Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2016

Stand United yaituliza Yanga Kambarage

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Shinyanga Stand United ya Shinyanga jioni ya leo imeibuka na ushindi mbele ya mashabiki wake dhidi ya Yanga SC katika uwanja wa CCM Kambarage kwa bao 1-0 mchezo wa Ligi kuu bara. Kama si bahati Yanga leo wangeweza kubugizwa mabao matatu kwani kikosi cha Stand kimecheza vizuri na kulitia msukomsuko lango la Yanga. Yanga imefungwa bao hilo katika kipindi cha pili baada ya kazi nzuri ya Kevin Sabato, Yanga ililala mbele ya 'Maproo' wake Donald Ngoma raia wa Zimbabwe na Amissi Tambwe wa Burundi huku pia ikiwa na mastaa wake wengine

Serengeti Boys yaiangamiza Congo Brazavile, lakini njia panda

Picha
Na Ikram Khamees, Dar es Salaam Timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys jioni ya leo imeichakaza vibaya timu ya taifa ya Congo Brazaville mabao 3-2 uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa kufuzu fainali za mataifa Afrika. Stars ilitangulia kupata mabao yake katika kipindi cha kwanza yakifungwa mapema kabisa mawili, hadi mapumziko Serengeti ilikuwa mbele, kipindi cha pili Serengeti iliongeza la tatu wakati Congo Brazaville wakajipatia mabao yao mawili. Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Yohana Oscar Nkomola aliyefunga mawili katika dakika ya 43 na 45 kipindi cha kwanza, bao la tatu lilifungwa na Issa Abdi Makamba. Magoli ya Congo Blazaville yamefungwa na Langa Lasse kwa mkwaju wa penalti baada ya Mbaungou Prastige kuchezewa rafu na Israel Patrick, goli lingine lilifungwa na Bopoumela Chardon katika dakika ya 88 akimalizia krosi ya Ntota Gedeon

Ngoma, Tambwe waendeleza moto Yanga ikiitwanga Mwadui kwao

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Shinyanga Mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC, jana jioni walicharuka baada ya kuichabanga bila huruma Mwadui ya Shinyanga mabao 2-0 mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kambarage. Mwadui inayonolewa na Jamhuri Kihwelo "Julio" ilishindwa kabisa kuonyesha makeke yake kama iliyokuwa nayo msimu uliopita baada ya kukubali kipigo hicho mapema kabisa. Mfungaji bora wa msimu uliopita Amissi Joselyin Tambwe akawa wa kwanza kuifungia bao Yanga na hadi mapumziko wakawa mbele kwa bao hilo, kipindi cha pili Yanga wakaongeza bao la pili lililofungwa na Donald Ngoma. Goli hilo lilipatikana katika dakika za mwishoni kabla mpira haujamalizika, matokeo mengine, Tanzania Prisons na Mbeya City zilitoka sare 0-0, Mbao FC ikaichapa Ruvu Shooting 4-1, Ndanda FC ikaifunga Majimaji 2-1. Mechi nyingine Simba ikailaza Azam 1-0, Mtibwa Sugar ikailaza Kagera Sugar 2-0 wakati leo hii Stand United inacheza na JKT Ruvu

Simba yaipiga kidude kimoja Azam FC jana

Picha
Na Saida Salum, Dar es Salaam Simba SC jana jioni ilijiongezea pointi tatu muhimu baada ya kuilaza Azam FC bao 1-0 katika mchezo mkali wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo uliokuwa mgumu hasa kutokana na timu zote mbilj kuwa na upinzani mkali kila zinapokutana, hadi mapumziko Simba hawajapata kitu wala Azam inayonolewa na nakocha wa Hispania Zeben Hernanndez na msaidizi wake Jonas Garcia. Azam iliyokuwa na washambuliaji wake John Bocco "Adebayor" na Ronaldo Ya Thomas bado walishindwa kuupenya ukuta wa Simba uliokuwa ukilindwa vema na Method Mwanjali na Novat Lufunga, Shiza Kichuya, Laudit na Ibrahim Ajibu waliongoza safu ya ushambuliaji ya Simba. Lakini katika kipindi cha pili Shiza Ramadhan Kichuya akaipatia Simba bao la ushindi, Simba sasa iko kileleni ikiwa na pointi 13

