Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2014

AMISSI TAMBWE NAYE ATAKA KUONDOKA SIMBA

Picha
Mfungaji bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara,  Mrundi, Amissi Tambwe, ameutaka uongozi wa klabu hiyo kumpa barua ya kuondoka klabuni hapo kama umemchoka na siyo kumsingizia mambo ya ajabu ambayo hajafanya na wala hatarajii kuyafanya. Tambwe ambaye alijiunga na Simba msimu uliopita akitokea Vital’O ya Burundi na kufanikiwa kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufunga mabao 19, hivi sasa hana amani tena katika kikosi cha timu hiyo. Hali hiyo inatokana na hivi karibuni baadhi ya viongozi wa Simba kumtaja kuwa anaihujumu timu hiyo akishirikiana na baadhi ya wachezaji wenzake.

RAIS MICHAEL SATA WA ZAMBIA AFARIKI DUNIA

Picha
Familia ya Bwana Sata wameiambia BBC kuwa Rais wa Zambia, Michael Sata, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77 katika hospitali ya London alikokuwa akitibiwa ugonjwa ambao haujatajwa.   Kifo chake kimetokea siku chache baada ya Zambia kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo. Mwanasiasa huyo mkongwe aliingia madarakani mwezi Septemba 2011 baada ya kuongoza chama chake cha Patriotic Front, na kumshinda Rupiah Banda, ambaye alikuwa rais wakati huo na chama chake cha Movement for Multi-Party Democracy, kikiwa madarakani kwa miaka ishirini.

MAKALA: KINACHOTOKEA SIMBA SASA NI UHARIFU KWA WACHEZAJI, HANSPOPPE AOMBE RADHI, SPUTANZA NI WAKATI WENU SASA KUKEMEAS

Picha
AWALI wakati wa majira ya usajili nchini, timu ya kandanda ya Simba SC iliamua kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake. Ikiwa chini ya rais, Evance Aveva, Simba iliamua kumfuta kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mcroatia, Zdravko Logarusic na kumuajiri, Patrick Phiri kutoka Zambia. Mabadiliko yalifanyika hasa, wachezaji wa kila aina walisajiliwa huku wale walioshindwa kufanya vizuri msimu uliopita wakiachwa. Lengo ya uongozi mpya ilikuwa ni kuifanya klabu ya Simba kurudi katika hali yake ya ushindani ambayo katika kipindi cha miezi 34 sasa imeshuka kwa kiwango kikubwa.

OKWI AJIFUNGA MIAKA MIWILI SIMBA

Picha
Kiungo mshambuliaji wa Simba,   Mganda, Emmanuel Okwi,   ameongeza mkataba wa kuichezea timu hiyo akisaini miaka miwili. Awali, kiungo huyo mwenye kasi kubwa uwanjani,   alisaini mkataba wa miezi sita ya kuichezea timu hiyo akitokea Yanga, akiondoka kwa mgogoro mkubwa. Meneja wa kiungo huyo,   Abdulfatah Saleh,alisema kuwa Okwi ameongeza mkataba huo baada ya kufikia makubaliano ya pande mbili kati yao na klabu hiyo.

PHIRI ATAMBIA REKODI KUIFUNGA YANGA

Picha
Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri, amesema rekodi yake nzuri katika mechi dhidi ya watani wa jadi ndiyo 'itakayowamaliza' wapinzani wao Yanga katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo itafanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba iko jijini Johannesburg, Afrika Kusini kujiandaa na mchezo huo ambao huvuta hisia za mashabiki wa soka ndani na nje ya nchi. Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili, Phiri ambaye katika misimu miwili tofauti aliyoinoa Simba kabla ya huu amefungwa mara moja tu na Yanga, alisema kambi ya Simba huko Afrika Kusini haiangalii mechi moja dhidi ya watani hao wa jadi, ila ni maalumu kurejesha morali kwa wachezaji msimu huu na haifikirii timu hiyo peke yake.

RAHEEN STERLING ARUDI MZIGONI LIVERPOOL, 'DOGO'YUKO FITI KINOMA'

Picha
KIUNGO wa Liverpool, Raheem Sterling amerudi jana mazoenini katika uwanja wa Melwood kufuatia kuzuka utata katika ombi lake la kutoanza kikosi cha England kilichoshinda bao 1-0 dhidi ya Estobia kwasababu ya uchovu.

CHANGAMOTO KUBWA WENGER AKIONDOKA – GAZIDIS

Picha
Changamoto kubwa kwa Arsenal itakuwa kutafuta meneja atakayechukua nafasi ya Arsene Wenger atakapoondoka Arsenal. Hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu Ivan Gazidis. Wenger, ambaye atafikisha umri wa miaka 65 Oktoba 22, alisaini mkataba wa miaka mitatu mwezi Mei. "Changamoto kubwa tutakayokabiliana nayo kama klabu, ni kipindi cha mpito kutoka kwa Arsene Wenger kwenda kwa meneja mwingine," amesema Gazidis. "Tuna meneja mzuri sana. Arsene wameiweka klabu mahala pazuri mno."

YANGA WAANZA KUINGIWA NA KIWEWE MECHI YA SIMBA, YONDANI, CANNAVARO HATIHATI KUCHEZA

Picha
Wanachama na wapenzi wa Yanga SC wameendelea kuilaumu TFF inayoongozwa na rais Jamal Malinzi kwa kitendo chao cha kuihujumu kuelekea mchezo wa watani wa jadi jumamosi. Wanachama hao wa Yanga wamelia na TFF kwa kitendo chao cha kuahirisha mchezo wao dhidi ya Simba SC ambao ulikuwa uchezwe Oktoba 12 ili kupisha timu ya taifa, Taifa Stars iliyocheza na Benin. Wameendelea kusema kuwa kusogezwa kwa mechi yao na kuipisha timu ya taifa ilikuwa mbinu ya kuihujumu Yanga kwani kalenda ya Fifa ilikuwa wazi kabla hata ratiba ya ligi ya kuu haijatoka.

MKOLA MAN AGEUKIA MALAVIDAVI

Picha
STAA wa ngoma ya ‘Mr Mapesa iliyosumbua sana katika vituo vya redio Christopher Mhenga ‘Mkola Man’ majuzi kati aliachia ngoma nyingine ya mapenzi ‘malovedav time’ katika studio za Hekman Record zilizopo jijini Dar es salaam chini ya prodyuza Galaton Money Devil. Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, Mkola Man alisema ameamua kutengeneza wimbo wa mapenzi kutokana na muda uliopo, ‘nimeona nifanye wimbo wa mapenzi kwa sababu huu ndio wakati wake, hakuna asiyejua utamu wa mapenzi, kila siku naimba nyimbo za kigumu sasa nimekuja kumridhisha wangu mpenzi’, alisema Mkola Man. Wimbo huo ameamua kumshirikisha mshirika wake wa karibu Yusa G, Amour Jay na Fabby ‘Bamaboy’, Mkola Man anamshukuru sana meneja wake Dk Sakaingo ‘Big Boss’ ambaye amemwezesha kurekodi wimbo huo na kugharamia mambo mengine.

PELLE KUICHEZEA ITALIA KWA MARA YA KWANZA

Picha
Graziano Pelle   Straika wa klabu cha ligi ya Premier ya Uingereza, Graziano Pelle anatarajiwa kuchezea taifa lake la kuzaliwa Italia kwa mara ya kwanza kwenye ngoma ya kufuzu Kombe la Euro la 2016 dhidi ya Malta. Wana Azzurri wanalenga kushinda mechi ya tatu mtawalia katika Kundi H baada ya kukomesha Norway (2-0) na Azerbaijan (2-1) huku vijana wa Antonio Conte wakilaumiwa kwa kukosa nafasi nyingi mbele ya lango. Washambuliaji Ciro Immobile (Borussia Dortmund) na Simone Zaza (Sassuolo) walialika gadhabu ya wengi kwa kutupa fursa nyingi dhidi ya Azerbaijan Ijumaa jijini Palermo na kocha huyo amekita matumaini yake na Pelle.

