Chilunda akwama kupaa Hispania
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Mshambuliaji chipukizi wa Azam FC Shaaban Iddi Chilunda ambaye ameuzwa kwa mkopo kwa klabu ya CD Tenerife ya Ligi daraja la pili nchini Hispania, ameshindwa kuelekea huko akisubiria mambo yakae sawa kuhusu vibali vya kufanyia kazi, hayo aliyasema leo alipoulizwa juu ya safari yake baada ya kuachana na Azam FC ambao ni mabingwa wa Afrika mashariki na kati.
" Kwa sasa klabu yangu mpya inashughulikia kibali cha mimi kuweza kufanya kazi Hispania na taratibu zote zikikamilika ndipo nitakuwa na uwezo wa kuondoka hapa na kwenda kuanza kazi sababu wenzetu wanazingatia sheria sana."
“Sababu huwezi kwenda kule kama huna kibali cha kazi kila kitu kikikamilika ndipo nitaweza kupewa visa na kuondoka hapa nchini kwa ajili ya kuanza kazi yangu rasmi ndani ya Tenerife,”
Maneno ya Shaaban Idd Chilunda Alipoulizwa kuhusiana na safari yake ya Kwenda nchini Hispania kwa ajili ya kuanza kuitumikia klabu yake mpya ya Tenerife ambayo ameingia nayo mkataba wa miaka 2 .