Dante ajihakikishia namba Jangwani

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Shinyanga Kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans Van der Pluijm, amesema ataendelea kumuamini katika kikosi chake cha kwanza, beki wake Vincent Andrew 'Dante' kama anavyomuamini kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Boniface Mkwasa. Nyota ya Andrew Vicent 'Dante' inazidi kung'ara! Baada ya kucheza vizuri kwa dakika zote dhidi ya Nigeria akiitumikia Taifa Stars katika michuano ya AFCON,kocha mkuu Mkwasa amevutiwa mno na mchezaji huyo habari ni ile ile kwa kocha mkuu wa Yanga SC Hans Van Pluijm anayesema. . "Ni kijana mwenye juhudi na nidhamu kubwa sana, anaongoza kuondoa mipira yote ya juu japo kiumbo sio mrefu. .  Ntaendelea kumtumia na kumuamini, ana kipaji kikubwa sana atafika mbali kama ataendelea kuwa na nidhamu ya kipaji chake" alisema Pluijm

Simba yamuuza kinyemela Danny Lyanga

Picha
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam Klabu ya Simba ya Dar es Salaam, inadaiwa imemuuza mshambuliaji wake Danny Lyanga kwa klabu ya Oman SC ya Oman inayoshiriki Ligi kuu nchini humo. Hata hivyo, Mtendaji mkuu wa Wekundu hao wa Msimbazi, Patrick Kahemela amekataa vikali kuthibitisha hilo na kudai Lyanga hajauzwa isipokuwa ameenda Oman kufanya majaribio ma kama akikubalika anaweza kuuzwa. Lakini mshambuliaji huyo aliondoka mwezi uliopita kujiunga na timu hiyo na sasa ni mchezaji wa Oman SC lakini haijulikani kama amesaini mkataba wa muda gani huku ikidaiwa Simba ilimuuza kinyemela. Lyanga ni mmoja kati ya washambuliaji hatari waliofanya vizuri msimu uliopita akiwa na Simba  sambamba na Ibrahim Ajibu, Hamisi Kiiza na wengineo

Kipre Tchetche akwama Umangani, sasa anaingoja Yanga mwakani

Picha
Na Mwandishi Wetu Mfumania nyavu mwenye uwezo wa juu, Kipre Herman Tchetche hatimaye ameshindwa kuendelea kuichezea klabu ya Al Nahda ya Oman hasa baada ya uongozi wa timu hiyo kushindwa kumalizana na Azam. Taarifa zenye uhakika kutoka Oman zinasema kwamba mshambuliaji huyo aliyekuwa tegemeo katika kikosi cha Azam FC amerejea kwao Ivory Coast na hana mpango wowote wa kujiunga tena na Azam isipokuwa hesabu zake mwakani arejee nchini kujiunga na Yanga SC. Yanga wanamsubiri kwa hamu Tchetche kwani walikuwa wakimuwania kwa kipindi kirefu isipokuwa viongozi wa Azam walikuwa hawako tayari kumuachia aende mitaa ya Jangwani na Twiga

Ngasa aitosa Yanga, atimkia Oman

Picha
Na Saida Salum, Dar es Salaam Mshambuliajj wa zamani wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mrisho Halfan Ngasa ameikacha rasmi Yanga na kuamua kutimkia nchini Oman kujiunga na klabu kongwe ya Fanja inayoshiriki Ligi kuu. Ngasa ameondoka na ndege Alhamisi na anatazamiwa kuingia mkataba na timu hiyo, kabla hajaondoka, Ngasa alizungumza na mwandishi wa habari hizi kuwa ameshafanya mazungumzo na Fanja na wamemtumia tiketi ya ndege ili akamalizane nao. Fanja ni moja kati ya timu kongwe barani Asia ambapo Watanzania kadhaa wamewahi kuitumikia, mshambuliaji huyo wa zamani wa Toto Africans ya Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba, Yanga, Azam na Simba za Dar es Salaam alikuwa mbioni kurejea Yanga lakini ameamua kuikacha na kuelekea Oman, Mtandao huu unamtakia kila la kheri

