Machapisho

Azam FC itakutana na ZED FC kombe la Shirikisho

Picha
Azam FC itakutana na ZED FC, katika raundi ya pili ya awali ya CAF Confederation Cup. ZED FC imefanikiwa kutinga hatua hii baada ya kupata ushindi wa jumla ya mabao 5-1 dhidi ya Asas Djibouti.

TRA United yapata ushindi wa kwanza Ligi Kuu

Picha
Timu ya TRA United ya mkoani Tabora imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 mchezo wa Ligi Kuu bara katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Magoli ya TRA United yamefungwa na Emmanuel Mwanengo, Nonyem Okorocha ambaye amejifunga na Anni Elija. Goli la Pamba Jiji limefungwa na Abdulkarim Yunusi, hali si nzuri kwa Pamba Jiji ikiendelea kufanya vibaya msimu huu, lakini huu ni ushindi wa kwanza kwa TRA United kuupata tangia kuanza ligi

Singida BS yafanya balaa kombe la Shirikisho

Picha
Timu ya Singida Black Stars ya Tanzania imetinga raundi ya kwanza kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuilaza Al Ghazala ya Sudan Kusini kwa jumla ya mabao 10-1 kufuatia jioni ya leo kwenye uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam kushinda 3-0. Mabao yaliyoiwezesha timu hiyo kutinga hatua hiyo yamefungwa na Jonathan Sowah aliyefunga mawili na Henry David moja kwa matokeo hayo Singida BS inaenda kukutana na Tusker ya Kenya.

Simba yajipigia Mighty Wonderers 6-1

Picha
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika Simba jioni ya leo imetinga raundi ya kwanza kwa kibabe baada ya kuifunga Mighty Wonderers mabao 6-1 na kuhitimisha kwa jumla ya mabao 7-1. Ikishinda leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Simba iliandikisha mabao yake kupitia viungo washambuliaji wake Clatous Chama aliyefunga mabao mawili, Libasse Gueye naye mawili, Morice Abraham na Keletso Makgalwa. Bao pekee la Mighty Wonderers limefungwa kwa mkwaju wa penalti na Anold Emmanuel

Juma Mgunda shakani

Picha
Juma Mgunda amekuwa kocha wa kwanza mzawa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara 2026/27 kupoteza michezo 4 mfululizo ya ligi. Pia amekuwa kocha wa kwanza mzawa kupoteza michezo minne mfululizo ya ugenini msimu huu: 2️⃣-1️⃣ vs JKT Tanzania 3️⃣-2️⃣ vs Singida Black Stars 2️⃣-0️⃣ vs Azam FC 1️⃣-0️⃣ vs Dodoma Jiji Kwa mwenendo huu kocha Mgunda anajiweka shakani na kuiweka timu majaribuni

Kipa wa Azam FC azikwa

Picha
Taratibu za mwisho za maziko ya kipa wetu, Iddy Salim, zimefanyika jana saa 12 jioni Kata Mziha, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro. Pumzika kwa amani, Iddi Salim

CFFA FC mpinzani wa Yanga ajae

Picha
Baada ya Young Africans kufuzu kwa kuitoa Gaborone United ya Botswana kwa jumla ya mabao 3-2, sasa Yanga imepata mpinzani mwingine kutoka ukanda wa Afrika ya Kusini katika hatua ya pili ya mchujo wa CAF Champions League 2026/27. Yanga itakutana na CFFA ya Madagascar, ambayo imefuzu baada ya kuiondoa Lijabatho FC ya Lesotho kwa jumla ya mabao 3-1. CFFA ilishinda 2-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani, kabla ya kulazimisha sare ya 1-1 ugenini kwenye mchezo wa marudiano, na hivyo kusonga mbele kwa jula ya 3-1. Mchezo wa kwanza: CFFA vs Yanga Oktoba 16–18, 2026 Mchezo wa marudiano: Yanga vs CFFA Oktoba 23–25, 2026 Yanga itaanza kibarua hicho kwa kusafiri hadi Madagascar, kabla ya kurejea Tanzania kwa mchezo wa marudiano ambapo itatafuta tiketi ya kusonga mbele katika mashindano hayo.

Depu hakamatiki

Picha
Mshambuliaji Aurelio Laurindo Depu ameendelea kung’ara katika Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), baada ya kufunga bao na kutoa assist katika sare ya 2-2 kati ya Petro de Luanda na UD de Songo jana. Katika mchezo wa kwanza, Petro de Luanda ilishinda 1-0 dhidi ya UD de Songo, huku Depu akifunga bao pekee la mchezo. Kwa matokeo ya jumla ya 3-2, Depu amehusika moja kwa moja katika mabao yote matatu ya Petro de Luanda katika michezo hiyo miwili.

