Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2014

HII NDIO PICHA INAYOONYESHA JIJI LA DAR ES SALAAM TANGIA MWAKA 1887

Picha
HUWEZI kuamini kwamba jiji la Dar es Salaam limeanza mbali sana na lilikuwa katika mitizamo tofauti, vijana wa leo wanakwambia hakuna maendeleo yoyote yaliyopatikana ndani ya miaka 50 na kinachoonekana mbele yao ni sawa na kazi bure.

KIPRE TCHETCHE WA AZAM FC NDIYE BORA LIGI KUU BARA

Picha
Mshambuliaji Kipre Tchetche wa mabingwa wapya Azam FC, ameibuka mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu katika tuzo za wanasoka bora zilizotolewa usiku wa kuamkia jana na mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), kampuni ya huduma za mawasiliano ya Vodacom Tanzania. Nyota huyo raia wa Ivory Coast, alitwaa tuzo yake akiwapiku Anthony Matogolo wa Mbeya City na Lugano Mwangama wa Tanzania Prisons aliokuwa akichuana nao katika kipengele hicho. Kwa tuzo hiyo, Kipre alizawadiwa Sh. milioni 5.2 ikiwa ni ongezeko la Sh. 200,000 ikilinganishwa na msimu wa 2013/14 wa ligi hiyo ambayo beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani aliinyakua. Meneja wa Azam FC, Jemadari Said alipokea tuzo ya Tchetche kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

MANCHESTER UNITED SASA NI YATIMA

Picha
Mmiliki wa Manchester United mmarekani Malcom Glazer ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 85 . Familia ya bwenyenye huyo ilinunua United kwa gharama ya Euro milioni 790 mnamo mwezi Mei mwaka wa 2005 licha ya pingamizi kali kutoka a kwa mashabiki wa klabu hiyo.

HAPANA CHEZEA MBEYA CITY WEWE! YATINGA ROBO FAINALI SUDAN

Picha
MBEYA City imetinga Robo Fainali za michuano ya Nile Basin inayoendelea nchini Sudan kufuatia sare ya bila kufungana na Enticelles ya Rwanda usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Khartoum. Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City imalize na pointi nne baada ya mechi tatu, ikiwa katika nafasi ya pili nyuma ya AFC Leopards ya Kenya walioongoza kundi kwa pointi zao tisa. Enticelles imemaliza nafasi ya pili kwa pointi zake mbili na Academie Tchite ya Burudi imemaliza mkiani mwa Kundi B kwa pointi moja iliyovuna kwenye sare na timu ya Rwanda.

MWANAMKE WA MIAKA 22 MBARONI KWA KUUZA MTOTO.

Picha
Mwanamke mwenye umri wa miaka 22 Chinelo Huma amekamatwa na kitengo cha kupambana na biashara haramu ya kuuza binadamu cha jimbo la Enugu kwa kitendo cha kumuuuza mtoto wake mwenye umri wa mwezi mmoja .

MAKALA; KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA KUMBE BOMU.

Picha
Na Prince Hoza KAMATI ya uchaguzi ya klabu ya Simba inayoongozwa na mwanasheria Dk Damas Daniel Ndumbaro imeonyesha kasoro nyingi na kukosa weledi baada ya kumtupa nje aliyekuwa mgombea nafasi ya urais katika klabu ya Simba Michael Richard Wambura. Wambura ameondolewa katika kinyang'anyiro hicho kwa madai si mwanachama halali wa Simba pia aliwahi kusimamishwa uanachama wake tangia mwaka 2010 wakati huo mwenyekiti akiwa Hassan Dalali 'Field Marshal'.

MSHIRIKI WA KTMA 2014 AKUTWA KWA SANGOMA MWANZA

Picha
Na Saida Hoza- Mwanza ALIYEKUWA mshiriki wa Kili Music Award 2014 Batarokota Linda amenaswa na kamera yetu akiwa kwa sangoma yaani mganga wa kienyeji akipatiwa dawa. Mwandishi wetu ambaye amepiga kambi jijini Mwanza ametabaisha kuwa mwanamuziki huyo wa nyimbo za asili amekuwa na kawaida ya kufuata dawa kwa sangoma huyo. Chanzo chetu cha habari kinaamini Batarokota amefuata ndumba ili afanye vizuri na kunyakua tuzo mbalimbali mwakani. Msanii huyo alipozungumza na Mtandao huu kuhusu kukutwa kwake kwa sangoma huyo, amekiri kutumia dawa za kienyeji lakini amekataa kuhusisha na imani za kishirikina. Aidha amefafanua kuwa sangoma huyo ni babu yake na amekuwa akimsaidia mara kwa mara, kuhusu kufuata dawa: Batarokota amesema ni kweli amekuwa akisumbuliwa kwa muda na mrefu na ugonjwa wa kichomi.

PATA PICHA NNE YA ZIARA YA PAPA FRANSIC MASHARIKI YA KATI

Picha

NYUMBA YA MSHIRIKI WA KILL MUSIC AWARD 2014 YAUNGUA MOTO

Picha
Na Saida Hoza- Mwanza Nyumba ya familia ya mzee Beatus Linda iliyopo maeneo ya Igoma-Kusini mkoani Mwanza iliwaka moto na kusababisha uharibifu wa mali zilizokuwemo humo. Moto huo uliosababishwa na gesi jioni ya saa 11 siku ya Jumanne  tarehe 4-4-2014 mtaa wa Dr Sheikh Ramadhan Panzi Igoma Kusini. Mmoja kati ya watu waliopatwa na janga hilo na mtoto wa mzee Beatus Linda ambaye ni mshiriki wa Kilimanjaro Music Award 2014 Batarokota ambaye wimbo wake wa Kwejaga Nyangisha ulishirikishwa.

TP MAZEMBE YAWAZUIA SAMATTA, ULIMWENGU KUCHEZA STARS

Picha
WASHAMBULIAJI wawili wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu huenda wasipatikane kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Zimbabwe Juni 1 mjini Harare hatua za awali Kombe la Mataifa ya Afrika.

RECHO WA BONGO MOVIE HATUNAYE

Picha
Msanii wa bongo movie, Rachel Haule 'Racho' amefariki dunia usiku wa leo katika hospitali ya Muhimbili alipopelekwa kujifungua. Kwa mujibu wa taarifa hiyo inasema kuwa marehemu Recho alifariki baada ya kujifungua mtoto ambaye naye akafariki naye baada ya kukimbizwa I.C.U kutokana na hali yake kuwa mbaya sana.

BRENDAN RODGERS AENDELEA KUULA LIVERPOOL

Picha
Brendan Rodgers ametia sahihi kandarasi mpya ya muda mrefu kuwa mkufunzi wa timu ya Liverpool iliyomaliza yapili msimu uliopita.

CAMEROON YAPATA USHINDI KWA TAABU

Picha
Nahodha wa Cameroon Samwel Eto’o katika mechi ya kujipima nguvu ambayo The indomitable Lions iliishinda Macedonia mabao 2-0 nchini Austria.

DIDA AAMUA KUACHANA NA YANGA, HUENDA AKATIMKIA UARABUNI.

Picha
Kipa chaguo la kwanza kwa Yanga kwa sasa Deogratius Munishi 'Dida' amesema hana uhakika wa kuendelea kubaki Yanga baada ya mkataba wake kumalizika kutokana na kasumba iliyoibuka ya kutokuwa na imani na wachezaji pindi timu inapokuwa  na matokeo mabovu.

BAADA YA KUFUNGWA NA REAL MADRID, ATLETICO YAZUIWA NYOTA WAKE WOTE KUHAMA

Picha
KLABU ya Atletico Madrid itapambana kuhakikisha wachezaji wake bora na inatumai kwa umuhimu wao katika klabu na kwa kocha wao, Diego Simeone itasaidia wakibaki. Kipa wa Chelsea anayecheza kwao kwa mkopo, Thibaut Courtois amezungumzia mustakabali wake baada ya kufungwa Real Madrid 4-1 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini kwa kiasi kikubwa hayuko mikononi mwa Atletico. "Sina mawasiliano ya moja kwa moja na Chelsea,"amesema kipa huyo mwenye umri wa miaka 22, Courtois. "Sina lolote dhidi yao. Ni kwamba nina dhamana hii na Atletico, baada ya yote nimeishi na klabu hii kwa misimu mitatu iliyopita,".

MAKALA: TAKUKURU KUWENI MAKINI UCHAGUZI MKUU SIMBA

Picha
Na Prince Hoza NATOA angalizo kwa taasisi ya kupambana na rushwa nchini Takukuru kuwa macho na uchaguzi wa klabu ya Simba unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu. Tayari uchaguzi huo umeonyesha kuwepo kwa vitendo vya rushwa vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya wagombea, wapo baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia kuwapa wanachama fedha ili wawachague.

TP MAZEMBE YAENDELEZA MAUAJI TENA

Picha
TP Mazembe walishindi mahasidi wao wa jadi AS Vita kutoka Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo katika mechi iliyobashiriwa kuwa ngumu ya kundi A ya kuwania ubingwa wa Afrika miongoni mwa vilabu .

KENYA YAVUNJA REKODI YA RELAY BAHAMAS

Picha
Rekodi tatu za dunia zimevunjwa katika mbio za matimko na kupokezana vijiti. Rekodi ya mbio za mita 1500 ya wanawake ilivunjwa na wakenya Mercy Cherono, Faith Kipyegon, Irene Jelagat na Hellen Obiri walipotumia muda wa dakika 16:33.58 zaidi ya sekunde 32 ndani ya rekodi ya awali.

WAMBURA, KABURU KUENGULIWA UCHAGUZI MKUU SIMBA

Picha
Michael Wambura na Geofrey Nyange ‘Kaburu’ pamoja na wagombea  wa ujumbe wa kamati ya utendaji ya Simba wamewekewa pingamizi la kuwania uongozi. Mwanachama Swaleh Madjapa kadi namba 00574, Mwinyi Dossy kadi namba 564 pamoja na kocha wa zamani wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ndio waliojitokeza jana kuweka pingamizi kwa wagombea hao.

PIGO:YAYA TOURE AUGUA GHAFLA, AKIMBIZWA UARABUNI KUTIBIWA

Picha
KIUNGO Yaya Toure anapatiwa matibabu nchini Qatar kwa maumivu ambayo hayajawekwa wazi kabla ya kuungana na wachezaji wenzake wa Ivory Coast katika iambi yao ya kujiandaa na Kombe la Dunia nchini Marekani, imesema taarifa ya Shirikisho la Soka Ivory Coast jana.

AMINA NGALUMA KUZIKWA MCHANA HUU

Picha
Na Robert Michael Mwanamuziki wa zamani wa kundi la African Revolutional 'Wana Tam Tam' pamoja na Double M Sound Amina Ngaluma 'Japaness' aliyefariki majuma mawili yaliyopita huko nchini Thailand anatarajia kuzikwa mchana huu katika makaburi ya Kitunda Machimbo jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Muumini Mwinjuma 'Kocha wa Dunia'ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa bedni hizo zote zlizopitia marehemu Ngaluma, amedai kuwa mwanamuziki huyo anazikwa mchana katika makaburi ya Kitunda na umati mkubwa wa wakazi wa jiji laDar es Salaam watakitojikeza. Mbali na wakazi wa Dar es Salaam, marehemu Ngaluma aliyetamba na wimbo wa 'Mgumba' atapata watu wqengi watakaokwenda kujitokeza kumzika, marehemu Ngaluma alifariki dunia nchini Thailand majuma mawili yaliyopita na mwili wake uliwasili nchini jana usiku.

KUMEKUCHA ULAYA LEO, ATLETICO MADRID V REAL MADRID

Picha
‘MWALI’ wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka huu anatarajiwa kumpata mwenyewe usiku wa leo katika fainali itakayopigwa Uwanja wa Luz mjini Lisbon, Ureno baina ya Real Madrid na Atletico Madrid za Hispania. Huo ni mchezo wa kuhitimisha msimu wa 59 wa michuano hiyo mikubwa zaidi ya klabu Ulaya na msimu wa 22 tangu michuano hiyo ianze kutumia jina hilo kutoka Klabu Bingwa ya Ulaya. Hii itakuwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo kukutanisha timu kutoka Jiji moja, Madrid.

SUAREZ: WAURUGUAY WAMTISHIA KIFO DUMMETT

Picha
Jeraha la Suarez sasa mashabiki wa Uruguay wamlaumu mlinzi wa Newcastle Paul Dummett. Mlinzi wa Newcastle Paul Dummett ametishiwa maisha yake na mashabiki wa Uruguay wanaomlaumu kwa kusababisha jeraha lililomlazimu Luis Suarez kufanyiwa upasuaji ambao sasa wanahofu huenda ikaathiri uwezo wake katika kombe la dunia .

WITNESS MWAIJAGA AKEMEA ULEVI KWA WASANII WAWAPO JUKWAANI

Picha
Na Robert Michael MSANII wa kizazi kipya aliyepata kung'ara na kundi la Wakilisha lililokuwa likishirikisha nyota watatu Witness Mwaijaga amekasirishwa na kushushwa kwa hadhi ya muziki huo nchini na baadhi ya wanamuziki. Mwanadada huyo mkali katika muziki wa miondoko ya Hiphop anaetamba na nyimbo zake ambazo ni "Zero" amemshirikisha Fid Q, "Safari" pamoja na "Attention", ambaye maskani yake ni Tukuyu mkoani Mbeya, amesema kuna baadhi ya wasanii wa Bongo wamekuwa wakishusha hadhi muziki wa Hiphop.

TAIFA STARS YAINGIA KAMBINI, MAGODORO YAMCHELWESHA NGASA

Picha
Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) kilienda Mbeya jana kikitokea Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Zimbabwe bila ya nyota wake watatu akiwamo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa.

MUZIKI NI ZAIDI YA SOKA- HAMOSNOTA

Picha
Na Mariamu Libibo MSANII chipukizi wa miondoko ya kizazi kipya anayetamba na wimbo wake wa 'Bye bye' Hashim Momba 'Hamosnota' (Pichani) amedai muziki ni zaidi ya mchezo wa soka na kama serikali ingetambua hilo ingewekeza vya kutosha. Akizungumza katika ofisi za Mambo uwanjani blogspot Hamosnota amesema anashangazwa na serikali kung'ang'ania mchezo wa soka ambao umeshindwa kuipa heshima nchi wala kuingiza mapato ya kutosha. Ameongeza kuwa kama serikali ingetumia muziki basi ingenufaika kwani unaingiza fedha nyingi kuliko soka, ametolea mfano shoo ya mwanamuziki Diamond Platinum iliyofanyika mwaka jana Mlimani City ambapo kiingilio chake ilikuwa 50, 000 na tiketi zilikwisha. Pia amedai kwenye shoo za muziki hakuna wiz\i kama ilivyo kwenye soka ambapo wizi wa tiketi umekuwa wimbo wa taifa, 'Serikali ingetumia muziki ingenufaika sana kwani muziki ni sehemu ya burudani kwa kiola mtu hivyo huingioza fedha nyingi', aliendelea.

WADAU WAKUTANA KUPANGA MAZISHI YA AMINA NGALUMA

Picha
WANAMUZIKI na wadau wa muziki wanakutana Alhamisi ya leo Saa 5 asubuhi kujadili namna ya kusaidia na kushiriki mazishi ya mwimbaji Amina Ngaluma (Pichani). Hilo litafanyika ndani ya ukumbi wa Vijana Social Hall (jirani na Mango Garden), Kinondoni jijini Dar es ambapo itaangaliwa namna nzuri ya kushirikiana na familia ya marehemu kuanzia hatua ya kuupokea mwili hadi mazishi. Mwili wa Amina Ngaluma aliyefariki nchini Thailand Alhamisi iliyopita, utawasili jijini Dar es Salaam Ijumaa hii saa 3.30 usiku kwa  ndege ya KLM. Mazishi yatafanyika siku inayofuata (Jumamosi) mchana. Mmoja wa waratibu wa kikao hicho cha Alhamisi kinachoshirikisha pia Shirikisho la Muziki Tanzania, Mwinjuma Muumin, amesema msiba huu umechukua muda mrefu, familia imeingia gharama kubwa katika kipindi chote hiki na hivyo ni wakati muafaka sasa kwa wanamuziki na wadau wa muziki  kukutana na kuangalia namna ya kuipunguzia mzigo familia ya marehemu.

RONALDO NA BALE KUCHEZA FAINALI YA UEFA DHIDI YA ATLETICO

Picha
Mchezaji bora duniani mwaka huu Cristiano Ronaldo na mshambulizi aliyegharimu kitita kikubwa zaidi duniani Gareth Bale watakuwepo katika timu ya Real Madrid itakayochuana na Atletico Madrid katika fainali ya kuwania kombe la mabingwa barani Uropa jumamosi hii.

MAN CITY YAMWANGUKIA YAYA TOURE

Picha
MKURUGENZI wa soka wa Manchester City, Txiki Begiristain atafanya mazungumzo ya amani na Yaya Toure kabla ya kuanza kwa Fainali za Kombe la Dunia ili kumaliza tofauti zilizojitokeza kati ya kiungo huyo na klabu hiyo.

MAKALA: G-BOY ALIA NA MAPRODYUZA, ADAI WANAWAPUUZA WASANII CHIPUKIZI

Picha
Na Robert Michael 0752 711688 ANAITWA Julius George Mgomela ( Pichani) ila maskani kwake Tabata Kisukuru humfahamu kwa jina la G-boy ambalo analitumia kwenye shughuri zake za muziki. Tayari G-boy amerekodi nyimbo mbili ambapo moja inaitwa 'Pesa mke wangu'na nyingine inaitwa Promise, nyimbo zote hizo amemshirikisha PNC na amefanyia katika studio za Iringa Record chini ya prodyuza Tudi Thomas. G-boy ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Kigoma amelalamikia ukata wa fedha ambapo amedai anaomba mdhamini ajitokeze ili aweze kuendeleza kipaji chake. 'Tatizo linalinisumbua ni ukata, sina pesa hivyo inanifanya nishindwe kupanga kazi zangu vizuri', alisema, Aidha G-boy anaelezea ukata wa fedha unamnyima fulsa ya kushirikiana na wasanii wakubwa kama vile Diamond Platinum.

DIEGO COSTA AENDA KWA SANGOMA WAKE

Picha
MSHAMBULIAJI Diego Costa amesafiri kwenda Belgrade kumuona mganga wa kienyeji Marijana Kovacevic maarufu kama 'Dokta Miujiza' kuhakikisha anakuwa fiti tayari kucheza mechi kubwa zaidi maishani mwake. Mserbia huyo anatumia placenta kuwasaidia wachezaji kupona haraka matatizo ya misuli na Jumamosi Costa anataka kuichezea Atletico Madrid dhidi ya Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

PAZIA LA USAJILI KUFUNGULIWA JUNI 15

Picha
Dirisha la usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara 2014/2015 unatarajiwa kuanza Juni 15 hadi Agosti 3 mwaka huu, imeelezwa jana jijini Dar  es Salaam. Akizungumza jana, Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa klabu zinatakiwa kuzingatia muda huo uliopangwa ili kuepusha malalamiko kutoka kwa wachezaji wao. Wambura alisema kuwa klabu zinatakiwa kutangaza kuacha au kusitisha mikataba yao kati ya Juni 15 na 30 mwaka huu wakati kipindi cha kwanza cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi Julai 30 mwaka huu.

Q CHILLA ATOBOA KILICHOMUUA KUAMBIANA

Picha
Na Robert Michael Msanii huyo wa "Bongo Fleva" akizungumza na blog hii amesema kifo cha "Adam Kuambiana" kilimkuta akiwa kwenye kambi ya kurekodi "Filamu". Wakiwa wanajitayarisha "Jumamosi" waanze kushuti filamu ya Adam Kuambiana inayoitwa "Jojo".Q Chillah anasema siku ya Ijumaa jioni Kuambiana" na wasanii wenzake walikuwa "Baa" wakinywa pombe. Hadi usiku wa Saa 8, Lakini Kuambiana alikunywa pombe huku akidai tumbo linamsumbua,Baada ya kumaliza kila mmoja alikwenda kulala.Ilipofika kesho yake "Jumamosi" saa 3.00.

YAYA TOURE ATHIBITISHA KAULI YA WAKALA WAKE, SASA KUHAMA RASMI MAN CITY

Picha
MWANASOKA bora wa Afrika, Yaya Toure ameibuka kumsapoti wakala wake, Dimitri Seluk aliyeishambulia Manchester City kwa kutojali kuhusu birthday ya kiungo huyo. Yaya amesema yote aliyoyasema Seluk ni ukweli mtupu na yeye ataamua mustakabali wake baada ya Fainali za Kombe la Dunia mwezi ujao. Seluk ameelezea shaka ya mchezaji huyo wa Ivory Coast kubaki Etihad kwa kusema kiungo huyo tegemeo haifurahii na klabu hiyo.

PROFESA J AWAPA SOMO WATU WENYE TABIA ZA UMBEA.

Picha
Na Robert Michael Msanii mkongwe wa miondoko ya kizazikipya nchini Joseph Haule ' Profesa J' amewataka baadhi ya "Watanzania" waache kumsema vibaya kutokana na ukimya wake ama anapopata matatizo kwani kuna wakati binadamu anakuwa katika kkwamo wa kimaisha.. Profesa akireport katika blog hii amesema kuwa ameamua kufanya wimbo wake wa "Kipi sijasikia" alio mshirikisha "Diamond Plutnumz" msanii aliepata tuzo 7 za "Kili music award" ili kufikisha ujumbe kwa watu wanao mtakia mabaya pamoja na kuwaelimisha waache tabia hiyo ya umbea. Aidha msanii huyo amesema kuwa kuna siku aliugua "Maralia" hivyo basi kutokana na kuugua alikonda lakini baadhi ya watu walisambaza umbea kuwa alikonda kwa "Ukimwi".

STAMINA ASHINDWA KUELEWANA NA MABEST.

Picha
Na Robert Michael Wasanii hawa wa muziki wa Hiphop wameshindwa kuelewana kutokana na nyota wa music wa hiphop"Stamina" kutohudhuria kwenye shoe aliyoshirikishwa na msanii mwenzake "Mabest". Inasemekana kuwa "Stamina" hakutoa taarifa ya kutoshiriki kwenye shoo hiyo kutokana na matatizo yake ya kifamilia. Hali hii ilipelekea msanii "Mabest" kuchukizwa na kitendo hicho na kujikuta akimfokea na kumlaumu "Stamina" kuwa kitendo alichokifanya sio kizuri. Aidha msanii "Mabest" aliona kuwa "Stamina" alifanya makusudi kutofika kwenye shoo yake. "Stamina" Anaiambia Blog hii kama ifuatavyo "Ndugu mwandishi sikuweza kumpa taarifa "Mabest" kwa sababu nilivurugwa na matatizo yaliyo tokea katika familia yangu hivyo "Mabest" nilimwelezea akutaka kunielewa.

