Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2017

Simba nao waikacha Mamelodi

Picha
Na Ikram Khamees, Dar es Sakaam Simba SC nao wametangaza kuikacha Mamelodi Sundows ya Afrika Kusini ambayo ilikuwa wacheze nayo kesho Jumatano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa kirafiki. Mamelodi wamewasili nchini ambapo ziara yao imeratibiwa na Rahim Zamunda Kangezi ambaye ni mmiliki wa timu ya Ligi Kuu Bara African Lyon na ilikuwa icheze mechi mbili na Yanga na Simba. Mamelodi imeletwa kwa kampeni maalum ya kupinga ujangili wa tembo hivyo sasa italazimika kucheza mechi moja na Azam FC katika uwanja wa Azam Complex Chamazi. Meneja wa Simba Mussa Hassan Mgosi amesema wameamua kuikacha Mamelodi kutokana na kukabiliwa na ushindani mkubwa kwenye mechi za Ligi na hivyo wanaogopa majeruhi kwani mchezo wao na Mamelodi ungekuwa mgumu kwakuwa Mamelodi ni mabingwa wa Afrika. Mgosi ameongeza kuwa kocha wao Mcameroon Joseph Omog amwasilisha mapendekezo yake na kuona ni bora Simba ikaachana na mchezo huo wa kirafiki ambao ungefanyika kesho, Simba itasafiri Alhamisi kuelekea

Adebayor apata timu Uturuki

Picha
Mshambuliaji wa kimataifa raia wa Togo Emmanuel Adebayor amejiunga na timu ya Ligi Kuu nchini Uturuki ya Istanbul Basaksehir ambayo kwa sasa inakamata nafasi ya pili. Adebayor amesaini mkataba wa miezi 18 huku kiasi cha pesa alichokabidhiwa ni siri kati yao, Nyota huyo sliyekuwa na timu yake ya taifa ya Togo kwenye fainali za mataifa Afrika nchini Gabon na kuondoshwa mapema ikiwa ya mwisho kwenye kundi C sasa ataanza maisha mapya Uturuki. Bosi wa timu hiyo Mustafa Erogut amesema walikuwa wakimtaka Adebayor kwa kipindi kirefu hivyo kumpata sasa imekuwa furaha kwao na wanaamini Adebayor atawafaa. Adebayor aliwahi kuzichezea Klabu za Arsenal, Manchester City, Tottenham Hotspur za England na Real Madrid ya Hispania

Mkwasa awa katibu mkuu Yanga

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ameteuliwa kuwa katibu mkuu wa Klabu ya Yanga leo na ataanza rasmi majukumu yake kesho. Makamu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amesema, Mkwasa anakuwa katibu mkuu akichukua mikoba ya kaimu katibu mkuu Baraka Deusdetit ambaye amerejeshwa kuwa Mkurugenzi wa fedha. Mkwasa aliyewahi pia kuichezea Yanga na baadaye kuifundisha, amekubali kuchukua cheo hicho na ameahidi kuifanyia makubwa Yanga, wengi wameshangazwa na uteuzi huo kwani wamezoea kumuona Mkwasa akiwa kama kocha. Lakini Sanga amesema Mkwasa anao uwezo wa kuiongoza Yanga kama katibu kwani anayo elimu ya kutosha, Mkwasa anaye amedai hatoingilia kazi za benchi la ufundi na atafanya kile kilichompeleka, Mkwasa alikuwa kocha wa Taifa Stars akirithi mikoba ya Mholanzi Mart Nooij

MAKALA: SIMBA ITAJUTIA MAAMUZI YAKE

Picha
Na Prince Hoza Simba SC inaelekea kubaya, nina maana viongozi wake wanakurupuka kwa kutoa maamuzi yasiyo na tija kwa mashabiki wake, Simba kwa sasa inakamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara. Timu hiyo ilikuwa ikiongoza ligi hiyo kwa kipindi kirefu lakini jana iliondolewa rasmi kileleni hasa baada ya jana Yanga SC kushinda mabao 2-0 dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu Bara. Yanga waaongoza kwakuwa na pointi 46 wakati Simba iliyofungwa bao 1-0 na Azam juzi Jumamosi katika uwanja huo huo wa Taifa ina pointi 45, tatizo linaloonekana kuiathili Simba ni kukosekana kwa muunganiko wa pamoja wa wachezaji wake. Benchi la ufundi linaloongozwa na Mcameroon Joseph Omog libaonekana kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo, lakini mimi wala simlaumu hata kidogo Omog kwani karibu wachezaji wote walioko Simba hakuhusika katika usajili wao. Wachezaji wa Simba walisajiliwa kwa matakwa ya viongozi na wanachama wao na ushabiki ulihu

Wasweden wa Ulimwengu wamnasa Ndemla

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam Klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki Ligi Kuu ya Sweden imethibitisha kufanya mazungumzo na Klabu ya Simba ya Tanzania ikitaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Simba Said Khamis Ndemla. AFC Eskilstuna ndiyo iliyomsajili Mtanzania mwingine Thomas Emmanuel Ulimwengu kwa mkataba wa miaka mitatu imevutiwa na Ndemla ambaye kwa sasa si chaguo la kwanza kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Mcameroon Joseph Marius Omog. Mmoja wa mabosi wa timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu msimu huu Hans Joachim Watkze amesema wanataka kumsajili Ndemla ambaye wamevutiwa naye na tayari wameshafanya mazungumzo na uongozi wa Simba ili waweze kumnasa. Hata hivyo Simba hawajaonyesha nia ya kumwachia licha kwamba wamekuwa wakimtumia Ndemla kama mchezaji wa akiba

SCHWEINSTEIGER KUBAKIA MAN UNITED

Picha
Bastian Schweinsteiger hataihama Klabu ya Manchestet United na atajumuhishwa kwenye kikosi cha klabu hiyo kinachocheza Ligi ndogo ya Ulaya, Europa League, kwa mujibu wa meneja wa timu hiyo Jose Mourinho. Kiungo huyo wa kati wa miaka 32 alifunga wakati wa ushindi wa United wa 4-0 kombe la FA dhidi ya Wigan Jumapili. Hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuanza mechi katika klabu hiyo tangu Januari 2016. Schweinsteiger aliachwa nje ya kikosi cha Europa League msimu huu na Mourinho akalazimishwa kushiriki mazoezi na kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 mwanzoni mwa msimu. Mourinho amesema mchezaji pekee ambaye huenda akaondoka mwezi huu ni Ashley Young. Ataenda kucheza Europa League kwa sababu tumeachwa na nafasi za kujaza kutokana na kuondoka kwa (Memphis Depay) na (Morgan Scheiderlin). Scheineiderlin aliuzwa Everton mnamo 12 Januari, naye Depay akajiunga na Lyon siku nane baadaye. United watakutana na Saint Etienne hatua ya 32 bora Old Trafford tarehe 16 Februali, na mechi ya

David Burhan afariki dunia

Picha
Na Prince Hoza, Dar es Salaam Kipa bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2013/14, David Abdallah Burhan amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Bugando, Mwanza. Kipa huyo wa Kagera Sugar ya Bukoba alifikishwa hospitalini hapo jana kutoka Bukoba na kwa bahati mbaya asubuhi ya leo ameaga dunia. Nahodha wa Kagera Sugar George Kavila ameiambia Mambo Uwanjani kwamba Burhan mtoto huyo wa mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Pan Africans, Abdallah Burhan alikuwa anasumbuliwa na tumbo la kuhara. Kavila amesema matatizo hayo yalianza wakati wamekwenda Singida kucheza na wenyeji wao Singida United mechi ya Kombe la Shirikisho la soka Tanzania (TFF) maarufu kama kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) katikati ya wiki. Uongozi wa Kagera Sugar ulijitahidi kuhakikisha Burhan anapona haraka kwani ulimkodia ndege na kumsafirisha Bukoba ambako nako walimpeleka Bugando na akafikwa na mauti, mwilj wa marehemu utasafirishwa hadi Iringa kwa mazishi, marehemu aliacha mke na wa

MISRI, GHANA ZAPETA AFCON

Picha
Goli lililofungwa na Mahmoud Kahraba dhidi ya timu ya taifa ya Morocco limeivusha timu ya taifa ya Misri katika Nusu fainali ya mashindano ya Afcon 2017. Mtanange huo uliopigwa kwenye uwanja wa Stade de Port Gentil usiku hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa hazijafungana. Bao lililoipatia ushindi Misri limefungwa dakika ya 88 ya kipindi cha pili ikiwa ni dakika 2 kabla kipyenga cha dakika 90 kupulizwa. Kwa matokeo hayo, Misri sasa itakutana na Burkina Faso katika hatua ya nusu fainali. Wakati Misri wakitinga hatua hiyo, Ghana nao walikuwa wa kwanza kufuzu nusu fainali jioni baada ya kuiadhibu DR Congo kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali na wa kusisimua. Andre Ayew na mdogo wake Jordan Ayew ambao ni watoto wa Abedi Pele gwiji la zamani la soka barani Afrika walifunga bao moja kila mmoja na kuisaidia Ghana kushinda mchezo huo mechi ya kwanza ya robo fainali ya michuano ya Afcon nchini Gabon. Ghana sasa itakutana uso kwa uso na ndugu zao wa Cameroon mchezo ambao utaam

TIP TOP CONNECTION KWISHINEI

Picha
Na Saida Salum, Dar es Salaam Kundi lililojipatia umaarufu mkubwa katika muziki wa kizazi kipya lililokuwa na maskani yake Manzese Tip Top jijini Dar es Salaam limesambaratika rasmi na kila msanii ameamua kufanya muziki huru. Akizungumza na Mambo Uwanjani, Aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo Hamad Ally "Madee" amesema mwisho wa Tip Top Connection umefika na sasa ni wakati wa kila msanii kufanya muziki kivyake 'Solo Artist, alisema Madee. Msanii huyo aliyetamba na nyimbo mbalimbali zilizopata kutambulika ndani na nje ya nchi, ameendelea kusema muziki wa kundi haulipi na ni bora msanii kujitegemea, Lakini inasemekana kusambaratika kwa kundi hilo kumetokana meneja wao Babu Tale kunogewa na Diamond Platinumz na kuamua kuachana na kundi hilo ambalo halimlipi

Chirwa aisogeza Yanga kileleni

Picha
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa raia wa Zambia Obrey Chirwa leo jioni ameisogeza kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza baada ya kuiongoza Yanga na kuifunga Mwadui FC mabao 2-0 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Hadi mapumziko timu zote zilienda vyumbani zikiwa hazijafungana, Yanga walitengeneza mashambulizi mengi langoni mwa Mwadui lakini umahiri wa kipa wao Shaaban Kado na mabeki wake ulisaidia kupunguza idadi ya mabao. Kipindi cha pili nacho kilionekana kigumu kwa timu zote, Lakini Obrey Chirwa aliyeingia kuchukua nafasi ya Mnyarwanda Haruna Niyonzima alipachika mabao yote mawili yalioipa Yanga ushindi huo wa mabao mawili yaliyoiweka kileleni. Yanga sasa ndio vinara wa Ligi hiyo wakiipoka Simba ambayo jana ililala dhidi ya Azam ikifungwa 1-0, Yanga wana pointi 46 sasa ikiwa imeiacha Simba kwa tofauti ya pointi moja zote zikishuka dimbani mara 20

Shekhan Rashid apiga bao lingine Sweden

Picha
Wakati mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu akienda nchini Sweden kucheza soka la kulipwa katika Klabu moja ya Ligi Kuu, kiungo wa zamani wa Simba Shekhan Rashid yeye ameongeza mtoto wa tatu. Shekhan yupo Sweden baada ya kuachana na soka la ushindani akaamua kuchukua uraia na kujikita kwenye maisha ya familia na hivi majuzi tu mkewe amejifungua mtoto (Pichani) akiwa na afya njema. Hongera Shekhan Rashid

Burkina Faso yatangulia nusu fainali Afcon, Cameroon nao kimeeleweka

Picha
Timu ya taifa ya Burkina Faso imefanikiwa kuingia nusu fainali ya mataifa ya Afrika baada ya kuendeleza ubabe kwa Tunisia  ikiwalaza mabao 2-0. Kwa maana hiyo Burkina Faso unasubiri mshindi kati ya Misri na Morocco ambazo zinaumana Jumapili, Simba wasiofungika Cameroon nao walifanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuilaza Senegar kwa mikwaju ya penalti 5-4. Miamba hiyo ya Afrika yenye rekodi ya kutinga robo fainali ya kombe la Dunia zilimaliza dakika 90 zikiwa 0-0 na katika mikwaju ya penalti Cameroon iliibuka mshindi na hasa kipa wake Joseph Ondoa akistahili pongezi baada ya kuokoa penalti ya Senegar.

WENGER AFUNGIWA MECHI NNE

Picha
Mkufunzi wa Arsenal Arsenel Wenger amepigwa marufuku ya mechi nne na faini ya pauni 25,000 baada ya kukiri mashitaka ya FA kwa tabia yake mbaya katika mechi dhidi ya Burnley. Wenger mwenye umri wa miaka 67 alishitakiwa kwa kumtusi na kumsukuma msaidizi wa refa Anthony Taylor baada ya kutakiwa kutoka uwanjani. Marufuku yake inaanza mara moja kwa hivyo atakosa mechi ya FA dhidi ya Southmpton. Iwapo mechi hiyo italazimika kurudiwa, Wenger atarudi uwanjani wakati wa mechi ya Ligi ya Uingereza dhidi ya Hull City mnamo tarehe 11 mwezi Februali. Hata hivyo iwapo mechi hiyo itakamilika siku ya Jumamosi na mshindi kubainika mechi dhidi ya Hull City itakuwa mechi yake ya nne na ya mwisho kuhudumia marufuku hiyo kufuatia mechi dhidi ya Watford na Chelsea

Serena Williams amgalagaza dadake

Picha
Serena Williams amedhihirisha kuwa yeye ndio mbabe wa Tennis duniani kwa sasa baada ya kumshinda dadake Venus Williams na kutwaa taji lake la saba la Australia Open na kuweka rekodi ya Opera kwa kushinda mataji 23 ya Grand Slam. Serena mwenye umri wa miaka 35 alishinda katika seti za 6-4, 6-4 ili kumpiku Steffi Graf katika orodha ya washindi wakuu tangu Grand Slam kuwakubali wachezaji wa kulipwa 1968. Raia huyo wa Marekabi sasa ataorodheshwa wa kwanza duniani kwa kumpiku aliyekuwa mchezaji nambari moja upande wa wanawake Angelique Kebber kutoka Ujerumani. Raia wa Australia Margeret Court ndiye mchezaji pekee ambaye yuko mbele ya Serena baada ya kushinda mataji 24 ya Grand Slam

Bocco aiangamiza Simba na kuisafishia njia Yanga

Picha
Na Ikram Khamees, Dar es Salaam Mshambuliaji John Raphael Bocco ameipa ushindi Azam wa bao 1-0 ikiilaza Simba SC na kusitisha kabisa ndoto za Wanamsimbazi kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi. Simba leo imecheza kandanda safi na kuonekana kuwamudu kabisa Azam ambao walisubiri hadi kipindi cha pili kuandikisha bao la ushindi ambalo sasa linawafanya Simba kusalia kileleni kwa masaa tu kwani kesho Yanga akishinda atakwea kileleni. Hadi mapumziko timu zote mbili zilienda vyumbani vikiwa havijafungana, beki Mzimbabwe Method Mwanjali ambaye amezoa tuzo mbili za uchezaji bora wa mwezi Desemba akianzia katika klabu yake ya Simba na ile ya wadhamini wa Ligi Kuu, Vodacom leo amebugi stepu kwa kumpa nafasi Bocco kuiangamiza Simba kinyama

Ni mechi ya kisasi Simba Vs Azam

Picha
Na Ikram Khamees, Dar es Salaam Leo ndio leo asiye na mwana abebe jiwe, vinara wa Ligi Kuu Bara Simba SC jioni ya leo wanashuka uwanja wa Taifa Dar es Salaam kukwaruzana na Azam FC mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotazamiwa kuwa mkali. Mchezo huo utakuwa mkali kutokana na miamba hiyo kutoka kuumana hivi karibuni katika fainali ya kombe la Mapinduzi iliyofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar na Azam kushinda 1-0. Simba wanaingia katika mchezo huo wa marudiano wa Ligi Kuu lakini wakitaka kulipiza kisasi baada ya kulala kwenye fainali, kwa upande wa Azam nao wanataka kushinda mchezo huo ili kulipiza kisasi kwani katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara walilala 1-0. Azam itawategemea zaidi nyota wake John Bocco 'Adebayor', Salum Abubakar, Himid Mao Mkami, Yahaya Mohamed na Stephano Kingue Mpongou, Simba nao watamtegemea zaidi Shiza Kichuya, Ibrahim Ajibu, Mohamed Ibrahim, Mzamiru Yassin na Laudit Mavugo. Endapo Simba itashinda mchezo huo itaendelea kukalia usukani kwa kufikisha pointi 4

Uwanja wa Taifa sasa ruksa Ligi Kuu

Picha
Na Saida Salum, Dar es Salaam Serikali imeuruhusu uwanja wa Taifa uliopo Temeke jijini Dar es Salaam kutumika kwa shughuri za michezo ikiwemo soka. Taarifa ya ruhusa ya uwanja huo imetolewa na Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na wasanii na Mhe Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli ndiye aliyetoa msamahs kwa uwanja huo ambao ulifungiwa. Kwa maana hiyo mechi ya kesho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba na Azam itachezwa kwenye uwanja huo, ikumbukwe mashabiki wa Simba ndio waliosababisha uwanja huo kufungwa baada ya kufanya vurugu kwa kung: oa viti walipocheza na mahasimu wao Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu

Nyosso apigwa marufuku mchangani

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam Nahodha wa zamani wa Mbeya City, Juma Said Nyosso amezuiwa kucheza katika michuano ya Asenga Diwani Cup inayofanyika Uwanja wa Shule ya msingi Tabata. Nyosso ambaye pia amewahi kuzichezea Ashanti, Simba na Coastal Union amejikuta akizuiwa kushiriki michuano hiyo ya mchangani ni kutokana na kamati inayoandaa michuano hiyo kuheshimu maamuzi ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) ambalo limemfungia mchezaji huyo. TFF ilimfungia Nyosso baada ya kudaiwa kumshika makalioni nahodha wa Azam John Rafael Bocco, beki huyo aliyeibukia kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys chini ya umri wa miaka 17 alifungiwa kwa muda wa miaka miwili adhabu ambayo itamalizika msimu ujao. Mchezaji huyo aliichezea timu ya Matumbi FC ya Tabata ambapo aliiwezesha kutwaa Ng' ombe mnyama katika michuano iliyopita, lakini hii ya Diwani Cup Nyosso amezuiwa kwa madai ana adhabu hivyo hapaswi kucheza

Simba yapeta rufaa ya Lufunga

Picha
Na Prince Hoza, Dar es Salaam Klabu ya Simba imepeta rufaa yake iliyokatiwa na Polisi Dar baada ya kumjumuhisha mchezaji wake Novat Lufunga katika mchezo wa michuano ya kombe la Azam Sports Federatipn Cup ambapo Simba ilishinda mabao 2-0. Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na Simba kudanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ulipelekea rufaa kwa timu ya Polisi Dar ikitaka ipewe ushindi kufuatia Simba kumtumia mchezaji mwenye kadi nyekundu aliyopewa mwaka jana kwenye michuano kama hiyo. Lufunga alipewa kadi nyekubdu wakati Simba ilipocheza na Coastal Union, lakini Kamati ya Mashindano ya TFF iliyokutana leo imeitupilia mbali rufaa hiyo na kusema Simba haikuwa na kosa lolote kumtumia mchezaji huyo kwani michuano ya mwaka jana si ya mwaka huu. Alfred Lucas ambaye ni Afisa Habari wa Shirikisho hilo amesema Simba ilikuwa na haki ya kumtumia Lufunga na Polisi Dar haiwezi kupewa ushindi wowote, hata hivyo Polisi Dar haikutimiza vigezo vya uwasilishaji rufaa kwani h

LUFUNGA AIPONZA SIMBA, SASA KUONDOLEWA FA CUP

Picha
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam Kitendo cha Klabu ya Simba kumtumia mchezaji wake Novat Lufunga katika mchezo wake wa kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu kama FA Cup dhidi ya Polisi Dar uliopigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na Simba kushinda mabao 2-0 umeiponza Klabu hiyo. Inasemekana Lufunga alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa michuano hiyo mwaka jana dhidi ya Coastal Union hatua ya robo fainali ambapo Simba iliondoshwa kwa kufungwa mabao 2-1, Lufunga alitolewa kwa kadi nyekundu na kwa mujibu wa sheria hakupaswa kucheza katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo inayosimamiwa na TFF na Bodi ya Ligi. Kwa maana hiyo kamati itakayoketi kuzungumzia sakata hilo inaweza kuiondosha mashindanoni Simba kwa kukiuka kanuni, endapo Simba itaondolewa timu ya Polisi Dar itafuzu hatua ya 16 bora ya mashindano hayo

Misri yaibutua Ghana lakini zote zafuzu robo fainali

Picha
Michezo miwili ya mwisho ya hatua ya makundi ya michuano ya Afcon 2017 imemakizika kwa Misri kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ghana na hivyo kuongoza kundi D kwa alama 7 huku Ghana wakiwa nafasi ya pili kwa alama 6. Bao la ushindi la Mafarao wa Misri lilifungwa na nyota wao Mohamed Salah, katika dakika ya 11 ya mchezo kwa mkwaju mkali wa mpira wa kutenga uliokwenda moja kwa moja nyavuni.. Katika mchezo mwingine wa kundi hilo rimu ya Uganda walitoshana nguvu na Mali kwa kufungana bao 1-1. Michezo ya hatua ya robo fainali itaanza kuchezwa Jumamosi ya Tarehe 28 kwa Burkina Faso kucheza na Tunisia huku Senegar wakicheza na Cameroon. Jumapili kutachezwa michezo miwili ya robo fainali ya pili kwa DR Congo kuchuana na Ghana nao Misri wakikipiga na Morocco ni vita ya Waarabu kwa Waarabu

Ferguson amfagilia Mourinho

Picha
Manchester United wanaendelea kuimarika chini ya meneja Jose Mourinho na ni bahati tu wamekosa lakini wangekuwa wakikabiliana vilivyo na Chelsea amesema meneja wa zamani Sir Alex Ferguson. Ferguson (75) alistaafu kams meneja mwaka 2013 lakini bado ana uhusiano wa karibu na Klabu hiyo ya Old Trafford kwani huhudhuria michezo yao mingi, "Nafikiri Mourinho amefanya kazi kubwa" amesema Ferguson katika mahojiano yake na BBC Sports. Ferguson pia alielezea kwa nini rekodi ya ufungaji magoli ya mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney haitavunjwa na mchezaji yoyote yule karibuni. Jose Mourinho ni meneja wa tatu kuiongoza Klabu ya Manchester United tangu Ferguson kustaafu alipochukua nafasi ya Louis Van Gaal mwezi Mei. Ingawa Mourinho alishinda mechi tatu zake za kwanza akiwa Manchester United, alishinda alama sita pekee kutoka kwa mechi saba za Ligi ya Premia zilizofuata

Simba yamtosa Okwi kisa kiwango

Picha
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM UONGOZI wa Klabu ya Simba umeweka bayana kwamba hawana mpango wa kumsajili mshambuljaji wake wa zamani Emmanuel Anord Okwi raia wa Uganda mpaka pale itakapojiridhisha na kiwango chake. Mwenyekiti wa kamati ya usajilj Zacharia Hanspoppe amesema hayo hasa baada ya kuenea kwa taarifa kuwa Simba inataka kumrejesha mchezaji wake huyo wa zamani ambaye amevunja mkataba wake na Klabu ya Sonderjyjske ya Denmark. Okwi amevunja mkataba na Klabu hiyo ya Ligi Kuu baada ya kutokuwa na uhakika wa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza hivyo akaona ni bora aondoke zake, Lakini meneja wa michezo wa Klabu hiyo akasema Okwi alisajiliwa kutoka Simba kwa lengo la kuisaidia timu hiyo lakini kiwango chake hakijawaridhisha na ndio maana kocha wa timu hiyo alikuwa hamtumii. Hanspoppe amedai kwa sasa hawana mpango wa kumrejesha Msimbazi hadi pale watakaporidhishwa na kiwango chake na hawatamtumia msimu huu labda ujao, Hanspoppe amewataka Wanasimba kutulia na kuachana

Simba kwameguka

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM Katibu mkuu wa Klabu ya Simba Patrick Kahemele ameachia ngazi na kuamua kurejea Kampuni ya Bakhressa Group Limited. Kahemele aliyekuwa katibu wa Simba tangu Juni mwaka jana anarejea Bakhressa Group kwenda kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Michezo ya Azam TV nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Charles Hilary. Gwiji wa habari Charles Hilary sasa anakwenda kuwa Mkurugenzi mtayarishaji wa vipindi vya Azam TV. Katika kipindi chake kifupi cha kufanya kazi Simba Kahemele alionyesha dira ya mabadiliko kabla ya kuondoka ghafla na kurejea Azam. Wazi kuondoka kwa Kahemele aliyeibukia Mtibwa Sugar na baadaye akawa meneja wa Azam FC na mwasisi wa Azam TV ni pengo kwa Simba. Bila shaka mjumbe wa kamati ya utendaji Collin Frisch atarejea kukaimu nafasi hiyo wakati Klabu ikitafuta mtu mwingine

Ivory Coast wavuliwa ubingwa wa Afrika, DR Congo wapeta

Picha
Bingwa mtetezi wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika Tembo wa Afrika Ivory Coast wametupwa nje ya michuano ya mwaka huu baada ya kuchapwa bao 1-0 na Simba wa Astlas Morocco. Goli pekee lililowaondoa miamba hao wa Afrika mashindanoni lilifungwa na Rachid Alioui katika dakika ya 64 ya mchezo. Nayo timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliitambia Togo kwa kuichapa mabao 3-1 na hivyo kufuzu robo fainali wakiwa vinara wa kundi C kwa alama 7 huku Morocco wakishika nafasi ya pili kwa pointi 6. Morocco na DR Congo wamefuzu kupitia kundi hilo huku Ivory Coast na Togo wameondoshwa rasmi

Olunga afuata mamilioni China

Picha
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars Michael Olunga amejiunga na Klabu ya Ligi Kuu ya China Guizhou Hengfeng Zhicheng kwa kitita cha fedha kisichohulikana kutoka kwa Klabu ya Djurgadens IF ya Sweden. Olunga mwenye umri wa miaka 22 aluachiliwa na Djurgadens IF baada ya vilabu vyote viwili kukubaliana. Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya, Olunga alikuwa amesalia na miaka mitatu katika kandarasi yake.  Mchezaji huyo wa zamani wa Gor Mahia na Tusker pua amekuwa akisakwa na Klabu ya Urusi ya CSKA Moscow. Guizhou Zhicheng Hengfeng ilikuwa imemuulizia mshambuliaji huyo na iliripotiwa kuwa tayari kutoa kitita cha shilingi milioni 467 zilizodaiwa na Djugardens.. Olunga pia alikuwa amevutia klabu ya Uturuki ya Galatasaray. Mchezaji huyo aliifungia Gor Mahia mabao 19 katika msimu wa 2015, na kuwasaidia kushinda taji la 15 la KPL pamoja na taji la Top 8 kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya Sweden

TUNISIA YAICHAKAZA ZIMBABWE 4-1, ALGERIA NAO WATUPWA NJE

Picha
Timu ya taifa ya Tunisia imefanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika baada ya kuichakaza Zimbabwe mabao 4-1 mchezo wa kundi B mjini Franceville, Gabon. Mabao ya Naim Slitt, Youssef Msakni, Taha Yassine na Wahbi Khazr yalitosha kabisa kuwapa ushindi huo mnono wakati goli la kufutia machozi la Zimbabwe lilifungwa na Knowledge Musona. Huo ni ushindi mkubwa kabisa katika fainali hizo za mwaka huu, Ssnegar nao wameifungasha virago Algeria baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo mwingine mkali ambao Algeria wangeweza kuchomoza na ushindi. Mchezaji wa Leicester City ya Uingereza Islam Sliman alifunga mabao mawili ya Algeria lakini Mousa Sow na Papa Diop wakasawazisha na kuiondosha Algeria mapema kwenye fainali hizo

Baloteli abaguliwa Ufaransa

Picha
Mshambuliaji wa timu ya Nice nchini Ufaransa Mario Balotelli anasema kuwa alikuwa mwathiliwa wa ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya Ijumaa dhidi ya Bastia. Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa miaka 26 alichapisha katika mtandao wa kijamii akisema ni jambo la kawaida kwamba wafuasi wa Bastia hufanya makelele ya tumbili kwa mechi yote na hakuna mtu katika idara ya adhabu anayechukua hatua. "Kwa hivyo ubaguzi wa rangi ni sheria halali nchini Ufaransa ama ni Bastia pekee? Soka ni mchezo mzuri lakini watu kama wafuasi wa Bastia wanaharibu, ni aibu kubwa'. Balotelli alicheza dakika 90 aluporudi uwanjani baada kuhudumia marufuku katika mechi iliyotoka sare ya 1-1 huko Corsica. Ujumbe huo uliotumwa katika mtandao wa Instagram uliosambazwa na Nice katika mtandao wa Twitter wa klabu hiyo. Jopo la adhsbu la Ligi ya Ufaransa ambalo hutoa maamuzi halijatoa tamko lolote, Balotelli amefunga mabao 10 katika mechin15 tangu kujiunga na Nice katika uhamisho huru kutoka Liverp

CAMEROON YATINGA ROBO FAINALI, GABON OUT

Picha
Wenyeji Gabon wameondoshwa kwenye michuano ya mataifa ya Afrika baada ya kulazimishwa sare tasa na Cameroon katika mchezo mkali na wa kusisimua. Licha ya Gabon kumtumainia nyota wakenAubameyang lakini hawakuweza kupata ushindi na kuifanya Cameroon itinge robo fainali kwa kushika nafasi ya pili kwakuwa na pointi tano na hasa baada ya Burkina Faso kuilaza Guinnea Bissau mabao 2-0 katika mchezo mwingine mkali. Kwa matokeo hayo Burkina Faso wamefikisha pointi tano lakini wanawazidi Cameroon kwa idadi ya magoli ya kufunga, tayari Cameroon imeangukia mkononi mwa Srnegar mchezo ambao unatajwa utakuwa kama fainali kutokana na uimara wa vikosi vyote

Simba yawatafuna Polisi Dar

Picha
Na Ikram Khamees, Dar es Salaam Wekundu wa Msimbazi Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Dar Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup. Ushindi wa Simba ni sawa na ule wa Yanga uliochezwa jana ambapo waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ashanti, hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao moja lililowekwa kimiani na mshambuliaji wake Pastory Athanas. Kipindi cha pili Simba waliongeza bao la pili lililofungwa na Mohamed Hussein Zimbwe Jr au Tshabalala, kwa maana hiyo Simba imeungana na Yanga kutinga hatua ya 16

Ghana yainyuka Mali na kutinga robo fainali, Uganda out

Picha
Ghana imefuzu hatua ya robi fainali ya michuano ya mataifa Afrika baada ya jana kuilaza Mali bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa saa 12 jioni katika dimba la Stade de Gentil Libraville Gabon. Kwa matokeo hayo yanaifanya Ghana ifikishe pointi sita na kutinga hatua ya robo fainali, mchezo mwingine uliopigwa katika uwanja huo huo saa 3 usiku timu ya taifa ya Misri iliichakaza Uganda bao 1-0. Wafungaji wa magoli katika mechi zote, Asamoah Gyan aliifungia Ghana bao LA ushindi, wakati Abdallah Said naye aliipatia Misri bao pekee la ushindi, Uganda sasa wamefungasha virago hasa baada ya kupoteza mechi zote mbili mfululizo na sasa watasaliwa na mechi ya kukamilisha ratiba

Yanga na Ashanti kumenyana leo FA Cup

Picha
Na Sharifu Sharifu, Dar es Salaam Mabingwa watetezi wa kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup, Yanga SC jioni ya leo wanaanza kampeni yao ya kutetea taji lao itakaposhuka uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuumana na Wauza Mitumba wa Ilala Ashanti United. Mchezo huo unatazamiwa kuwa mkali kutokana na timu zote kupokea ratiba ya michuano hiyo ghafla, Ashanti haipewi nafasi kubwa ya kuifunga Yanga kwakuwa ni timu ya daraja la kwanza, lakini inaweza kufanya miujiza na kuchomoza na ushindi. Yanga nao wanauchukulia mchezo huo kama njia ya kuelekea kwenye ushiriki wa michuano ya Shirikisho mwakani, kesho Simba SC itacheza na Polisi Dar katika uwanja huo huo wa Uhuru

Ivory Coast yanusurika kichapo Afcon

Picha
Mabingwa watetezi wa Mataifa ya Afrika, Ivory Coast wamenusurika kichapo kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kufungana mabao 2-2 na DR Congo mechi ikipigwa katika Uwanja wa Stade d'Oyen Libraville Gabon. DR Congo ilitangulia kupata bao la kuongoza kunako dakika ya 9 lililofungwa na Kabano kabla ya Wilfred Bony kuisawazishia Ivory Coast katika dakika ya 26 kipindi cha kwanza. Mshambuliaji hatari wa DR Congo Kabananga alipachika bao la pili katika dakika ya 28, hadi mapumziko DR Congo ilikuwa ikiongoza kwa mabao hayo mawili kwa moja. Mabingwa watetezi Ivory Coast walisawazisha bao katika dakika ya 67 kipindi cha pili likifungwa na Die na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare, lakini katika mchezo mwingine Morocco iliichabanga Togo mabao 3-1

ZANZIBAR KUPEWA UWANACHAMA WA KUDUMU CAF

Picha
Na Saida Fikiri Jr, Dar es Salaam Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) linadikiria kuipa uwanachama kamili Zanzibar badala ya huu ilionao sasa wa muda. CAF katika kikao chake kimepitisha ombi la Zanzibar kuomba uwanachama kwenye Shirikisho hilo, endapo Zanzibar itapewa uwanachama itaweza kushiriki michuano yote inayoandaliwa na CAF. Kwa sasa Zanzibar inaahiriki michuano ya vilabu peke yake lakini kwenye suala la taifa huungana na Bara kuunda Taifa Stars na zile nyinginezo

Malinzi aula Fifa

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Shirikisho la Mpira wa miguu ulimwenguni (FIFA) limemteua Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Jamal Emily Malinzi kuwa mjumbe maalum wa kamati ya maendeleo ya soka duniani. Malinzi sasa atakuwa na jukumu la kuendeleza soka duniani kama.afanyavyo hapa nchini, hii imekaa njema kwa kiongozi wa mpira wa miguu nchini, Malinzi atahudumu katika nafasi hiyp kwa miaka mitano. Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani (Fifa) Gian Infatinho amesema Malinzi ni mtu muhimu katika maendeleo ya mpira wa miguu duniani na kwa jitihada zake anaweza kuisaidia kamati hiyo kufikia malengo yake

Thomas Ulimwengu aanguka miaka miwili Sweden

Picha
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu amesaini mkataba was miaka miwili kujiunga na timu ya Ligi Kuu nchini Sweden ya AFC eskilstuna iliyopanda Ligi Kuu msimu huu. Ulimwengu amejiunga na timu hiyo baada ya kusota kwa muda mrefu tangu alipoachana na timu yake ya TP Mazembe ya DR Congo aliyoiongoza kuipa mataji ya Ligi ya kwao na Afrika. Mshambuliaji huyo amefuata nyayo za Watanzania wenzake Athuman Machupa, Shehan Rashid, Joseph Kaniki na Haruna Moshi ambao wamewahi kucheza Sweden, hata hivyo meneja wa mchezaji huyo Jamal Kisongo amesema kutua Sweden kwa nyota huyo hakuna maana kwamba amefeli. Anadai Ulimwengu alipata ofa mbalimbali Ubelgiji, Ufaransa, Italia, Hispania lakini hakuna hata timu moja iliyokuwa 'Serious' kumchukua, hivyo Ulimwengu kutua Sweden si kwamba amefeli bali amekwenda kuimarisha kiwango chake ili ajiandae kwenda juu zaidi

Mchezaji wa Kagera Sugar afiwa na baba yake

Picha
Na Paskal Beatus, Bukoba Mshambuliaji wa timu ya Kagera Sugar Paul Ngway Ngalyoma amefiwa na baba yake mzazi mzee Lucas Ngalyoma na kumfanya ajiondoe kwenye kikosi hicho ili kushirikiana na familia yake katika msiba huo mkubwa kwake. Akionyesha masikitiko yake, Nahodha wa Kagera Sugar, George Kavila amesema ni pigo kubwa kwao kumkosa Paul Ngway kwakuwa ameondokewa na baba yake mzazi ambaye amefariki dunia. "Huo ni msiba wetu sote, mzee Lucas Ngalyoma alikuwa baba wa mwenzetu hivyo sote tumeumia, tunaamini msiba huu umeipata Kagera Sugar nzima kwani tulianza kumkosa Ngway kwenye mchezo wa jana dhidi ya African Lyon" alisema Kavila huku akiwa na huzuni

SENEGAR WATINGA ROBO FAINALI AFCON

Picha
Senegar imefuzu hatua ya robo fainali ya Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kuichapa Zimbabwe  kwa mabao 2-0. Mabao ya Senegar yamefungwa na Sadio Mane na Henry Salvet aliyefunga kwa mkwaju wa adhabu. Senegar wangeweza kuibuka na ushindi mnono zaidi lakini umahiri wa kipa wa Zimbabwe ulipunguza mabao ya kufunga. Kabla katika kundi hilo, Tunisia waliwafunga Algeria kwa mabao 2-1 na kujiweka katika nafasi ya kufuzu. Senegar ina pointi sita ambazo zimeipa nafasi ya kufuzu. Tunisia inafuatilia ikiwa na pointi tatu, Zimbabwe na Algeria kila moja ina pointi moja na zote zimebakiwa na mchezo mmoja

Rasmi: Jesus kucheza Man City

Picha
Klabu ya Manchester City ya England imepata idhini ya kumnunua rasmi winga wa Kibrazil mwenye umri wa miaka 19 Gabriel Jesus na sasa anaweza akacheza dhidi ya Tottenham Jumamosi ijayo. Jesus amehamia City kutoka Klabu ya Palmeiras ya Brazil kwa £27m. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alikubali kuhamia City kwa mkataba wa miaka mitano Agosti mwaka jana. Alisalia na Palmeiras hadi mwisho wa msimu wa soka Brazil mwezi Desemba. Jesus ana uwezo wa kuibuka kuwa miongoni mwa washambuliaji bora zaidi katika soka, mkurugenzi wa soka wa City Txiki Begiriatain amesema

Mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga ahukumiwa kifungo

Picha
Na Mwandishi Wetu Mchezaji wa zamani wa Tukuyu Star, Ndovu ya Arusha, Yanga na Simba Seleman Mathew Luwongo amehukumiwa kifungo cha kwenda jela miezi 6 bila kulipa faini yoyote baada ya kufanya mkutano wa kisiasa wa hadhara bila ya kibari. Taarifa ambazo Mambo Uwanjani inazo zinasema kuwa Mathew ambaye aliwahi kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amefanya mkutano wa kisiasa akiwa na chama.chake kipya cha CHADEMA mkoani Lindi ambako anakoendesha shughuri sake za kisiasa. Serikali ya Awamu ya tank inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli imepiga marufuku mikusanyiko yote ya kisiasa bila kupata kibari maalum, lakini Mathew na wenzake walikiuka agizo hilo na kujikuta akianzia mwaka 2017 gerezani

Okwi atemwa Denmark, yadaiwa ameshuka kiwango

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Mshambuliaji Mganda Emmanuel Anord Okwi ameamua kuondoka nchini Denmark, Okwi amevunja mkataba wake na Klabu ya Sonderjske Fodbold ambayo alijiunga nayo akitokea Simba. Mkuu wa masuala ya michezo ya Klabu hiyo, Jorgen Hayson amesema Okwi mwenye umri wa miaka 24 ameamua kuvunja mkataba baada ya kuona hajapata namba ya uhakika katika kikosi hicho. "Okwi hakupata nafasi ya kucheza kama ambavyo alitarajiwa lakini kiwango chake pia hakikukua kumshawishi kocha aanze kumpa nafasi kwa kiwango cha juu", alisema na kuongeza. "Mwisho akaamua kuondoka, tumekaa na kufikia makubaliano vizuri, zaidi ninamtakia kila la kheri aendako, alisema. Okwi alitua katika kikosi hicho Julai 2015 akitokea Simba na kusaini mkataba wa miaka mitano na mkataba wake ungeisha mwaka 2020. Hata hivyo mara kwa mara Okwi amekuwa akihusishwa kurejea Simba lakini amekuwa haeleweki, mara kadhaa amekuwa akikanusha na mara nyingine akieleza yuko tayari kuzungumza au yujo taya

Cameroon yakwea kileleni kundi A

Picha
Mabingwa mara nne Cameroon wamekwea kileleni katika kundi A baada ya kupigana na kupata ushindi dhidi ya Guinea Bissau wanaocheza Kombe la Mataifa kwa mara ya kwanza. Guinea Bissau walioshangaza wengi kwa kufuzu katika michuano hii, waliongoza kupitia bao maridadi labPiquito, Cameroon walisawazisha baada ya mapumziko kufuatia mkwaju mkali wa chini nje tu ya eneo la hatari. Michael Ngadeu- Ngadjui akitandika shuti jingine kali na kuansikisha ushindi wa kwanza kwa Cameroon katika michuano hii tangu mwaka 2010. Simba wa Cameroon ambao wakati fulani walikuwa wakitawala soka la Afrika, walishindwa kufuzu katika michuano miwili kati ya mitatu iliyopita, na walipoteza mechi zao zote tatu mwaka 2015. Hata hivyo, baada ya kutoka sare katika mchezo wa kwanza dhidi ya Burkina Faso, sasa wana nafasi kubwa ya kuingia robo fainali. Cameroon wanaongoza kundi lao baada ya mechi nyingine kumalizika kwa sare ya 1-1.. Awali wenyeji Gabon walipigana kufa na kupona na kuokoa pointi moja baada ya kulaz

VAN GAAL AKANUSHA KUSTAAFU UKOCHA

Picha
Aliyekuwa meneja wa Man United Louis Van Gaal amesema kuwa hajastaafu na kwamba anachukua likizo ya muda, Van Gaal mwenye umri wa miaka 65 hajajiunga na timu nyingine tangu aondoke Old Trafford mnamo mwezi Mei mwaka jana. Siku ya Jumatati gazeti moja la Uholanzi De Telegraaf lilisema Van Gaal amemaliza muda wake wa ukufunzi na amestaafu kama mkufunzi hatua iliyoshinikizwa na kifo cha mwanawe. Lakini alikimbilia kituo kimoja cha redio nchini Uhispania Gadena Ser kwanza ijapokuwa kustaafu kunawezrkana bado hajaamua, Raia huyo wa Uholanzi pia alifichua kwamba amekatas kuifunza Klabu ya Uhispania ya Valencia mwezi uliopita. "Iwapo nitaendelea au la pia itategemea na maombi nitakayopata", alisema na kuongeza. "Nimevifunza vilabu vingi na nadhani ni vigumu kuviinua vikiwa katika hali hiyo, sio kweli kwamba nimestaafu, sio sasa, lakini nitaamua mwisho wa likizo yangu mwezi Juni ama Julai mwaka huu", alisema Van Gaal