Aziz Ki amponza kocha Manqoba Yanga

Picha
Young Africans imefanikiwa kuifunga Gaborone United kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kufuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo. Hata hivyo, licha ya ushindi huo, baadhi ya mashabiki wa Yanga hawakuridhishwa na mwenendo wa kocha wao, Manqoba Mngqithi, hasa katika eneo la mabadiliko ya wachezaji. Uamuzi wa kumtoa Aziz Ki uliibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki, huku baadhi yao wakiona kuwa timu ilikosa ubunifu baada ya mabadiliko hayo. Baadhi ya mashabiki wameenda mbali zaidi kwa kutaka kocha huyo aondolewe, wakidai ameshindwa kuingia kwenye mfumo unaompa nafasi na kutumia ipasavyo uwezo wa Aziz Ki. Hata hivyo, pamoja na malalamiko hayo, Yanga imefanikiwa kupata ushindi na kusonga mbele katika mashindano hayo. Sasa Wananchi wanaelekeza nguvu zao kwenye maandalizi ya michezo inayofuata.

Akina Mayele wapeta Afrika

Picha
Al Ahli Tripoli imefanikiwa kutinga hatua ya pili ya awali ya CAF Confederation Cup baada ya kuiondosha KMKM ya Zanzibar kwa ushindi wa jumla ya mabao 7-0. Mchezo wa kwanza wa ugenini Al Ahli walishinda 3-0 na mchezo wa leo wa marudiano wameshinda 4-0. Fiston Mayele amefunga jumla ya magoli 3 kwenye michezo yote miwili. 

TP Mazembe hiyoo raundi ya kwanza

Picha
Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefuzu hatua ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) baada ya kuiondosha Medeama SC ya Ghana kwa matokeo ya jumla ya 4-1 kwenye hatua ya awali. TP Mazembe imechomoza na ushindi wa 3-1 kwenye mchezo wa marudiano uliopigwa Lubumbashi baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa huko Ghana wiki iliyopita. FT: TP Mazembe 🇨🇩 3-1 🇬🇭 Medeama SC ⚽ 03' Mwaungulu ⚽ 19' Kazema ⚽ 88' Mwaungulu ⚽ 90+2' Amponsah TIMU ZINGINE ZILIZOFUZU HATUA YA PILI: 🇿🇦 Orlando Pirates 🇸🇩 Al Merreikh SC 🇸🇩 Al Hilal Omdurman 🇸🇸 Al Merreikh Bentiu FC 🇿🇼 Scottland FC 🇲🇬 CFFA FC 🇲🇦 Maghreb Fez FC 🇦🇴 Petro de Luanda 🇳🇦 African Stars

Yanga yatinga raundi ya kwanza Ligi ya mabingwa Afrika

Picha
Mchezo wa marudiano hatua ya swali Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAF Champions League) kati ya klabu ya Yanga dhidi ya Gaborone United umemalizi kunako dimba la Azam Complex jijini Dar Es Salaam huku Yanga wakifuzu kwenda hatua ya pili kwa mabao (2-1). Mabao ya Yanga wamefungwa na Peter Shalulile na Sheikh Ibrahim Toure wakati goli la Goborone United limefungwa na Lebongang. Hivi sasa uwiano wa mabao ya jumla "Aggregate" ni (3-2).

Singida BS kukutana na Tusker kombe la Shirikisho

Picha
Iwapo Singida Black Stars watafanikiwa kufuzu kesho dhidi ya Al Ghazala Wau, watakutana na Tusker FC katika raundi ya pili ya awali ya CAF Confederation Cup. Tusker FC tayari imefuzu rasmi hatua hiyo baada ya kuiondosha Al Ahli Madani kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2.

Clara Luvanga aandika historia soka la wanawake duniani

Picha
Mchezaji wa Kimataifa wa Tanzania, Clara Luvanga, ameandika historia ya kuwa Mchezaji aliye sajiliwa kwa pesa Nyingi zaidi katika Historia ya soka la Wanawake Duniani baada ya kukamilika kwa uhamisho wa kujiunga na Washington Spirit ya Marekani akitokea Al-Nassr, kwa kusaini mkataba wa miaka minne utakaodumu hadi mwaka 2029. 𝐎𝐑𝐎𝐃𝐇𝐀 𝐘𝐀 𝐒𝐀𝐉𝐈𝐋𝐈 (4) 𝐆𝐇𝐀𝐋𝐈 𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐂𝐇𝐄𝐙𝐀𝐉𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐊𝐄 𝐃𝐔𝐍𝐈𝐀𝐍𝐈 1. Clara Luvanga kutoka: Al Nassr to Washington kwa ada ya €1.7m (tsh 5.2bilion). 2.Grace Geyoro kutoka PSG to London City €1.65m (tsh 5bilion). 3.Kerolin Nicoli kutoka Man City to Barcelona €1.5m (tsh 4.6 bilion). 4.Felicia Schröder Häcken to Real Madrid €1.5m (tsh 4.6bilion). Kwa kifupi Mtanzania Luvanga ndo mchezaji ghali kuliko wote Duniani.

Opah Clement naye asajiliwa Saudi Arabia

Picha
Kapteni wa timu ya taifa ya Tanzania, Twiga Stars, Opah Clement, amejiunga na klabu ya AlUla FC Women inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake Saudi Arabia. Opah amejiunga na AlUla akitokea SD Eibar ya Ligi Kuu nchini Hispania ambayo ameitumikia kwa msimu mmoja, huku klabu hiyo ya Alula ikiwa tayari imemtambulisha rasmi kama mchezaji wake mpya.

Harmonize aenda kumpa pole Samia Kizimkazi

Picha
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Rajab Abdul Kahali 'Harmonize' amefika kumpa pole na kumfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, leo Septemba 11, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan. Maalim Hafidh amefariki dunia Septemba 7, 2026 katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar.

Eto'o atuhumiwa kulamba bilioni 1.7

Picha
Samuel Eto’o yuko kikaangoni baada ya kupewa tuhuma za matumizi ya pesa hovyo. kwa taarifa kutoka vyanzo vya habari, vinaeleza kuwa nyota wa Barcelona, ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT), Kuna kiasi cha pesa fulani hakionekani, na kiwango hicho si chini ya takribani dola 665,000 [TZS bilioni 1.7], zilizohusishwa na malipo ya mchezo wa kirafiki kati ya Cameroon na Urusi mwaka 2023. Kufuatia sakata hilo, Eto’o, ambaye amekuwa akiongoza FECAFOOT tangu mwaka 2021, wataanza zoezi la uchunguzi dhidi ya jambo hilo linalomkabili. Kwa upande wa mshitakiwa ambaye ni Eto’o, amesema kuwa upande wake uko wazi kwa uchunguzi zaidi ili kuona wapi amekosea. Pia, nyaraka zake zote zitaanza kuchunguzwa, na kuripotiwa kuonyesha kuwa fedha hizo ziliagizwa kutumwa kwenye akaunti yake binafsi katika benki nchini Qatar.

Clara Luvanga atinga makao makuu Yanga

Picha
Mchezaji wa zamani wa Yanga Princess Clara Luvanga ambaye kwa sasa anacheza Ligi kuu nchini Marekani amemtembelea Rais wa Yanga SC Injinia Hersi Said ofisini na kuzungumza mambo mbali mbali kuhusu maendeleo ya mchezaji huyo siku hadi siku

Libasse Gueye ashinda tuzo ya mwezi NBC Primier League

Picha
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kupitia Kamati ya Tuzo za TFF imemtangaza kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Libasse Gueye, kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Agosti wa Ligi Kuu ya NBC (2026/27), huku kocha mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi, akitwaa tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi huo. Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Libasse Gueye, ametwaa tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango bora na kutoa mchango mkubwa katika michezo mitano ambayo Simba ilishinda yote. Akifunga bao moja na kuhusika kwenye mabao mengine matano (Assist 5) hivyo amehusika kwenye Magoli 6, Amewashinda Maxi Nzengeli (Young Africans) na Oscar Mwajanga (Mbeya City) walioingia naye fainali. Kocha wa Young Africans, Manqoba Mngqithi, amechaguliwa kuwa kocha bora baada ya kuiongoza timu yake kushinda michezo yote mitano na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi. Amewabwaga Steve Barker (Simba SC) na Florent Ibenge (Azam FC).

AS Maniema ziarani Tanzania

Picha
Jioni hii klabu ya AS Maniema Union,ya Congo DR imeanza safari ya kuja Tanzania. AS Maniema Union Wamealikwa na Azam Fc na watatua usiku wa leo. Lengo la timu hiyo kuja Tanzania ni kucheza mechi ya kirafiki na Azam FC.