Singida United nooma, yamnyakua rasta wa Mwadui
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Klabu ya Singida United ya mkoani Singida inazidi kujiimarisha katika zoezi LA usajili baada ya jana kufanikiwa kupata saini ya kiungo mahiri wa aliyekuwa timu ya Mwadui FC ya mjini Shinyanga, Awesu Awesu.
Mkurugenzj wa klabu hiyo Festo Sanga alimtambulisha mchezaji huyo mbele ya waandishi wa habari na kusema timu yake imedhamilia kufanya vema msimu ujao kwa kusajili wachezaji nyota.
Juzi Sanga aliwatambulisha wachezaji wengine watatu iliowasajili, wachezaji ambao walitambulishwa kusajiliwa na klabu hiyo ni Jamal Mwambeleko kutoka Simba SC, Athamas Mdamu kutoka Alliance School na Rajabu Zahir wa Ruvu Shooting