Mtibwa yaibana koo Simba

Picha
Na Ikram Khamees, Morogoro Simba SC ya Dar es Salaam jioni ya leo imeshindwa kuchomoza na ushindi baada ya kulazimishwa sare isiyo na mabao 0-0 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kukaa kileleni ikifikisha pointi 45 ikiongoza kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya hasimu wake mkuu Yanga SC ambao jana walishinda 1-0 dhidi ya Majimaji ya Songea. Mchezo wa leo ulikuwa mkali ambapo kila timu ikicheza vizuri lakini ngome ya ulinzi ya Mtibwa iliyokuwa ikisimamiwa vema na Henry Joseph iliwazuia kabisa washambuliaji wa Simba waliokuwa wakiongozwa na Mrundi Laudit Mavugo

Misri walazimishwa suluhu na Mali

Picha
Timu ya taifa ya Mali jana imeilazimisha sare tasa Misri 'Pharao' 0-0 mchezo wa kundi D Mataifa ya Afrika inayoendelea huko Gabon. Kwa matokeo hayo Ghana itakuwa kileleni kwa pointi zake 3 baada ya jana kutangulia kushinda 1-0 dhidi ya Uganda ambao ni wawakilishi wa Afrika mashariki

Ni kivumbi na jasho Simba na Mtibwa

Picha
Na Ikram Khamees, Morogoro Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC jioni ya leo inakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Simba wataingia katika mchezo huo ikiwa na lengo moja la kushinda mchezo huo ili iweze kufufua matumaini ya kutwaa ubingwa wa bara baada ya kushindwa kuutwaa kwa muda wa miaka minne mfululizo. Endapo itashinda katika mchezo huo itafikisha pointi 47 na kuzidi kuiacha Yanga iliyo katika nafasi ya pili na pointi 43, lakini Mtibwa Sugar wanaonolewa na Salum Mayanga wametamba kuibuka na ushindi katika mchezo huo. Mtibwa inawategemea zaidi Shaaban Mussa Nditi, Haroun Chanongo na Rashid Mandawa wakati Wekundu wa Msimbazi nao tumaini lao lipo kwa Shiza Kichuya, Muzamiru Yassin na Mohamed Ibrahim ' Mo'

YAYA TOURE AKATAA MAMILIONI YA WACHINA

Picha
Kiungo wa kati wa Klabu ya Manchester City Yaya Toure amekataa ombi la mshahara wa pauni 430,000 kwa wiki kutoka China. Toure mwenye umri ws miaka 33 amevutia timu nyingi katika ligi ya China wakati ilipoonekana kwamba huenda asishirikishwe katika mechi zozote chini ya mkufunzi Pep Guardiola. Aliamua kutoondoka wakati huo na akakatas tena alipopewa kitita hicho wakati wa dirisha hili la uhamisho, kandarasi ya raia huyo wa Ivory Coast inakamilika mwishoni mwa msimu huu. Toure amekuwa mchezaji muhimu wa City tangu aliporudishwa katika kikosi cha kwanza na alianza mechi yake ya saba mfululizo wakati wa kushindwa kwa mabao 4-0 dhidi ya Everton katika ligi ya Uingereza hapo Januari 15 mwaka huu. Nyota huyo yuko huru kuingia mkataba na klabu yoyote ughaibuni tangu Januari lakini imedaiwa kwamba bado anaipenda ligi ya Uingereza na timu yake ya City, Toure hajapata hakikisho lolote kugusu kandarasi kutoka kwa kocha wake Guatdiola

Ghana yaichapa Uganda Afcon

Picha
Timu ya taifa ya Ghana 'Black Stars jioni ya leo imeanza vema kampeni yake ya kutwaa ubingwa wa mataifa ya Afrika baada ya kuilaza bao 1-0 timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes' katika mchezo mkali na wa kusisimua uliofanyika nchini Gabon. Iliwachukua Ghana kupata penalti iliyowekwa kimiani na Andwer Ayew na kuipa ushindi nchi yake ambayo sasa inaongoza kwenye kundi lake ikiwa na pointi 3, Misri na Mali zitaumana katika mchezo mwingine unaofuata. Farouk Miya nusura aisawazishie bao Uganda lakini jitihada zake zilishindikana na hadi mwisho wa mchezo Ghana washindi wa pili wa mataifa ya Afrika iliyopita wametoka kidedea kwa ushindi huo mdogo dhidi ya watoto wa Yoweri Museveni

Yanga yavunja mwiko Songea, yaigagadua Majimaji 1-0 na kuisogelea Simba kileleni

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Songea Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Dar Young Africans maarufu Yanga, jioni ya leo imejiongezea pointi tatu baada ya kuilaza Majimaji bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa uwanja wa Majimaji mjini Songea. Mchezo ulikuwa mkali na wa kusisimua huku wenyeji Majimaji wakiliandama lango la Yanga kama nyuki na kama si uimara wa mabeki wa Yanga na kipa wao huenda matokeo yangekuwa mengine. Yanga walitangulia kupata bao la mapema kabisa likifungwa na Deus Kaseke, hata hivyo Yanga nao watajilaumu kufuatia washambuliaji wake kutokuwa makini, kwa ushindi huo wa leo Yanga imevunja mwiko wa kutoifunga Majimaji kwenye uwanja wa nyumbani kwao tangu mwaka 1985. Yanga pia imeamsha mbio za kuifukuza Simba kileleni kwani imefikisha pointi 43 ikiwa nyuma ya pointi moja na Simba inayoongoza Ligi hiyo, Simba kesho itacheza na Mtibwa Sugar uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro

Majimaji na Yanga nani kucheka leo?

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Songea Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga SC, jioni ya leo wanashuka Uwanja wa Majimaji mjini Songea kuwavaa wenyeji wao 'Wana Lizombe' Majimaji mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL). Majimaji inayonolewa na Kally Ongala mchezaji wa zamani wa mabingwa hao watetezi na Azam FC, Mchezo huo utakuwa wa kisasi kwani Majimaji ilifungwa mabao 3-0 na Yanga zilipokutana Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa mara ya kwanza. Hivyo leo Majimaji inataka kulipiza kisasi na pia inataka kujinusuru kutoka mkiani, Yanga nao wanataka kuendeleza ubabe kwa Majimaji lakini pia inataka kuwapa furaha mashabiki wake baada ya kutolewa kwenye kombe la Mapinduzi huko Zanzibar na kikubwa zaidi wanataka kuwapoza mashabiki wao. Kwa vypvyote pambano litakuwa kali na la kusisimua, Yanga waliwasili mjini Songea Jana jioni wakipitia Tunduru kwa basi ambako walipata mapokezi makubwa toka kwa mashabiki wao