Ukata wairejesha Yanga Kaunda

Picha
Na Prince Hoza Imebainika kwamba mabingwa wa soka nchini Yanga wameshindwa kuendelea kujifua kwenye uwanja wa Gymkhana au Boko Veteran baada ya mwenyekiti wao Yusuph Manji kukataa kulipia gharama kwa kile kinachodaiwa kukasilishwa. Manji amekacha kulipia gharama za kukodi viwanja baada ya kukataliwa kwa ombi lake la kutaka kuikodi Yanga kwa miaka kumi na inadaiwa amesitisha mpango huo. Pia baada ya Manji kususa, wachezaji wa timu hiyo bado hawajalipwa fedha zao na sasa wanacheza chini ya kiwango ili kutaka walipwe fedha zao, wakati hilo likiendelea, uongozi wa Yanga umejikuta ukiirudisha timu katika uwanja chakavu wa Kaunda kwavile hakuna uwezekano wa kufanyia mazoezi kwingine

Mwinyi Haji Ngwali akana kutumia dawa za kulevya

Picha
Na Mwandishi Wetu Beki wa kushoto wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC, Mwinyi Haji Ngwali amekanusha vikali kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na anawashangaa wale wote waliokuwa wakimzushia. Mwinyi ameshangazwa na watu waliokuwa wakimponda mitandaoni kwamba anatumia dawa za kulevya na ndio maana kiwango chake kilishuka, lakini mlinzi huyo amefichua kuwa kushuka kwa kiwango chake kulitokana na uchovu wa mwili na si madawa. Hata hivyo beki huyo kwa sasa amerejea kwenye kiwango chake kama zamani na sasa amerejeshwa tena kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars

Tshabalala azawadiwa gari na Hanspoppe

Picha
Na Prince Hoza, Dar es Salaam Beki wa kushoto wa Simba SC, Mohamed Hussein 'Tshabalala' ukipenda Zimbwe Jr amezawadiwa gari aina ya Ruum na mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Klabu ya Simba, Zackaria Hanspoppe leo asubuhi. Kiungo huyo wa ulinzi amezawadiwa gari hilo hasa baada ya kuonyesha kiwango kikubwa akiwa na timu hiyo inayoshikilia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Tshabalala amekuwa katika wakati mzuri tangu alipojiunga na timu hiyo misimu miwili iliyopita, beki huyo alipiga krosi mbili zilizozaa magoli wakati Simba ikiifunga Ndanda FC mabao 3-1 katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi kuu bara

Pan Africans waikana Yanga mchana kweupe, wasema hawana udugu nao

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Mwanachama wa Pan Africans FC ya Dar es Salaam, Abbas Ally Mwinyisimba, amesema Pan haina undugu na Yanga tofauti na watu wengi wanavyofahamu. Akizungumza hayo jana, Mwinyisimba amedai Pan Africans imetokea ubavuni kwa Yanga baada ya kutokea mgogoro mkubwa mwaka 1976 uliopelekea Yanga Raizon na Yanga Kandambili ambapo ndipo mgawanyiko huo ukazaa Pan Africans ambayo haina undugu tena na Yanga. "Hata mume akimuacha mkewe ndio basi tena huwezi kusema wana undugu, undugu ni pale wanapokuwa pamoja, sisi Pan hatuna undugu na Yanga isipokuwa tulitokea ubavuni mwao, hata Sunderland (Sasa Simba) nao walitokea ubavuni mwa Yanga lakini hawana undugu", alisema mwanachama huyo aliyekuwa akihamasisha wanachama wenzake kuudhuria mkutano mkuu unaofanyika leo Dar es Salaam. Pan Africans iliwahi kuwa mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara miaka iliyopita na ikawa moja kati ya timu tishio kwenye soka la Tanzania ikiwa na wachezaji mashuhuri kama Juma Pondamali &

Yanga yaikandika Majimaji 3-0 yakamata nafasi ya pili

Picha
Na Prince Hoza YANGA SC jioni ya leo imechupa kutoka nafasi ya saba hadi ya pili baada ya kuilaza Majimaji ya Songea mabao 3-0 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam mchezo wa Ligi kuu bara raundi ya tatu. Yanga iliandika kalamu ya mabao katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Donald Ngoma aliyemalizia kwa shuti kali mpira uliogonga mwamba uliotokana na penalti ya Simon Msuva. Msuva alipiga penalti mara tatu, mbili akifunga na mwamuzi akikataa, na moja aligongesha mwamba na Ngoma kumalizia, Akaunti ya magoli iliendelea kipindi cha pili ambapo Amissi Tambwe alifunga magolj mawili na kuifanya Yanga ifikishe pointi saba ikiwa imecheza mechi tatu, kesho Simba itacheza na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Uhuru

Kocha wa zamani wa Simba Afariki

Picha
Simba SC imeendelea kupatwa na misiba ya makocha wake wa zamani hasa baada ya kumpoteza kocha wake Mohamed Hassan Msomali, na jana usiku, James Agrey Siang' a amefariki dunia. Siang’a aliidakia timu ya Taifa ya Kenya mwaka 1972 katika fainali za mataifa ya Afrika. Siang’a aliifundisha timu ya Taifa Kenya kati ya mwaka 1999 na 2000. Baada ya hapo alikuja Tanzania akateuliwa kuifundisha Taifa Stars mwaka 2002. Siang’a alikwishapata vifundisha vilabu vya Simba SC na Moro United pia na Express ya Uganda.Octoba 2004, akiwa katika klabu ya Moro United, Siang’a aliteuliwa tena kuwa kocha wa Taifa Stars lakini alikataa wadhifa huo. Kabla ya kuifundisha Gor Mahia ya Kenya, ikumbukwe Siang'a alitokea Mtibwa Sugar ambayo ndiyo ilikuwa klabu yake ya mwisho kuifundisha hapa Tanzania. "Ni kweli tumempoteza ndugu yetu Siang'a. Amefariki ijumaa usiku kufuatana na taarifa tulizopewa na familia yake, tunasubiri taarifa zaidi kutoka kwao ili tujue nini kinaendelea. Mungu apumzishe ro

Coutinho arejea Yanga kuchukua nafasi ya Chirwa

Picha
Na Saida Salum, Dar es Salaam Andrey Coutinho yupo nchini kwa lengo kuu moja tu kuja kujaribu bahati yake ya kuitumikia Yanga SC kwa mara nyingine tena. . "Kama ukisikia nimerudi katika ligi kuu Tanzania basi jua nimerudi katika klabu nnayoipenda Yanga, siwezi kuichezea timu yoyote zaidi ya Yanga . . Nimegundua soka la Yanga linahitaji nguvu na akili, sasa nipo kamili! "Ntasubiri hapa kwa siku 5 kuangalia uwezekano wa kujisajili Yanga, nimepanga kesho kuwepo uwanjani kuwasalimia mashabiki na wachezaji wenzangu"alimalizia raia huyo wa Brazil. Coutinho amemaliza mkataba wake katika klabu ya Rakhine United FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Myanmar barani Asia akifanikiwa kutupia wavuni magoli 10. Haya ya Coutinho yakiendelea winga Mtanzania Mrisho Ngassa anaendelea kusotea ombi lake mara baada ya kuomba kurudi Yanga ili amalizie soka lake kiheshima katika klabu aipendayo. Ngassa ambaye alivunja mkataba na klabu yake ya Free State ya Afrika Kusini kwa kile kinachodaiwa kuwek

Ndanda yaikwamisha Yanga

Picha
Na Ikram Khamees, Mtwara Yanga SC mabingwa wa soka Tanzania bara, wamejikuta wakikwamishwa na vijana wa Ndanda FC baada ya kulaximishwa sare tasa 0-0 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Vijana wa Ndanda walionekana kuwadhibiti vilivyo Yanga katika kipindi cha kwanza wakipeleka mashambulizi langoni kwa Yanga na kama si umahiri wa kipa Ally Mustapha huenda Yanga ingelala. Hata hivyo Yanga itajilaumu wenyewr baada ya kukosa mabao ya wazi kupitia kwa washambuliaji wake Obrey Chirwa na Saimon Msuva, Yanga sasa imefikisha pointi nne ikiwa imecheza mechi mbili

Simba kusahihisha makosa kwa Ruvu Shooting leo?

Picha
Saida Salum, Dar es Salaam Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, jioni ya leo wanashuka uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuwakabili Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Simba wanataka kusahihisha makosa yao kwani katika mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu walilazimishwa sare tasa ya 0-0 hivyo leo hawatakubali kulazimishwa tena sare. Ikiwa chini ya washambuliaji wake Laudit Mavugo raia wa Burundi, Fredrick Blagnon raia wa Ivory Coast na Ibrahim Ajibu 'Kadabla' kwa vyovyote wataondoka na pointi tatu. Nao Ruvu Shooting ya Masau Bwire nayo itamtegemea zaidi kiungo wake mkongwe Shaaban Kisiga 'Marlone' ambaye aliwahi kuichezea Simba katika misimu kadhaa iliyopita

Yanga kuendeleza mauaji Mtwara

Picha
Na Ikram Khamees, Mtwara Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, Young Africans (Yanga) jioni wanashuka katika dimba la Nangwanda Sijaona mjini hapa kuwavaa wenyeji wao Ndanda FC mchezo wa Ligi kuu bara. Licha kwamba Yanga itawakosa nyota wake muhimu kama Ally Mustapha 'Barthez', Vincent Bossou na Haruna Niyonzima 'Fabregas', lakini hata hivyo ina shehena ya wachezaji nyota na inaweza kurejea na ushindi. Ndanda nayo ikiwa imejeruhiwa katika mechi mbili ilizocheza ikifungwa mabao 3-1 na Simba jijini Dar es Salaam, pia ikifungwa mabao 2-1 na Mtibwa Sugar Morogoro, haitakubali kuendelea kupoteza mbele ya Yanga ambao wamekuwa na rekodi mbaya kwenye uwanja huo wakicheza na Ndanda. Hata hivyo Yanga ina kumbukumbu nzuri ikianza ligi kwa kishindo baada ya kuilaza African Lyon mabao 3-0 uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, safu ya ushambuliaji ya Yanga itaongozwa na mfungaji bora msimu uliopita Amissi Tambwe raia wa Burundi akisaidiana na Donald Ngoma raia wa Zimbabwe,

Mwaisabula afichua ya Serengeti Boys

Picha
Na Prince Hoza, Dar es Salaam Kocha wa zamani wa Bandari Mtwara, Ashanti na Yanga SC, Kenny Mwaisabula 'Mzazi' amefichua ya Serengeti Boys ya kutumia wachezaji vijeba mwaka 2004 na kuondoshwa na CAF kwenye fainali za mataifa Afrika zilizofanyika Gambia. Akizungumza katika kipindi cha michezo cha MBS kinachorushwa kuanzia saa tano asubuhi mpaka saa saba mchana na redio Sibuka ya jijini Dar es Salaam, Mwaisabula amesema Serengeti timu ya umri wa miaka 17 lakini ilikusanya wachezaji waliozidi umri huo. Mzazi aliwataja wachezaji kama Athuman Idd 'Chuji' , Mrisho Ngasa, Kiggy Makassy, Amir Maftah, Hassan Bwaza, Patrick Mangunguli, Nizar Khalfan, Nurdin Bakari, Yusuph Mgwao na David Mwantebe tayari walishazidi umri huo kwakuwa walianza kucheza Ligi kuu kabla hawaitwa timu hiyo ya vijana. Mbali na Nurdin kugundulika, bado kulikuwa na wachezaji wengine anaowafahamu kudanganya umri ni wengi akiwemo Chuji na Mangunguli, 'Chuji alikuwa anaichezea Polisi Dodoma halafu akait

Simba yaipigisha kwata Polisi Dodoma

Picha
Na Ikram Khamees, Dodoma Magoli mawili yaliyofungwa na Abdi Banda na Said Ndemla kila kipindi, yametosha kabisa kuwapigisha kwata Polisi Dodoma iliyokubali kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Simba SC katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa. Vijana wa Simba wanaonolewa na Mcameroon, Joseph Omog walicheza kandanda safi na la kuvutia na kufanikiwa kujipatia mabao hayo mawili. Simba imeamua kuelekea Dodoma ikiwa katika harakati zake za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania  Mhe John Magufuli ambaye ameamua kuihamishia serikali yake mjini Dodoma

Simba yaipigisha kwata Polisi Dodoma

Picha
Na Ikram Khamees, Dodoma Simba SC jana jioni imefanikiwa kuwapigisha kwata maafande wa Polisi Dodoma baada ya kuwachapa mabao 2-0 mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini hapa. Simba wakicheza kandanda zuri na la uhakika ilifanikiwa kujipatia bao lake la kwanza katika kipindi cja kwanza lililofungwa na kiungo Abdi Banda. Mabingwa hao wa zamani waliandika bao la pili katika kipindi cja pili lililofingwa na Said Ndemla, Simba imeamua kuelekea Dodoma na kucheza mechi ya kirafiki ikiwa kama kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe John Magufuli aliyehamua kuihamishia serikali yake Dodoma

Smart Sport yaibwaga TFF Mahakamani

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, jana imeipa ushindi kampuni ya kuuza na kusambaza vifaa vya michezo ya Smart Sport ambayo ilifungua kesi ya madai dhidi ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF). Kwa mujibu wa Mahakama hiyo, TFF imetakiwa kuilipa Smart Sport Shilingi Milioni 30 za Kitanzania zikiwa kama gharama zitokanazo na deni la kampuni hiyo dhidi yao. Awali TFF kupitia kwa Afisa Habari wake Alfred Lucas alikanusha vikali TFF kudaiwa na Smart Sport, lakini Mahakama ikaona TFF inadaiwa na kampuni hiyo. Smart Sport inaidai TFF baada ya kugharamia vifaa vya michezo ikiwemo jezi, viatu, soksi, mipira, tracksult na vinginevyo kwenye timu zote za taifa na imekuwa ikipigwa danadana kila inapodai fedha zake. Mtandao huu ulipomuuliza Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Emily Malinzi kuzungumzia sakata hilo alishindwa kutoa maelezo na kudai hana muda kwa sasa kuelezea suala hilo na labda wamtafute siku nyingine. Hata hivyo TFF inaweza kukata rufaa

Kiiza tayari kabisa kumrithi Ngasa Free State

Picha
Na Mwandishi Wetu Wakati mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Khalfan Ngasa akivunja mkataba wake na Free State, mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Kiiza tayari amejiunga na timu hiyo kuchukua nafasi ya Ngasa. Kiiza aliyetupiwa virago vyake na klabu ya Simba ya Tanzania, amesajiliwa kwa mkataba wa mwaka mmoja na Free State majuzi lakini imebainika amekwenda kuchukua nafasi ya Ngasa. Kiiza ambaye aliwahi kuzichezea Yanga na Simba, amejiunga na timu hiyo akiwa na matumaini kibao ya kung' ara kwanj tayari alishafanikiwa kufunga mabao 19 katika timu yake ya mwisho kuichezea ya Simba katika Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara

Kisa mataji, Ngasa aitosa Free State

Picha
Na Mwandishi Wetu Mshambuliajj wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngasa ameamua kuvunja mkataba na klabu yake ya Free State Stars inayoshiriki Ligj kuu ya ABSA nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bethlehem Afrika Kusini zinasema kwamba Ngasa ameamua kuachana na Free State kwa kile kinachodaiwa kukosa furaha ya kubeba mataji. Ngasa amesema Free State haina malengo na imekuwa ikipambana bila mafanikio, "Nataka kucheza timu yenye uwezo wa kunyakua mataji, karibu timu zote nilizowahi kucheza zimetwaa ubingwa", anasema Ngasa. Ngasa ameweka mpango wake wa kutaka kujiunga na timu nyingine ambayo anadai ataitaja hivi karibuni, Ngasa amewahi kuzichezea Toto Africans, Kagera Sugar, Yanga, Azam na Simba, je atarejea Bongo?