Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2015

YANGA YAMALIZANA NA STRAIKA LA PLATINUM YA ZIMBABWE

Picha
Katika kuhakikisha inafanya vizuri katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara pamoja na mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, uongozi wa Yanga umesema umemalizana na mshambuliaji wa Platinum FC ya Zimbabwe, Donald Ngoma, baada ya kukubaliana kusaini mkataba wa miaka miwili. Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka ndani ya uongozi wa Yanga tayari wamekamilisha mazungumzo na mchezaji huyo na anatarajiwa kutua nchini mapema mwezi ujao kumaliza taratibu zilizobaki na kisha kuungana na kikosi cha mabingwa hao wa Bara ambacho kitaanza mazoezi Juni 8, mwaka huu. Chanzo hicho kiliendelea kueleza kuwa wanaamini uwezo wa mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa ya Zimbabwe utasaidia kuimarisha safu ya ushambuliaji baada ya Mrisho Ngasa kuondoka. "Hapa ninavyozungumza na wewe huyo mchezaji ni mali ya Yanga tayari, tumeshamalizana naye, tumempa mkataba wa miaka miwili," alisema kiongozi huyo wa juu wa Yanga.

COUTNHO AJIPELEKA SIMBA

Picha
Kiungo wa Yanga raia wa Brazil Andrey Coutinho huenda akavaa uzi mwekundu na nyeupe msimu ujao kufuatia taarifa zake za kutaka kutemwa ndani ya Yanga hivyo na yeye ameanza maandalizi ya kujiunga na Simba msimu ujao. Coutinho ambaye anasifika kwa mipira wa faulo na kona, yuko mbioni kujiunga na Simba kwa dau la kawaida ili kuwaumiza Yanga ambao wametangaza kumtema, rafiki wa karibu wa mchezaji huyo amedai mipango ya swahiba wake kujiunga na Simba ni mikubwa na muda wowote anaweza kumalizana nao. Pia watu wa Simba wameonyesha kumuhitaji kiungo huyo kutokana na umahiri wake aliounyesha katika ligi hiyo, Coutinho anakumbukwa kwa magoli yake mazuri ya faulo likiwemo lile aliloifunga Azam FC wakati timu yake ya Yanga ikilala 2-1.

MR CHEKA AJA KIVINGINE

Picha
Anselim Malembo ndio jina lake halisi lakini mashabiki wake wanamfahamu kwa jina la Mr Cheka hasa kutokana na wimbo wake uliopata kutamba katika miaka ya mwanzoni 2000 uitwao 'Mr Cheka' aliomshirikisha Mheshimiwa Temba, hatimaye msanii huyo ametangaza kurejea tena kwenye gemu. Safari hii Mr Cheka ameamua kuwashirikisha wakongwe waliopata kutamba kitambo Juma Nature 'Kibra' na Mchizi Mox, akizungumza na Mambo uwanjani, Mr Cheka amesema tayari ameshatengeneza audio na wakongwe hao iitwayo 'Nacheka' ambapo amedai ni maombi ya mashabiki wake waliomtaka arudi katika muziki.

Nooij: Stars fiti kuivaa Swaziland leo.

Picha
Timu ya Soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), leo inatarajiwa kushuka katika Uwanja wa Olympia Park, Rustenburg Afrika Kusini kuvaana na Swaziland katika michuano ya Baraza la Vyama vya Soka Kusini mwa Afrika (Cosafa). Tanzania itashuka uwanjani katika mechi hiyo ya Kundi B, itakayopigwa majira ya saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki ikiwa kama nchi alikwa kwenye michuano hiyo. Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Stars, Mart Nooij, amesema kuwa wachezaji wake wako tayari kwa mchezo huo baada ya kufanya mazoezi kwa siku zote walizokuwa huko licha ya hali ya hewa ya kuwa ya baridi kali.

Barca watwaa ufalme wa Uhispania

Picha
Barcelona ndio wafalme wa Uhispania baada ya kuinua taji lao la tano katika miaka saba la La Liga Jumapili walipowarudishia watetezi Atletico Madrid mkono kwa kuwachapa goli moja kwa yai ugani Vincente Calderon. Wana Blaugrana walipoteza kombe hilo musimu jana baada ya kupokea kichapo cha 1-0 uwanjani mwao Nou Camp katika mechi ya kufunga kampeni lakini walipata kisasi na kutamba kukamilisha taji la 23 katika historia yao ya kifahari. Bila shaka, nyota wao shupavu, Leo Messi wa Argentina ndiye aliyeitikia mwito na kuzamisha goli maridadi kama ilivyo kawaida yake kuamua kivumbi hicho kilichowaniwa kwa makali katika dakika ya 65 kipindi cha pili.