Yanga yapata bonge la kipa anadaka kama nyani

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Yanga SC leo imetambulisha nyota wawili wote wanatoka Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Congo (DRC) kipa anayedaka kama nyani Klauz Kinzi Kindoki na straika mwenye mashuti Heritier Makambo wwamesainishwa mkataba wa miaka miwili kila mmoja.

Dirisha la usajili linafungwa usiku wa saa sita usiku Yanga imeamua kuwasainisha nyota hao wawili ikiwa kama sehemu ya kukiimarisha kikosi chake ambacho msimu uliopita kiliteteleka baada ya kushindwa kutetea taji lake lililokwenda kwa mahasimu wao Simba SC.

Mpaka sasa Yanga imesajili wachezaji saba ambao ni Makambo na Kindoki waliotambulishwa leo, wengine ni Mohamed Issa Banka toka Mtibwa Sugar, Mrisho Ngasa wa Ndanda FC, Fesal Salum "Fei Toto", wa JKU na Deus Kaseke toka Singida United pia imemsajili Elisha Muroiwa toka Singida United ambaye aliletwa kama msaada toka kwa Mwigulu Nchemba

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA