ubelgiji katika klabu ya KRC Genk na pia kina vijana wengi zaidi. Kikosi hicho ni kama ifuatavyo: Makipa Aishi Manula (Azam FC), Deogratus Munishi "Dida" (Yanga SC), na Said Mohamed (Mtibwa Sugar). Mabeki Shomary Kapombe (Azam FC), Hassan Kessy (Yanga SC), Mohamed Hussein "Tshabalala" (Simba SC), Gardiel Michael (Azam FC), Andrew Vincent (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni (Azam FC). Viungo Ni Himid Mao (Azam FC), Jonas Mkude (Simba SC), Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Frank Domayo "Chumvi" (Azam FC), Muzamiru Yassin (Simba SC), Simon Msuva (Yan

AZAM FC MWENDO MDUNDO, YAIDUWAZA MBABANE 1-0

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika Azam FC wameanza vizuri michuano hiyo kwa kuichapa Mbabane Swallors ya Swaziland kwa bao 1-0. Mechi hiyo ilipigwa kwenye uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam usiku, uliudhuriwa na mashabiki wengi waliotaka kuona Azam FC inamaliza kazi mapema. Hata hivyo, Azam FC ililazimika kusubiri kwenye robo ya nne ya dakika 90 yaani dakika ya 25 za mwisho kupata bao dhidi ya Mbabane ambao walikomaa hadi mwisho wa dakika 45 mambo yakiwa 0-0. Ushindi huo unailazimu Azam FC kuwa makini zaidi kulinda ushindi wake huo mfinyu itakapokuwa ugenini mjini Mbabane katika mechi ya pili itakayoamua matokeo. Bao lililoipa ushindi Azam lilifungwa na winga machachari Ramadhan Singano "Messi" ambalo sasa litaifanya Mbabane kushinda mabao mawili itakaporudiana majuma mawili

Azam FC kuwafuta machozi Watanzania

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Klabu bingwa Afrika mashariki na kati Azam FC usiku wa saa 1:15 wanatelemka uwanjani kuwavaa Mbabane Swallors ya Swaziland mchezo wa raundi ya kwanza kombe la Shirikisho barani Afrika. Mechi itapigwa katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi na vijana wa Azam wanataka kuwafuta machozi Watanzania hasa baada ya wawakilishi wengine wa Tanzania Dar Young Africans jana kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Azam FC, Jaffari Iddi Maganga amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mtanange wa leo na wamepanga kushinda ili kuwafuta machozi Watanzania, "Tunataka kushinda ili tukae katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya makundi", alisema Iddi ambaye alikuwa mtangazaji wa Radio One

Simba yaua Polisi Dodoma 3-0

Picha
Na Saida Salum. Dodoma Simba SC wameendelea kuwapa raha mashabiki wake baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji Polisi Dodoma uwanja wa Jamhuri mjini hapa. Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi Laudit Mavugo ameendelea kuwatesa makipa wa Tanzania baada ya kufunga bao la kwanza katika mchezo huo wa kirafiki jioni ya leo. Dakika 45 za kwanza zilimalizika Simba wakiwa mbele kwa bao moja, lakini kipindi cha pili wakaongeza mabao mawili kupitia kwa winga wake machachari Shiza Ramadhan Kichuya kwa penalti na mshambuliaji Juma Luizio Ndanda akafunga la tatu.

YANGA, ZANACO HAKUNA MBABE

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Yanga SC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Zanaco ya Zambia katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Matokeo hayo yanamaanisha Yanga watahitaji ushindi wa ugenini katika mchezo wa marudiano nchini Zambia ili kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo. Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa kutoka Djibout, Djamal Aden Abdi aliyesaidiwa na Hassan Yacin na Farhan Salime hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0. Bao hilo lilifungwa na winga machachari wa timu hiyo Simon Msuva dakika ya 39 baada ya kuwachambua mabeki wa Zanaco kufuatia pasi nzuri ya kiungo Mzambia Justin Zulu. Bao hilo lilikuja baada ya Yanga kubadilisha maarifa ya kuwashambulia Zanaco, kutokea pembeni hadi kuamua kuingia ndani ya eneo la hatari kwa kugongeana pasi. Kwa dakika zote 30 za awali. Zanaco wakafanikiwa kukomboa bao katika dakika ya 78 kupitia kwa mshambuliaji wake Mghana, Attram Kwame

Simba waapa kuifanyia mauaji Polisi Dodoma leo

Picha
Na Saida Salum. Dodoma Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC jioni ya leo nao wanajitupa katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa kucheza na timu ya maafande wa Polisi Dodoma mchezo wa kirafiki. Simba ambao waliwasili jana na kupokewa na maelfu ya wapenzi wa soka mjini hapa, walialikwa na chama cha soka mkoa Dodoma (DOREFA) wanacheza na Polisi Dodoma ambao wanashiriki Ligi Daraja la kwanza Tanzania Bara. Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Haji Manara amesema kikosi chake kimepania kuendeleza wimbi la ushindi bila kuangalia wanakutana na timu gani, Manara amedai Simba na Polisi Dodoma zimekuwa zikikamiana sana hasa zilipokuwa zinakutana kwenye Ligi Kuu Bara. Simba ipo Dodoma ikiwa njiani kuelekea Arusha ambapo mwishoni mwa wiki ijayo itacheza na Madini ya Arusha mchezo wa Robo fainali kombe la TFF

Muziki upo Taifa leo, Yanga vs Zanaco, Lwandamina aanza na Tambwe, Ngoma, Msuva na Chirwa

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara Dar Young Africans maarufu Yanga SC jioni ya leo inatelemka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwakaribisha majirani Zanaco ya Zambia mchezo wa hatia ya 32 Ligi ya mabingwa barani Afrika. Mabingwa hao wa Bara ambao kwa sasa wapo kwenye msoto wa fedha lakini wameahidi kupigana kufa au kupona ili kuweza kuchomoza na ushindi katika mchezo huo wa kwanza ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya makundi, endapo Yanga itafuzu makundi itaweza kujipatia mamilioni ya shilingi kutoka kwa wadhamini wa michuano hiyo. Mkufunzi mkuu wa Yanga Mzambia George Lwandamina amewaanzisha washambulizi wake hatari na tegemeo kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Bara mara 26 na tumaini kubwa kwa mashabiki hao, Lwandamina amesndelea kumuamini kipa Deogratus Munisi Dida akinpanga langoni huku akisaidiwa na mabeki Hassan Kessy, Haji Mwinyi, Nadir Haroub, Vincent Bossou na Thabani Kamusoko. Wengine Simon Msuva na

NGASA- NARUDI FANJA

Picha
Na Albert Babuu. Dar es Salaam Kiungo mshambuliaji wa Mbeya City Mrisho Khalfan Ngasa amesema atarejea tena Oman kujiunga na klabu yake ya Fanya inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Ngasa aliyejiunga na Fanja kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Free State Stars ya Afrika Kusini, aliamua kurejea nyumbani kujiunga na Mbeya City kufuatia kumalizika kwa pasipoti yake ya kusafiria ambapo ilimlazimu kurejea nchini ili kushughurikia tatizo hilo. "Ni kweli narudi Fanja FC ya Oman, milango imekamilika na kinachosubiriwa ni kumalizika mkataba wangu mwishoni mwa msimu, nilisaini mkataba mfupi ili niweze kurejea Oman kwa sababu nilikuja nyumbani kushughurikia hati yangu ya kusafiria", alisema Ngasa. Ngasa aliibukia kupitia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys mwaka 2004 baadaye akatamba na Toto Africans kabla hajasajiliwa na Kagera Sugar ambayo nayo ikampeleka Yanga SC, Ngasa aliuzwa kwa Azam FC

Chacha, Matandika washinda kesi yao ya rushwa

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Maofisa wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) wameshinda kesi yao ya tuhuma za rushwa iliyokuwa ikiwakabili, Juma Matandika ambaye ni msaidizi wa rais wa TFF Jamal Malinzi na Martin Chacha aliyekuwa mkurugenzi wao wa mashindano wa TFF walikuwa wanashutumiwa kuomba rushwa ya milioni 25 kwa viongozi wa Geita Gold Mine wameachiwa huru. Sauti zilizodaiwa kuwa ni zao zilisikika zikieleza mipango ya kusaidia Geita Gold na ilitakiwa fedha kwa ajili pia ya kuwapa viongozi wengine. Ingawa wadau wengi wanaojua sauti zao waliamini ni wao kabisa, lakini Mahakama ya Mkazi Kisutu imetupilia mbali ushahidi wa sauti uliowasilishwa mahakamani hapo

TANGAZO: HODI....HODI....HODI....ZANZIBAR

Picha
NI YULE YULE ALIYEWAACHA HOI RAIA WA NCHI ZA INDIA, CHINA, MAREKANI NA URUSI HADI WAKAMNG' ANG' ANIA ABAKI KWAO: CHIFU PANDUKA: Ni bingwa wa tiba asilia, amejibu maombi ya Wazanzibar ambao kwa muda mrefu walitamani ujio wake, CHIFU PANDUKA: Atakuwa Zanzibar kuanzia Jumatatu ijayo hadi Jumatano. CHIFU PANDUKA: Anaendelea kuonyesha miujiza yake kwa Dawa yake ya uzazi hasa kwa wanawake wasiopata ujauzito, yeye amekuwa akiwapa Dawa na baadaye kushika ujauzito, wengi wamepata watoto kwa ajili yake, basi usikose kwenda kumuona ili kujibu ndoa yako. CHIFU PANDUKA: Anazo Dawa nyingine mbalimbali kama za Nguvu za kiume, Magonjwa sugu, Kisukari, Presha, anakinga ya nyumba, mashamba na hata mali zako zisiibiwe. Kwa wavuvi CHIFU PANDUKA anayo Dawa ya bahati irakayokufanya uvue samaki wengi. CHIFU PANDUKA pia anayo Dawa ya mvuto wa biashara, acha kulalamika biashara yako haitoki, anayo Dawa inayoleta wateja pia anayo Dawa ya mvuto wa mapenzi kaa upendwi utapendwa, anatoa mikosi mwilini,

HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA YANGA, KUREJEA KWA MASTAA WAO

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Hizi ni habari njema hasa kwa mashabiki wa Yanga hasa baada ya daktari wa kikosi hicho Edward Bavu kuanika taarifa njema kwa afya za wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza ambao walikosekana kwenye kikosi cha kwanza baada ya majeraha ya muda mrefu na mfupi. Bavu ameanika afya ya mshambulizi raia wa Zimbabwe Donald Dombo Ngoma kuwa sasa anaweza kurejea uwanjani kwenye michezo ijayo ukiwemo wa marudiano dhidi ya Zanaco ya Zambia. Mbali na Ngoma, Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko nao wako fiti kabisa na huenda katika mchezo wao dhidi ya Zanaco utakaochezwa Jumamosi ijayo kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam nyota hao watacheza kama kocha George Lwandamina ataamua kuwapanga katika kikosi chake. Hizo ni taarifa njema kabisa kwa mashabiki wa Yanga kwani kikosi hicho kilionekana kupungua makali hasa baada ya kushindwa kuwatumia nyota hao, Lakini hata hivyo Yanga haikuteteleka kwani iliweza kuifunga Kiluvya United mabao 6-1 na kuingia robo fainali ya kombe la T

Kagera Sugar wasema wataisimamisha Simba

Picha
Na Mwandishi Wetu. Bukoba Kocha mkuu wa Kagera Sugar Mecky Mexime amesema kikosi chake hakitakubali kugeuzwa ngazi ya kuelekea kwenye ubingwa na Wekundu wa Msimbazi Simba SC watakapokutana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Mexime ameyasema hayo mapema kuelekea katika mchezo huo ambao utapigwa katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Mexime amedai anaifahamu vizuri Simba na hatishwi na soka lao hivyo amewataka wapenzi na mashabiki wa Kagera Sugar kuwa na uhakika wa ushindi. Mexime amedai Kagera Sugar inataka kumaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu hivyo ni lazima washinde mechi zao za mwisho hasa wanazochezea uwanja wa nyumbani, "Kwa sasa tunataka kukamata nafasi ya tatu, najua ukiwa mshindi wa tatu unapewa zawadi hivyo tuna uhakika mkubwa wa kuchukua kitita cha wadhamini", amesema Mexime, Simba na Kagera Sugar zitakutana hivi karibuni

Zanaco waja kuendeleza ubabe kwa Yanga

Picha
Na Paskal Beatus. Dar es Salaam Wawakilishi wa Zambia katika michuano ya Afrika, Zanaco imwasili nchini leo tayari kwa kibarua kizito dhidi ya wawakilishi wa Tanzania Yanga SC kwenye michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika. Mchezo wa raundi ya kwanza Ligi ya mabingwa barani Afrika kati ya Yanga na Zanaco utachezwa mwishoni mwa wiki hii na tayari Zanaco wameshatua nchini kwa ajili ya mpambano huo, Hii ni mechi ya kisasi kwani mwaka 2006 Zanaco iliitoa Yanga katika michuano kama hiyo. Yanga ilitolewa kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam kulazimishwa sare ya 2-2 na kisha kulala 1-0 Zambia, hata hivyo mechi hiyo itakayopigwa uwanja wa Taifa itaonyeshwa Live na Azam TV na tayari Yanga imeshauza haki za matangazo

Mwanjali bado bado sana kurejea uwanjani

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Simba SC bado itaendelea kumkosa mlinzi wake wa kati Mzimbabwe Method Mwanjali aliyeumia hivi karibuni na kukosa mechi kadhaa za mashindano. Daktari wa Simba Yassin Gembe amesema mchezaji huyo anaweza kurejea uwanjani mwezi ujao na sasa tayari ameanza mazoezi mepesi mepesi ingawa bado hali yake haijatengamaa. Kukosekana kwa Mwanjali kumeweza kusababisha ukuta wa Simba kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara kwa mara, Mwanjali amesababisha pengo kubwa kwenye safu ya ulinzi ya Simba ambayo imeruhusu mabao manne ikicheza mechi kadhaa za Ligi Kuu ya Bara na kombe la TFF

CONTE AWATAKA CHELSEA KUTOBWETEKA

Picha
Mkufunzi mkuu wa Chelsea ya England Antoine Conte amewataka wachezaji wake kutobweteka na matokeo na badala yake kukaza kila wabapokutana na timu pinzani licha kwamba wako kileleni kwa uwiano wa pointi 10 na washindani wao wakuu kwenye mbio hizo Tottenham Hotspur. Chelsea waliifunga West Ham mabao 2-1 lakini amegundua kuwepo ushindani mkubwa kwa kila timu inayokutana nayo, amedai vilabu hukamia mno ili kuwashinda lakini amewataka vijana wake kupambana hadi tone la mwisho kwani wakibweteka wanaweza kupokwa uongozi . Mkufunzi huyo anaamini kupambana kwa vijana wake kutawafanya waendelee kuwa kileleni kwani hadi sasa wanaongoza kwa tofauti ya pointi 10 dhidi ya wapinzani wao Tottenham Hotspur

Mdaula United wasaka timu ya kucheza nayo Dar

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Timu ya Mdaula United ya Mdaula wilayani Chalinze mkoani Pwani iko katika mchakato wa kusaka timu ya kucheza nayo mechi ya kirafiki itakapoanza ziara yake ya kimichezo jijini Dar es Salaam. Kocha na mhamasishaji wa Mdaula United, Shaaban Kipresha ameiambia Mambo Uwanjani kwa simu kuwa vijana wake ambao wanashiriki Ligi Daraja la tatu mkoani Pwani wanataka kuwasili Dar es Salaam ambapo wanahitaji angalau mechi moja kabambe ya kujipima nguvu. "Ni kweli tunakuja Dar es Salaam hasa baada ya kumaliza ziara yetu hapa Mlandizi, tumecheza na Mlandizi Worriors na kushinda _4-3 mchezo wa kirafiki, lengo letu tuje Dar na tucheze mechi moja ya kirafiki na timu yenye ushindani", alisema Kipresha mchezaji wa zamani wa Baghdad na Big Bonn zote za Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam

Yanga yaitumia salamu Zanaco, yaisurubu Kiluvya United 6-1

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Yanga SC imefanikiwa kuingia robo fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup kwa uahindi mnono wa mabao 6-1 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya Kiluvya United ya Dar es Salaam mchezo wa kukamilisha hatua ya 16. Katika mchezo huo wa upande mmoja, Yanga iliandika mabao yake kupitia kwa mshambuliaji wake Mzambia Obrey Chirwa aliyefunga magoli manne peke yake na kuvunja rekodi ya Mrundi Amissi Tambwe aliyewahi kufunga magoli manne. Magoli mengine yalifungwa na Geofrey Mwashiuya na Juma Mahadhi wakati lile la Kiluvya United lilifungwa na Edgar Charles baada ya kumtambuka beki wa Yanga Mtogo Vincent Bossou, kwa ushindi huo Yanga itakutana na Tanzania Prisons hatua ya robo fainali katika uwanja wa Taifa. Pia ushindi huo ni salamu kwa wapinzani wao Zanaco ya Zambia ambao watakutana nao Jumapili mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika raundi ya kwanza, mechi hiyo itapigwa Jumapili ijayo

Yanga kujiuliza kwa Kiluvya United

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara na mabingwa watetezi wa kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu kombe la TFF Yanga SC wanashuka dimbani kuwavaa Kiluvya United katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Mchezo huo wa robo fainali ya kombe la Azam unatarajia kuwa mkali na wa kusisimua hasa kutokana na Kiluvya United kutaka kuikamia zaidi Yanga ambao ni miamba ya soka nchini. Mechi hiyo inachezwa Jumanne na Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema mchezo utakuwa mgumu kwakuwa wapinzani wao hawatakubali kupoteza, "Timu ndogo zinapokutana na timu kubwa huwa shughuri pevu kwani zinakamia sana", alisema Mkwasa ambaye kitaaluma ni kocha

Simba yapata mwaliko Dodoma

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC wamepata mwaliko maalum kutoka kwa chama cha soka mkoani Dodoma (DOREFA) na watacheza mechi ya kirafiki Jumamosi ijayo tarehe 11/3/2017. Haji Sunday Manara ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo amesema klabu yake imealikwa na DOREFA kwa lengo la kwenda kuwasabahi wakazi wa Dodoma. Manara amedai Simba ina mashabiki wengi Dodoma na kwa bahati mbaya mkoa huo hauna timu ya Ligi Kuu hivyo wamekosa kuona mechi zao kwa muda mrefu, Manara amesema Simba itacheza na Polisi Dodoma siku ya Jumamosi katika uwanja wa Jamhuri. Wekundu hao ambao wanaongoza ligi hiyo kwa pointi 55 itatumia ziara hiyo kujiweka sawa na ligi ambayo itasimama kwa wiki moja, Manara amedai Simba itasafiri na wachezaji wake wote

Azam FC sasa kugeukia kimataifa

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam FC sasa inageukia anga za kimataifa baada ya usiku wa kuamkia jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex uliopo Chamazi. Kikosi hicho kitashuka dimbani Machi 12 katika uwanja wao wa Azam Complex kuchuana na wageni wao Mbabane Swallors ya Swaziland mchezo wa raundi ya kwanza kombe la Shirikisho barani Afrika. Mtendaji mkuu wa Azam Saad Kawemba ameiambia Mambo Uwanjani leo kuwa Azam iko kamili kwa kuliwakilisha vema taifa na itafanya kweli katika michuano hiyo inayoshika nafasi ya pili kwa ukubwa barani Afrika kwa upande aa vilabu

MKWASA AAPA KUWABAKISHA NGOMA, BOSSOU

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Yanga SC kesho inatupa karata yake nyingine ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC)  maarufu kombe la TFF itakapocheza na Kiluvya United mchezo wa robo fainali Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ameanza kwa kuwaomba radhi mashabiki na wapenzi wa Yanga hasa baada ya kikosi chao jana kulazimishwa sare na Mtibwa Sugar mchezo wa Ligi Kuu Bara. Mchezo huo ulifanyika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, lakini Mkwasa akatumia nafasi hiyo kuwaambia Wanayanga kuwa licha kwamba wanapitia msoto mkali lakini anajotahidi angalau kuwabakisha mastaa wote wa kikosi cha kwanza wanaomaljza mikataba yao. Mkwasa amesema atawabakisha Donald Ngoma, Thaban Kamusoko raia wa Zimbabwe ambao mikataba yao inamalizika, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda, Amissi Tambwe Burundi na Vincent Bossou raia wa Togo, nyota hao wote wataendelea kukipiga Yanga alisema Mkwasa ambaye amewahi kuichezea timu hiyo na baadaye kuwa kocha kwa vipindi to

Yanga yashindwa kuing' oa Simba kileleni

Picha
Na Ikram Khamees. Morogoro Winga Simon Msuva ameshindwa kuiweka kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kukosa penalti Yanga ikishindwa kuondoka na pointi tatu katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Timu hizo zilitoshana nguvu baada ya kutoka sare tasa ya 0-0 na kuofanya Yanga kuambulia pointi moja inayowasogeza kidogo ikifikisha pointi 53 nyuma ya Simba kwa tofauti ya pointi mbili. Yanga sasa itakuwa na kibarua kingine Jumatano ijayo itakapocheza na Kiluvya United mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup

Nay wa Mitego asema hakuna wa kumzuia asianzishe kanisa lake

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Emmanuel Elibarik maarufu Nay wa Mitego amesema hakuna mtu yeyote wa kumzuia asianzishe kanisa lake la uponyaji mara tu atakapoamua kufanya hivyo. Nay wa Mitego amesema Mzee wa Upako hawezi kumzuia adianzishe kanisa kwakuwa hata yeye ameanzisha kanisa na hakukuwa na mtu wa kumzuia. Msanii huyo amepanga kuanzisha kanisa mara baada ya kuachana na muziki, "Kwa sasa bado nafanya muziki wa kidunia, ila nitakapoona inatosha basi nitafungua kanisa langu na kumtumikia Mungu", msanii huyo anayetamba na wimbo wa "Muda wetu". Hivi karibuni Mzee wa Upako alisema endapo Nay ataanzisha kanisa lake basi atamshitaki, lakini Nay amemjibu kwakusema hakuna mtu mwenye uwezo wa kumzuia asifungue kanisa lake