Dakika za mwisho mwisho Simba yambakiza Ndemla, Apaa
Na Aisha Maliyaga. Dar es Salaam
Dirisha la usajili limefungwa Jana usiku ambapo klabu zote 20 zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania zimetakiwa kukamilisha kila moja wapo, Simba imelifunga dirisha hilo kwa staili ya kipekee.
Unaambiwa jana imemalizana na kiungo wake Said Ndemla na ikampandisha ndege kuelekea Uturuki kuungana na wenzao waliotangulia juma lililopita, Simba iliondoka na kikosi cha wachezaji 26 tu ikimwacha Ndemla asubirie kwanza kumalizana na uongozi, Ndemla pia alikuwa akiwaniwa na klabu ya AFC Eskilistuna ya Sweden.
Pia Simba imemchukua kiungo wa Mtibwa Sugar Hassan Dilunga na sasa wote hao pamoja na Erasto Nyoni, Meddie Kagere na Haruna Niyonzima wamesafiri kuelekea Uturuki kuungana na wenzao, Simba pia imewaacha Jamal Mwambeleko, Ally Shomari, Said Mohamed Nduda, Moses Kitandu, Juuko Murushid na Laudit Mavugo