KCB kudhamini Ligi Kuu Bara

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Benki ya biashara ya Kenya (KCB) imeingia mkataba na Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) wa kuidhamini Ligi Kuu Tanzania Bara wenye thamani ya shilingi Milioni 409 za Kitanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya utiaji saini ya mkataba huo, Rais wa Shirikisho la soka nchini Wallace Karia amesema KCB imeingia mkataba wa kuidhamini Ligi Kuu Bara 2018/2019 ikiwa kama mdhamini mwenza huku jitihada zikiendelea kumpata mdhamini mkuu wa ligi hiyo.

Mkataba huo ulisainiwa asubuhi katika hoteli ya Serena iliyopo mjini Dar es Salaam, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom bado haijathibitisha kama itadhamini tena ligi hiyo ama itaachana moja kwa moja na udhamini huo hasa baada ya mkataba wao kumalizika

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI