Makambo aula Yanga CAF, Ngasa atemwa
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Uongozi wa mabingwa wa zamani wa Tanzania Bars Yanga SC imeweka wazi kumuorodhesha straika Heritier Makambo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo (DRC) katika kikosi chake kinachoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Shirikisho la Moira wa miguu barani Afrika, CAF jana lilipitisha usajili wa wachezaji wawili wa Yanga ambao awali ulishindikana, wachezaji ambao usajili ulipitishwa na kiungo mshambuliaji Deus Kaseke na mshambuliajj Matheo Antony, lakini uongozi wa klabu hiyo kwa kushirikiana na benchi la ufundi imeamua kumuongezea straika Mkongoman Heritier Makambo ambaye alisajiliwa hivi karibuni akitokea FC Lupopo.
Kupitishwa kwa Makambo kunamuondoa Mrisho Ngasa katika idadi hiyo hivyo sasa Makambo atakuwa miongoni mwa wachezaji wa Yanga watakaotumika katika michuano hiyo ya Afrika huku Ngasa akisubiria msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoanza Agosti 22 mwaka huu