NDANDA FC YANASA WAWILI KWA MPIGO

Na Mwandishi Wetu. Mtwara

Baada ya kuondokewa karibu na nyota wake wote wa kikosi cha kwanza uongozi wa klabu ya Ndanda FC ya mjini Mtwara imefanya usajili wa kushitua baada ya kufanikiwa kuwanasa waliowahi kuwa wachezaji wao wa zamani Atupele Green na Kiggy Makassi.

Uongozi WA Ndanda umethibitisha Jana kuwa imempa kandarasi ya mwaka mmoja mshambuliaji Atupele Green wa Kagera Sugar na sasa atakuwa miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo msimu ujao, pia imemnasa Kiggy Makassi aliyekuwa Singida United naye akisaini kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Kurejea kwa nyota hao kunafufua matumaini ya timu hiyo ambayo iliondokewa na washambuliaji wake tegemeo kama Omari Mponda aliyejiunga na Kagera Sugar Tibar John aliyeenda Singida United, Nassoro Kapama aliyejiunga na JKT Tanzania na Mrisho Ngasa Yanga SC

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA