MKWASA ABWAGA MANYANGA YANGA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Katibu mkuu wa klabu ya Yanga Charles Boniface Mkwasa ametangaza kujiuzuru nafasi take hiyo lakini sababu kubwa akizitaja na kiafya ambapo amedai amejulishwa na jopo la madaktari wake kumtaka apumzike.
Akizungumza Leo Mkwasa amesema amekuwa akisumbuliwa Mara kadhaa lakini anaendelea kufanya kazi ambazo zimekuwa zikimchosha, katibu mkuu huyo ambaye kitaalamu no kocha mwenye leseni A anajiweka kando huku kukiwa na lawama kubwa dhidi take.
Katibu huyo anadaiwa kuihujumu Yanga katika suala la usajili ambapo mpaka sasa imeshindwa kuwasilisha majina ya wachezaji watatu waliosajiliwa kwa ajili ya michuano ya CAF, wachezaji ambao walisajiliwa ni Mrisho Ngasa, Deus Kaseke na Mkongoman, Heritier Makambo.
Wanayanga bado hawana matumaini na Mkwasa na huenda anatumia nafasi hiyo kujiweka kando ili aweze kutuliza akili zake, Mkwasa pia amewahi kuichezea klabu hiyo katika miaka ya 80, pia amewahi kuinoa Mara kadhaa kabla hajawa kocha WA Taiga Stars