YANGA YAKIONA CHA MOTO, YAPIGWA 4-0 NA GORMAHIA

Na Salum Fikiri Jr. Nairobi

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Yanga Sc usiku huu imeambulia kichapo cha mbwa mwizi baada ya kufungwa mabao 4-0 na Gor Mania ya Kenya katika mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika uwanja wa Kasarani mjini Nairobi.

Gor Mahia ilitawala eneo la katikati na kuwafanya Yanga washindwe kulishambulia lango lao hivyo ilikuwa rahisi kwao kulisakama mango LA Yanga na dakika ya 22 kipindi cha kwanza, mshambuliaji Jacques Tuyisenge aliipatia Gor Mania bao LA kwanza kabla ya Ephrahim Guikan kufunga la pili dakika ya 45.

Hadi mapumziko Gor Mania walikuwa wanaongoza kwa mabao hayo mawili, kipindi cha pili Gor Mahia waliendeleza kasi yao na Mwinyi Haji WA Yanga akajifunga katika dakika ya 65 na kufanya Gor Mania kupata bao LA tatu kabla tens Guikan kufunga bao la nne dakika ya 85, kwa matokeo hayo Gor Mahia inafikisha pointi tano na kukaa kileleni huku Yanga ikiburuza mkia

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA