MBAO FC YAMTAMBULISHA PASTORY ATHANAS
Na Paskal Beatus. Mwanza
Klabu ya soka ya Mbao FC ya jijini Mwanza nayo imeendelea kujiimarisha kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kumtambulisha rasmi mshambuliaji wa zamani wa Stand United, Simba SC na Singida United, Pastory Athanas kuitumikia timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Athanas aliyewahi kucheza Simba SC nusu msimu kisha kutupiwa virago amejiunga na timu hiyo ya jijini Mwanza inayonolewa na beki wa zamani wa Simba, Amri Said "Steam" na sasa kikosi hicho kinajivunia kumpata straika Hugo machachari.
Tayari timu hiyo imeshafanikiwa kunasa baadhi ya mastaa mbalimbali ambao watakuja kuipa mafanikio, ujio wa Athanas ni kuondoka kwa kiungo mshambuliaji wake Habib Kiyombo aliyejiunga na Singida United