PAZIA LIGI KUU BARA NI SIMBA NA PRISONS, NGAO YA JAMII SIMBA NA MTIBWA SUGAR

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Mabingwa wa Tanzania Bara Simba Sc wanatarajia kukutana na timu ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ngao ya Jamii mechi itakayofanyika jijini Mwanza Agosti 18 mwaka huu.

Baada ya hapo itashuka uwanjani kuumana na Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Agosti 22 huku pia  ikishuka tena dimbani Septemba 30 mwaka huu kuumana na mtani wake wa jadi Yanga Sc.

Ligi hiyo itaanza rasmi Agosti 22 kwa timu zote 20 kushuka dimbani, ratiba ya ligi hiyo imetolewa leo na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, TFF kupitia Bodi ya Ligi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA