Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2023

RAINFORD KALABA AISAPOTI POWER DYNAMOS

Picha
Gwiji wa Chipolopolo na TP Mazembe Rainford Kalaba ameiunga mkono Power Dynamos kuifunga Simba SC ya Tanzania wikendi hii katika mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika wikendi hii. Ikumbukwe Kuwa Dynamos ina mlima mkubwa wa kupanda baada ya kutoka sare ya 2-2 nyumbani katika mechi ya kwanza. Walifunga Goli La Kwanza kupitia kwa Joshua Mutale na Cephas Mulombwa, lakini juhudi zao zikazimwa na Clatous Chama, aliyefunga mabao yote Mawili Ya kusawazisha Huku kukiwa na uchezaji mkali unaohitajika ili kusonga mbele kwa raundi zinazofuata, Kalaba anaiambia Duniayetu kwamba bado haijakamilika kwa Aba Yellow. "Wasahau Kuhusu Matokeo Ya Kwanza, Wachukulie Kama Zile ni Dakika 45 Za Kipindi Cha Kwanza, Na Ni rahisi Power Dynamos Kuwafunga Simba sc Pale Tanzania Kuliko Simba Sc Kuwafunga Yeah Maana Wao Watakuwa Na Presha Kubwa Mbele Ya Mashabiki Wao" Alisema Rainford Kalaba Aliongeza Na Kusema "Katika Mpira Lolote Linawezekana, Na Hakuna Timu Isiyofungika na Kama Mliwaf

YANGA HAOOO MAKUNDI

Picha
Na Fikiri Salum MABINGWA wa soka Tanzania bara, Dar Young Africans, maarufu Yanga SC usiku wa leo imefuzu hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika, baada ya kuichapa bao 1-0 timu ya El Merreikh ya Sudan katika uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.  Kwa ushindi huo Yanga SC inatinga moja kwa moja hatua ya makundi, hasa baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3-0. Yanga ilitangulia kushinda kwa mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika uwanja wa Pele mjini Kigali nchini Rwanda.  Goli pekee la Yanga lilifungwa na Walid Clement Mzize, kesho wawakilishi wengine wa Tanzania Simba SC watawakaribisha Power Dynamos katika uwanja huo huo wa Azam

DUBE KUIKOSA YANGA

Picha
Klabu ya Azam FC imetangaza kuwa Mshambuliaji wao hatari,Prince Dube anatarajiwa kukaa nje ya Uwanja kwa mda wa wiki tatu kufuatia kupata majeraha ya nyonga kwenye Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo Azam ilikutana na Singida Fountain Gate FC. Kwenye mda ambao atakuwa nje Prince Dube atakosa mechi mbili za Ligi Kuu ambazo zitakuwa ni dhidi ya Dodoma Jiji pamoja na Coastal Union na huku kama akopona mapema huenda akarudi Uwanjani kwenye mechi kati ya Azam FC dhidi ya Yanga ambayo itakuwa October 25 ikiwa ni siku nne tangu mda ambao amepangiwa na Daktari wa kukaa nje ya Uwanja kuisha. Pia Azam FC imetangaza kuwa Kiungo Mshambuliaji wao,Yahya Zaidi Pia atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki tatu kufuatia kuchanika kwa Kiraba (meniscus) kinachokuwa katikati ya goti, kinacholiimarisha lisikwaruzane. Kiraba hicho pia huwezesha goti kufanya kazi vizuri kwa maana ya kukunja na kukunjua.

AZIZ KI AKIRI YANGA YA MSIMU HUU NI KALI

Picha
Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Aziz Stephanie Ki amesema kuwa kikosi cha timu hiyo msimu huu ni bora zaidi kuliko msimu uliopita kwani wameanza vizuri kwenye mechi zao na kila mmoja ana uwezo wa kufunga badala ya kumtegemea mchezaji mmoja. Aziz Ki amesema hayo kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Merrikh ya Sudan itakayopigwa leo Septemba 30, 2023 katika dimba la Azam Complex, Chamazi. Katika mechi tatu za Ligi, Yanga imeshinda mechi zote ikiwa imefunga mabao 11 bila kuruhusu bao hata moja wakati kwenye Ligi ya mabingwa, katika mechi tatu wamefunga mabao 9, na kuruhusu bao 1 pekee. “Siwezi kuwaahidi lolote mashabiki kwa sababu hujui lolote kuhusu kesho, lakini jambo la muhimu ni kujituma kwa sababu timu ilinisajili kwa kuwa inataka kuingia hatua ya makundi. Msimu uliopita haikuwezekana lakini tunamshukuru Mungu. “Huu msimu timu yetu iko imara zaidi ya msimu uliopita kwa ninavyoiona mimi. Kila mchezaji anacheza vizuri kwa hiyo tunaamini timu itashinda na k

WINGA ANAYETAKIWA SIMBA, AKIRI YEYE NI YANGA DAMU

Picha
Winga wa timu ya Power Dynamos ya Zambia Joshua Mutale ameweka wazi kwamba yeye ni Yanga kwa sababu alifurahishwa na mafanikio ya timu hiyo na kuamua kuvaa jezi zao. Mutale anahusishwa kujiunga na Simba SC hasa baada ya kuichachafya timu hiyo katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya mabingwa Afrika uliofanyika Ndola, Zambia na timu hizo kufungana mabao 2-2. Winga huyo alikutwa amevaa jezi za Yanga katika ukurasa wake wa istagram, lakini alipoulizwa kwanini amevaa jezi ya Yanga huku yeye akotakiwa na mahasimu wao wakuu, amedai aliipenda Yanga kutokana na soka lao la kuvutia, pia anekiri kutaka kuja kucheza Tanzania ingawa hajaitaja Simba wala Yanga

HATUTAFANYA HAMASA- AHMED ALLY

Picha
Meneja wa Habari wa klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema klabuvyake haitafanya hamasa kuelekea mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Power Dynamos kwakuwa uwanja utaingiza watu wachache. Ahmed Ally amedai wataitumia mechi hiyo kama sehemu ya maandalizi ya kujiandaa na michuano ya African Football League itakayoanza hivi karibuni. "Hatutafanya hamasa kubwa maana tunaweza kuwatia watu mzuka alafu tutakosa sehemu ya kuwaweka, itakuwa ya kawaida sababu watu 7,000 tutajaza kwa haraka." "Mechi hii tutaitumia kama maandalizi ya kwenda kucheza CAF Football League."- Ahmed Ally.

YANGA KUENDELEZA 5G KESHO?

Picha
Kikosi cha wachezaji wa wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga SC leo wameendelea kujifua wakijiandaa kucheza kesho na wawakilishi wa Sudan,El Merreikh katika uwanja wa Azam Complex, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Yanga inahitaji sare yoyote au kufungwa goli moja ili iweze kusonga mbele kwani mpaka sasa ina ushindi wa mabao 2-0 iliyoupata Kigali, Rwanda katika mchezo wa mkondo wa kwanza ambapo El Merreikh ilikuwa nyumbani.

TIMU YA PAPE SAKHO WA SIMBA HOI UFARANSA

Picha
Timu Iliyomsajili Pape Sakho, QR Metropole ya Ufaransa Inayoshiriki Ligi Daraja La Pili Nchini Humo Imecheza Michezo 8 Ya Ligi 2, haijashinda Hata Mmoja, Imetoa Sare 2, na Kukung'utwa 6, Ikifunga Magoli 6 na kupigwa Magoli 12, Ikiwa na points 2 Pekee, Points Zinazoisaidia Timu ya Pape Sakho Kushika Mkia Katika ligi hiyo. Katika michezo hiyo 8, Kijana Machachari Pape Sakho Hajaona Hata Dakika 1, Hata Benchi Hajawahi Onja katika michezo hiyo 8 hadi sasa.

KWA TIZI HILI LA EL MERREIKH YANGA AKICHOMOKA JEURI

Picha
Kikosi cha El Mereikh kimefanya mazoezi yake jioni ya leo kwenye Uwanja wa Azam Complex tayari kwa Mchezo wao wa Marudiano wa Kufuzu hatua ya Makundi ya #CAFChampionsLeague dhidi ya Yanga SC hapo kesho. .

ASANTE KWASI AIPONZA TABORA UNITED, YAFUNGIWA TENA NA FIFA

Picha
Klabu ya Ligi Kuu ya NBC ya Tabora United ambayo ilikuwa ikiitwa Kitayosce FC imefungiwa kufanya usajili wa wachezaji wa kimataifa mpaka itakapomlipa mchezaji Asante Kwasi. Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya mchezaji huyo raia wa Ghana kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo akidai malipo ya ada ya usajili na malimbikizo ya mshahara. “Klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo,” imesema taarifa iliyotolewa na TFF. Mbali na uamuzi huo wa FIFA kuifungia klabu hiyo kufanya usajili, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa ndani.

SIMBA WAJIFUA VIKALI KUIUA POWER DYNAMOS

Picha
Kikosi cha wachezaji wa Simba SC wanaendelea kujiandaa, kujipima na kuangalia wapi kuboresha kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.  Kikosi hicho kinajifua katika uwanja wake wa Mo Simba Arena uliopo Bunju B nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam

MWONEKANO WA UWANJA UTAKAOJENGWA ARUSHA KWA AJILI YA AFCON

Picha
Mwonekano wa uwanja mpya wa Arusha utakaojengwa na serikali jijini Arusha ikiwa sehemu ya maandalizi ya kuandaa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2027 ikishirikiana na Kenya na Uganda.  Uwanja huo utakaojengwa katika Kata ya Olmoti utakuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 30,000 waliokaa.

FEITOTO AFURAHIA KUPUNGUA UZITO

Picha
Kiungo fundi wa soka anayekipiga Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amekiri wakati anajiunga na timu hiyo alikuwa chibonge. Lakini kwa sasa amejitahidi kupambana hadi kukata zaidi ya kilo sita na kujiona mwepesi na kuanza kurejesha makali aliyokuwa nayo enzi akiitumikia Yanga. . Kiungo huyo alisema awali alipojiunga Azam alikuwa na uzito wa kilo 75, lakini baada ya kupigishwa tizi la maana kwa sasa amebaki na kilo 69 na kujiona mwepesi na kurejea kwenye ule utamu uliompa mashabiki akiwa na Yanga aliyoichezea misimu minne. . Fei alisema wakati anaanza kucheza alipata wakati mgumu sana, kwani alikuwa kibonge ila anamshukuru sana kocha kwani alimsaidia mno na kumrejeshea katika hali ya kuwa fiti.  “Timu ilinipatia mkufunzi maalum wa kunifundisha mazoezi binafsi yalinisaidia kurudi katika hali, kwani nilikaa nje karibu miezi minne bila kucheza na kwa bahati nimepunguza uzito na sasa nimeanza kurejea katika makali niliyokuwa nayo Yanga,” alisema Fei Toto.

MWAKINYO AGOMEA PAMBANO

Picha
Na Mwandishi Wetu Bondia Hassani Mwakinyo wa Tanzania ameweka wazi kesho hatopanda ulingoni kutokana na uongo na udanganyifu wa mapromota baada ya kubadilishiwa mpinzani wa awali Rayton Okwiri na kupewa bondia Julius Indongo wa Namibia

RAIS SAMIA AFURAHIA TANZANIA, KENYA NA UGANDA KUPEWA UENYEJI AFCON

Picha
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefanikiwa kuwa wenyeji wa michuano mikubwa ya soka Afrika (AFCON2027), tukishirikiana na Kenya na Uganda.  Nawapongeza nyote mlioshiriki kuhakikisha nchi yetu inapata fursa hii adhimu. Nawaagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha tunafanya maandalizi mazuri. Ikiwemo kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu, viwanja viwili vipya vya kisasa vya michezo Arusha na Dodoma.

MAJOGORO AWA MCHEZAJI BORA SAUZI

Picha
Mtanzania Baraka Majogoro (26) hapo jana aliibuka Mchezaji bora wa mechi ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini 🇿🇦 wakati timu yake ya Chippa Utd ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Super Sport Utd. Chippa Utd bila Majogoro 🤝 Kaizer Chiefs 0-0 Chippa Utd 🤝 Chippa Utd 0-0 Ts Galaxy 🤝 Chippa Utd 1-1 Orlando pirates ❌ Chippa Utd 0-2 Mamelodi Chippa wakiwa na Majogoro ✅ Cape Town Spurs 0-1 Chippa Utd (90') ❌ Chippa Utd 2-3 Royal AM (90') ✅ Richards Bay 1-2 Chippa Utd (90') ✅ Chippa Utd 1-0 Super Sport (90') Chippa Utd wanashika nafasi ya 4️ kwenye Msimamo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini wakiwa na alama 12 katika mechi 8️ walizocheza hadi sasa.

KOCHA EL MERREIKH AKIRI WATAPATA USHINDI DHIDI YA YANGA

Picha
"Young Africans SC ni miongoni mwa timu zinazoogopwa kwa sasa Barani Africa. Sisi Al-Merrikh tutawaheshimu lakini hatutakaa nyuma, kama Yanga waliweza kupata magoli mawili ugenini hata sisi tunaweza kupata magoli mawili ugenini, Dar es Salaam." Osama Nabieh,Kocha wa klabu ya Al-Merrikh

SIMBA KUCHEZA SAA 10 NA POWER DYNAMOS

Picha
"Mchezo dhidi ya Power Dynamos utachezwa siku ya Jumapili Oktoba mosi saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex. Tumeamua kucheza saa 10 sababu michezo mingi hapa karibuni tumecheza muda huo hivyo hatukutaka kubadili muda lakini pia Jumatatu itakuwa siku ya kazi hivyo tunataka watu wawahi kurudi nyumbani." "Kuelekea kwenye mchezo huo ambao ndio utafatiliwa zaidi Afrika kwa wikiendi hii kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza. Ukubwa wa Simba SC ndio unafanya mchezo huo uwe mkubwa zaidi." "Kikosi leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex pale Chamazi kwa ajili ya kuzoea uwanja. Tangu tumeanza msimu huu hatujawahi kutumia ule uwanja. Wapo wachezaji wetu wengi wanaujua uwanja ule na wpao wengine hawaujui." "Wachezaji watatu watakosekana kwenye huo mchezo. Wachezaji hao ni Aishi Manula, Henock Inonga na Aubin Kramo."- Ahmed Ally.

SIMBA WASHINDWE WENYEWE KWA POWER DYNAMOS

Picha
Na Ikram Khamees Mabingwa wa Zambia Power Dynamo watakosa huduma ya wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza katika mchezo wa mkondo wa pili wa klabu bingwa dhidi ya Simba SC Tanzania utakaochezwa Jumapili hii. Nyota hao ni goli golikipa Lawrence Mulenga na Dominic Chanda, Lawrence aliumia vibaya na kuwahishwa hospitali katika mechi dhidi ya Zesco, Mulenga aligongana Kelvin Kamapamba na kupoteza fahamu. Kwa upande wa beki wa kati wa klabu hiyo Dominic Chanda yeye alionyeshwa kadi nyekundu katika mkondo wa kwanza wa michuano hiyo uliochezwa Zambia na timu hizo kutoka sare.

NYOTA YANGA KAMILI KUIVAA EL MERREIKH

Picha
Wachezaji wa Kikosi cha Yanga wameanza mazoezi ya kujiandaa na Mchezo wa marudiano wa Kufuzu hatua ya Makundi ya #CAFChampionsLeague dhidi ya El Mereikh ya Sudan utakaopigwa Septemba 30,2023 kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa moja kamili jioni. Beki wao wa kushoto,Joyce Lomalisa amepona maumivu aliyoyapata kwenye Mechi ya Yanga dhidi ya Namungo FC na yupo fit kwaajili ya kuwatumikia Wananchi. .