Simba wazidi kunoga huko Uturuki

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Baada ya kufanikiwa kufika salama jana huko nchini Uturuki katika mji mkuu wa Istambul na kuelekea mji wa Antaly uliopo kilometa 15 kutoka mji mkuu, wameanza mazoezi yao leo na wako tayari kwa mapambano.

Wekundu hao wanafanya mazoezi makali chini ya kocha mkuu Mbelgiji Patrick Winand Aussems na msaidizi wake Irambona Masoud Djuma huku wachezaji wake wakionekana kufurahia ziara hiyo ya Uturuki.

Simba itaendelea kukaa huko kwa majuma mawili na itarejea nyumbani ifikapo Agosti 5 mwaka huu ambapo pia itashuka dimbani katika hafla ya Simba Day itakayofanyika Agosti 8 ambayo huadhimishwa kila mwaka

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI