Singida United wajifua vikali Mwanza, yasalenda kwa Fei Toto
Na Paskal Beatus. Mwanza
Wakati klabu bingwa ya soka nchini Simba SC ikiweka kambi nchini Uturuki, timu ya Singida United ya mkoani Singida yenyewe imeamua kwenda kujichimbia jijini Mwanza kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bars inayotarajia kuanza Agosti 22 mwaka huu.
Kikosi hicho kinachonolewa na Hemed Morocco kinafanya mazoezi kabambe asubuhi, mchana na jioni kuhakikisha wachezaji wanakuwa fiti I'll angalau kufanya vema kwenye ligi hiyo, msimu uliopita Singida United ilikomea nafasi ya tano lakini msimu huu hawataki masihara hats kidogo.
Lakini kikosi hicho kikiwa na nyota wake wote iliowasajili katika kipindi hiki cha usajili, imeachana na kiungo wake mpya Fesal Salum "Fei Toto" na kuridhia akaitumikie Yanga SC, Fei Toto alisajili katika vilabu hivyo viwili hivyo ikaona vema nyota huyo acheze na akaitumikie Yanga msimu ujao, ridhaa hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Singida United Dr Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mbunge wa Iramba