BIASHARA MARA YANASA BEKI KISIKI WA SIMBA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Timu ya Biashara United ya mkoani Mara ambayo imepanda Ligi Kuu imekamilisha usajili wa beki wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc, Meshack Abel na kumpa mkataba wa miaka miwili.
Beki huyo wa kati aliyewahi pia kuzichezea African Lyon na Bandari ya Mombasa nchini Kenya amejiunga na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.
Biashara United tayari imeshawasajili wachezaji wengine watatu hivyo imekuwa katika kipindi kizuri cha kujiimarisha kwani ujio wa beki huyo ni mwanzo wa kufanya vizuri msimu ujao, Meshack alitikisa alipokuwa Simba kutokana na umahiri wake