RWANDA YAMTAKA STEPHEN CONSTANTINE

Picha
Constantine anatazamiwa kufanya mazungumzo na shirikisho hilo la Ferwafa Alhamisi. Timu taifa ya soka ya Rwanda inamtaka Raia Muingereza Stephen Constantine kuwa mkufunzi wake katika mkataba wa miaka miwili.

JULIO AMTUNISHIA KIFUA KABURU, AMUAMBIA “TUNAOMBA PENZI KWA DEMU MMOJA, MWENYE BAHATI YAKE ATABEBA TOTOZ”

Picha
KOCHA wa Mwadui FC ya Shinyanga, Jamhuri Kihwelu 'Julio' amekifafananisha kitendo cha kuwania uongozi katika klabu ya Simba na maamuzi ya mwanaume kumtongoza mwanamke. Akichukua fomu kwenye ofisi za makao makuu ya Simba mjini Dar es Salaam jana kuwania Umakamu wa Rais wa Simba katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Juni 29 mwaka huu, Julio amesema kuwania uongozi wa Simba kunafanana sana na kumtongoza mwanamke.

SEVILLA WAPELEKA TAJI LINGINE LA ULAYA HISPANIA

Picha
SEVILLA ya Hispania imetwaa ubingwa wa Europa League baada ya kuifunga Benfica ya Ureno kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120. Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Juventus, mjini Torino, Italia ulikuwa wa kawaida na timu zote zilicheza kwa tahadhari, hali iliyosababisha hata mashambulizi yawe machache. Sifa zimuendee kipa Mreno wa Sevilla Antonio Alberto Bastos Pimparel aliyewazuilia ndugu zake leo na kucheza penalti moja ya Rodrigo, wakati ya Cardozo ilikwenda nje.

JK AWAREJESHA STARS SAMATTA NA ULIMWENGU

Picha
BAHATI ya aina yake. Washambuliaji wawili wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watawasili Jumamosi mchana kwa ajili ya kuichezea Taifa Stars dhidi ya Zimbabwe kuwania tiketi ya Fainali za Mataifa ya Afrika Morocco mwaka 2015.

MAKALA: ETI HII NDIO TIMU YA MWISHO DUNIANI KWA UBORA WA KANDANDA!

Picha
Nicky Salapu ,kipa aliyeshiriki mechi waliofungwa 31-0 na Australia Mwaka wa 2001 timu ya Australia iliandikisha rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika kandanda ya kimataifa . Australia ilifunga Samoa mabao 31 kwa nunge . Mshambulizi wa Australia Archie Thompson,vilevile aliiingia katika daftari za kumbukumbu kama mfungaji mabao mengi zaidi katika mechi ya kimataifa alipofunga mabao 13.

KILIMANJARO TOUR YAZINDULIWA

Picha
Meneja wa bia ya Kilimnajro, George Kavishe amesema ziara ya tour Kilimajaro itahusisha mikoa ya Kilimanjaro, Mwanza, Kigoma, Kahama, Iringa, Mbeya, Dodoma, Tanga, Mtwara na Dar es Salaam.

RIO FERDINAND ALIVYOTEMWA 'KIROHO MBAYA' MAN UNITED

Picha
BEKI Rio Ferdinand amemaliza maisha take ya soka Manchester United baada ya kuambiwa hatapewa Mkataba mpya.   Mkuu wa Old Trafford, Ed Woodward alimpa habari hizo za kusikitisha Ferdinand mwenye umri wa miaka 35 katika chumba cha kubadilishia nguo Jumapili wakati wa mchezo wa mwisho na Southampton.    Wengi wamesikitishwa na kitendo cha Woodward kuamua kumuacha 'kiroho mbaya' Ferdinand baada ya miaka 12 ya kuitumikia klabu hiyo kwa moyo wake wote.

CD YA JAY-Z AKICHAPWA NA WIFI YAZUA BALAA

Picha
Mitandao ya kijamii imewaka moto kufuatia kanda ya video iliyozuka ikionyesha dadake mwanamuziki wa kimataifa Beyonce Knowles , Solange Knowles akimchapa makonde mwanamuziki Jay-Z ambaye pia ni shemeji yake katika lifti. Hoteli ambako kisa hicho kinadaiwa kutokea mjini New York, 'The Standard Hotel' ilisema kuwa inachunguza ambavyo kanda ya kisa kilichotokea ndani ya Lifti iliweza kusambazwa baada ya kanda hiyo ya video kuzuka katika mtandao mmoja wa udaku TMZ.

DIAMOND PLATINUM, OMMY DIMPOZ WATIMKIA UINGEREZA

Picha
Wanamuziki wa miondoko ya kizazi kipya Ommy na mwenzake Diamond Platinum majuzi waliondoka jijini Amsterdam Uholanzi kuelekea London Uingereza. Diamond amekwenda huko kutengeneza video ya wimbo wake mpya ambayo itafanywa na Director aliewahi kufanya kazi na wasanii kama Davido, Wizkid na FUSE ODG.

RUKSA KLABU LIGI KUU KUSAJILI WATANO WA KIGENI

Picha
Na Boniface Wambura, Dar es Salaam MKUTANO wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Wenyeviti wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kupata maoni yao juu ya changamoto zilizojitokeza katika ligi hiyo uliofanyika juzi umeamua idadi ya wachezaji wa kigeni katika Ligi Kuu iendelee kubaki watano. Klabu za VPL zilizohudhuria mkutano huo ni Azam, Coastal Union, JKT Ruvu, Mbeya City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Polisi Morogoro, Ndanda FC, Ruvu Shooting, Stand United na Tanzania Prisons.

REAL MADRID YAJIONDOA VITA YA UBINGWA LA LIGA

Picha
MAKOSA mawili ya kizembe ya Sergio Ramos na Xabi Alonso yamevunja matumaini ya Real Madrid kutwaa mataji matatu msimu huu baada ya kufungwa 2-0 na Celta Vigo usiku huu. Ili kuweka hai matumaini ya ubingwa wa Hispania, maarufu kama La Liga, Madrid walihitaji Barcelona na Atletico Madrid zipunguzwe kasi, lakini wao wameshindwa kutumia vyema furs yao.

MASIKINI! YANGA KUVUNJA MKATABA NA OKWI

Picha
Katika kile kinachoonekana Yanga imepanga kuachana na mshambuliaji wake Emmanuel Okwi, uongozi wa klabu hiyo umempa masharti magumu nyota huyo wa Uganda ili aendelee kukitumikia kikosi chao. Akizungumza na waandishi kwenye ofisi za makao makuu ya Yanga jijini Dar es Salaam jana, makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga alisema wameamua kufanya mazungumzo na Okwi ili kumaliza tofauti zilizojitokeza kati ya uongozi wao na mkali huyo wa kufumania nyavu. Uongozi wa Yanga jana ulikuwa umekutana kwa mazungumzo na wenyeviti na makatibu wakuu wa matawi ya klabu hiyo klabu hapo. "Tuliingia mkataba na Okwi wa miaka miwili na nusu kwa sharti kwamba kibali chake cha kucheza mpira nchini atalipa mwenyewe.

PICHA: MAN CITY WAKIFURAHIA UBINGWA WAO JANA

Picha
  Mabingwa wa England: Manchester City wamebeba ndoo ya pili katika misimu mitatu baada ya kuifunga West Ham mabao 2-0