SIMBA ZIARANI UTURUKI LEO
Na Paskal Beatus. Dar es Salaam
JUMLA ya wachezaji 26 wa kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba SC wameondoka alfajiri ya leo kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kambi ya majuma mawili kujiandaa na msimu mpya WA Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bars.
Simba ilianza safari yakr jana ambapo baadhi ya viongozi na watendaji walianza kusafiri pamoja na vifaa itakavyotumia ikiwa huko, Simba imepanga kufikia katika mji wa Antalya ambao upo kilometa 15 kutoka mji mkuu wa Istanbul.
Wekundu hao watacheza mechi tatu za kirafiki na kwa mujibu wa viongozi wake wamesema kikosi chao kitarejea Agosti 5 mwaka huu na kitacheza mchezo WA kirafiki WA Simba Day kabla hakijaenda mjini Lindi kucheza mechi ya kirafiki na Namungo FC katika uzinduzi WA uwanja wa Majaliwa Stadium