AUNT EZEKIEL AMKANA WAZIRI NYALANDU MAREKANI

Picha
Mwigizaji wa filamu nchini, Aunty Ezekiel amekanusha uvumi ulioenea kuwa alikwenda nchini Marekani akifuatana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu . Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Aunty alisema hadi sasa haelewi nia ya wanaovumisha habari hiyo isiyokuwa na chembe ya ukweli wowote. “Mashabiki wangu wajue nilikwenda Marekani kwa mwaliko wa Blogu ya Vijimambo, ambao walitaka nikashiriki katika sherehe yao ya kutimiza miaka minne, wakati wote nilikuwa na mwenyeji wangu, Lukasi Mkami,” alisema. Mwigizaji huyo alisema akiwa Marekani alipigiwa simu na waandishi wengi wakimuuliza kuhusu ziara yake na aliwaeleza ukweli ulivyo, lakini anashangaa kibao kimemgeukia. “Sijakaa Marekani siku 14 kama inavyoelezwa, nimekaa kule siku 10 tu, nimeenda tarehe 13 (Septemba) na kurudi 24. Nilikutana na Nyalandu tarehe 13, Waziri alikuwa mgeni rasmi, tangu usiku huo wa hafla sikumwona tena na sijui kama aliendelea kuwapo Marekani au aliondoka.”

UHOLANZI YANYUKWA ULAYA

Picha
Kitimtim cha kutafuta tiketi ya kuelekea nchini Ufaransa kwaajili ya michuano ya soka barani Ulaya mwaka 2016 iliendelea tena usiku wa kuamkia leo huku nyasi za viwanja kadhaa zikiwa katika wakati mgumu. Katika kitimtim hicho timu ya Uholanzi iliwanyima raha mashabiki wake baada ya kukubali kupokea kipigo cha mabao 2-0, kutoka kwa Iceland. Nayo Wales ikautumia vema uwanja wake wa nyumbani baada ya kuigalagaza Cyprus kwa jumla ya mabao 2-1. Italy ilikuwa ugenini dhidi ya Malta huku mchezo huo ukimalizika kwa kila timu kucheza pungufu baada ya wachezaji wao kuoneshwa kadi nyekundu.

KOCHA ENGLAND AKOMSOA RODGERS

Picha
Kocha wa England Roy Hodgson amehoji kauli ya kocha wa Liverpool Brenden Rodgers ya kwamba wachezaji wanahitaji siku mbili baada ya mechi ili kuwawezesha kurejea katika hali zao za kawaida. Kauli ya kocha huyo wa Liverpool ilikuja baada ya mchezaji Raheem Sterling kulalamika kuchoka kabla ya mchezo wa ugenini wa England mchezo ambao timu hiyo iliibuka kidedea dhidi ya Estonia.

NYERERE DAY: TUMUENZI NYERERE KWA VITENDO

Picha
Ili kumuenzi Nyerere, TFF irejeshe kombe lake Na Fikiri Salum WATANZANIA wameadhimisha siku ya kumbukumbu ya kifo chake rais wa kwanza wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere ambaye alifariki Oktoba 14 mwaka 1999 katika hospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza. Ni miaka 15 tangia kifo chake ambapo kuna mengi ya kukumbuka enzi za utawala wake, kumbukumbu ya Nyerere ndiyo imenisukuma hadi kuandika makala hii, Watanzania wengi wamekuwa wakimzungumzia Mwalimu kutokana nay ale aliyofanya ambapo wengi wao wanasema bado Watanzania wameshindwa kumuenzi kwa vitendo.

BREKING NEWS: WAKILI DAMAS NDUMBARO ‘ ATUPWA JELA YA SOKA’ MIAKA SABA

Picha
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka nchi TFF, imemfungia wakili Damas Ndumbaro kujihusisha na mambo ya soka kwa muda wa miaka saba na faini ya kiasi cha pesa. Ndumbaro ambaye aliingia katika mzozo mkubwa na rais wa TFF, Ndugu, Jamal Malinzi wiki iliyopita baada ya TFF kuagiza kila klabu kukatwa asilimia tano za mapato yatokanayo na udhamini wa klabu hizo wanaoupata kutoka kwa Vodacom, wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara, na Azam Tv. Ndumbaro alikimbilia katika vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu zimemuagiza kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na havitakubali jambo hilo litokee, huku akijiamini na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya sheria, Ndumbaro alivuka mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani wa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa Shirikisho, Malinzi.

SIMBA YAPATA PIGO SOUTH AFRICA

Picha
Klabu ya Simba imepata pigo jingine kabla ya kukutana na wapinzani wao wa jadi Yanga baada ya kipa wao Hussein Sharrif ‘Casillas’ kuumia ugoko katika mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Orlando Pirates nchini Afrika Kusini walipoweka kambi. Hiyo ni habari mbaya kwa Simba ambayo kipa wake namba moja Ivo Mapunda hayupo fiti kwa asilimia 100 kutokana na majeraha ya kidole ambayo aliumia kwenye mazoezi ya klabu hiyo visiwani Zanzibar hivi karibuni.

TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI YA WATANZANIA

Picha
Vijana wa Taifa Stars wamemshusha pumzi kocha wa timu hiyo, Mart Nooij baada ya kuichapa Benin mabao 4-1 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jana. Mabao ya Stars yalifungwa na Nadir Haroub kwa kichwa dakika ya 16 akiunganisha vizuri mpira wa faulo uliopigwa na Erasto Nyoni na Amri Kiemba alifunga kiufundi bao la pili dakika ya 40 akitumia makosa ya beki wa Benin, Ore Fortune kabla ya Thomas Ulimwengu hajafunga la tatu katika dakika ya 49 akiunganisha krosi ya Mrisho Ngassa na bao la nne lilifungwa na Juma Liuzio dakika ya 71 akitumia vizuri pasi ya Ulimwengu. Benin ilipata bao lake pekee katika dakika ya 90 lililofungwa na Suanon Fadel kwa shuti akitumia vizuri pasi ya Stephane Sessegnon aliyewatoka mabeki wa Stars.

HISPANIA YAIBUKA KIDEDEA MATAIFA ULAYA

Picha
Harakati za kutafuta tiketi ya kufuzu kuelekea nchini Ufaransa mwaka 2016 kwenye michuano ya soka ya mataifa bara la Ulaya ziliendelea tena usiku wa kuamkia leo wakati timu kadhaa ziliposhuka dimbani.

MAKALA: SIMBA NA YANGA NI MABOMU YANAYOSUBIRI ZAMU YA KULIPUKA

Picha
Na Prince Hoza NINGEANZA kwa pongezi kwa timu ya taifa, Taifa Stars ambapo mwshoni mwa wiki ilifanikiwa kuilaza timu ngumu ya taifa ya Benin katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotambuliwa na shirikisho la soka duniani Fifa, mchezo huo ulifanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kabla ya kufanyika mchezo huo kulitanguliwa na mchezo wa kirafiki kati ya waumini wa dini mbili za Kiislamu na Kikristo, katika mchezo huo waumini hao walijigawanya katika timu mbili na moja iliitwa Amani na nyingine iliitwa Mshikamano, Aman ilishinda 1-0 goli likifungwa na Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

SANGOMA AIPA YANGA USHINDI DHIDI YA SIMBA.

Picha
Yanga imetabiriwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya hasimu wake Simba watakapokutana Oktoba 18 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.  Mnajimu na mtabiri maarufu nchini Dk Mtakoma ubishi ametoa utabiri wake kuhusu mchezo huo ambapo nyota zinaipa Yanga mabao mawili. 

SIMBA NA YANGA TIKETI ZA KIELEKTRONIKI LAZIMA- TFF

Picha
Serikali imelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuendelea kutumia tiketi za elektroniki licha ya klabu kongwe nchini Simba na Yanga kukataa kutumia tiketi hizo katika mechi yake ya kwanza ya watani wa jadi msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL). Mwishoni mwa mwezi uliopita viongozi wa Simba na Yanga walikubaliana kwa pamoja kukataa tiketi za elektroniki kutumika katika mechi yao ya mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Oktoba 18, mwaka huu wakidai mfumo huo una changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kuwafanya wachelewe kupata mapato yao.

COSTAL UNION FC KUMBURUZA ALIYEKUWA MFADHILI WAO "BINSLUM" MAHAKAMANI

Picha
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umesema utakwenda mahakamani kuishtaki Kampuni ya Binslum Tyre kutokana na kitendo cha kutengeneza tisheti za Coastal Union zenye nembo ya kampuni Sound na kuwapa bure mashabiki kuingiza nazo kwenye mechi mbalimbali za ligi kuu Tanzania bara wakiwa wamelipiwa na viingilo vya mchezo husika. Hali hiyo ni kinyume na utaratibu kutokana na kuwa tayari kampuni hiyo ilishajitoka kufadhili timu hiyo na tayari klabu ya Coastal Union ilikwishapata mfadhili mwengine ambayo ni kiwanda cha Kutengeneza Unga Ngano mkoani Tanga cha Pembe Flours Mills.

KIONGERA, IVO WATOSWA SIMBA.

Picha
Kiungo mshambuliaji Raphael Kiongera na kipa Ivo Mapunda wameachwa kwenye kikosi cha Simba kinachoondoka leo kwenda Afrika Kusini kuweka kambi ya muda kujiandaa na mechi yao dhidi ya watani, Yanga, Oktoba 18. Kiongera na Ivo watakaa nje ya uwanja kwa muda mrefu na Mkenya huyo aliyeumia goti ataruhusiwa kurudi uwanjani Desemba wakati Ivo aliumia kidole kidogo cha mkono. Beki na nahodha wa kipindi kilichopita, Nasoro Masoud ‘Chollo’ ambaye ameanza mazoezi ya gym jana huenda akawamo kwenye msafara huo, ingawa uwezekano wa kucheza mechi hiyo ni mdogo.

ZAMBIA YAMPATA KOCHA MPYA

Picha
Timu ya soka ya Zambia imemuajiri Nico Lobohm kama naibu kocha wa Honour Janza. Raia huyo wa Uholanzi amepewa kandarasi kuwa miongoni mwa kamati ya kiufundi hadi mwisho wa kampeni ya kuwania kufuzu katika kombe la mataifa bingwa barani afrika mnamo mwaka 2015. Rais wa Shrikisho la soka nchini Zambia Kalusha Bwalya amebaini kuwa Lobohom aliwahi kufanya kazi nchini humo.

KENYATTA ATINGA ICC

Picha
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amefika mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC huko Hague, ambako anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu.

LIVERPOOL YAANZA MAZUNGUMZO MAPYA NA STERLING

Picha
Raheem Sterling  Afisa Mkuu Mtendaji wa Liverpool, Ian Ayre, amefanya mazungumzo na waakilishi wa Raheem Sterling kuhusu mkataba mpya, meneja Brendan Rodgers amefichua. Rodgers alishikamana kuwa klabu hicho cha ligi ya Premier ya Uingereza kina ‘utulivu’ kuhusu mshambuliaji huyo chipukizi nyota licha ya taarifa anaweza kuondoka. Mchezaji huyo wa wingi wa Uingereza amehusishwa na miamba wa Uhispania, Real Madrid kufuatia ripoti kuwa hana makini ya kuongeza muda katika kandarasi yake na Liverpool inayodumu hadi 2017.

MAXIMO AIKATIA TAMAA YANGA KWA SIMBA

Picha
Kocha wa Yanga, Marcio Maximo amesema anaiheshimu Simba lakini ana matumani kikosi chake kitaibuka na ushindi katika mechi yao ya kwanza ya watani wa jadi msimu huu itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Oktoba 18, mwaka huu. Aidha, Mbrazil huyo amesema hana mpango wa kulipa kisasi cha kipigo cha mabao 5-0 ambacho Yanga ilikipata msimu wa 2011/12 dhidi ya Simba.

BLATTER ATAKIWA KUACHIA NGAZI FIFA

Picha
Mjumbe wa zamani wa shirikisho la soka duniani amesema kuwa heshima ya Fifa haitaweza kurudi mpaka pale Rais Wa shirikisho hilo Sepp Blatter atakapoachia ngazi. Michael Hershman ameiambia BBC kuwa Sepp blatter hanabudi kuondoka na kupisha mtu mwingine kukiongoza chombo hicho. Amedai kuwa hivi sasa yanatakiwa mabadiliko ya uongozi baada ya Fifa kuwa katika mlolongo wa shutuma za rushwa kwa miaka mingi,hivyo basi ni vyema uongozi ukabadilika.

KENYATTA NDANI YA ICC

Picha
Mahakama ya kimataifa ya ICC, inajianda kuwa mwenyeji wa mkutano maalum wa siku mbili kuhusu kya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye atakuwa rais wa kwanza aliye mamlakani kufika mbele ya mahakama hiyo.   Kenyatta anakabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu anazodaiwa kutenda baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

PATRICK PHIRI AINGIWA KIWEWE MECHI YA WATANI

Picha
Baada ya kulazimishwa sare ya tatu mfululizo kwenye Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) dhidi ya Stand United juzi, Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia Patrick Phiri amesema "kazi yetu ya ukocha ina majanga, unapokuwa kocha wa soka lazima ukubali kwamba unakaribisha majanga." Kikianza na washambuliaji wawili wa kimataifa, Mganda Emmanuel Okwi na Mrundi Amissi Tambwe, Kikosi cha Simba kilishikwa kwa sare ya bao moja na Timu ya Stand United kutoka Shinyanga, ikiwa ni sare ya tatu kwa timu hiyo ya Msimbazi katika mechi zake zote za mwanzo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

KUICHEKI TAIFA STARS v BENIN BUKU NNE TU!, ULIMWENGU, KAZIMOTO NDANI YA DAR

Picha
Na Boniface Wambura, Dar es salaam Kiingilio cha mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Benin (Squirrels) itakayochezwa Jumapili Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam ni sh. 4,000. Washabiki watakaolipa kiingilio hicho katika mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa ni kwa ajili ya viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu. Kwa washabiki watakaokaa jukwaa la VIP B kiingilio ni sh. 10,000. Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo ni za elektroniki ni Viti vya VIP A na C hakutakuwa na viingilio, na badala yake vitatumika kwa ajili ya wageni maalumu watakaolikwa kutoka katika madhehebu ya dini za Kikristo na Kiislamu.

WENGER AMKUBALI DIEGO COSTA, ASEMA NI MTU HATARI SANA

Picha
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa Diego Costa ni mshambuliaji hatari na kwamba mshambuliaji huyo wa Chelsea ni tishio kubwa kwa kikosi chake katika mechi ya Leo itakayochezwa katika uga wa stamford Bridge. Kilabu zote mbili hazijafungwa tangu msimu huu wa ligi uanze,lakini Chelsea iko juu ya Arsenal kwa pointi sita. Costa aliyenunuliwa kwa kitita cha pauni millioni 32 kutoka kilabu ya Uhispania ya Atletico Madrid,amefunga mabao 8 katika mechi 6 za ligi ya Uingereza alizoshiriki.

BADO NAIHESHIMU ARSENAL- FABREGAS

Picha
Cesc Fabregas Nahodha wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas, ambaye alingaria maadui wao Chelsea kwenye ngoma kali ya ligi ya Premier Jumapili, amesema bado anaheshimu waajiri wake wa zamani licha ya mashabiki wao kumkemea. Fabregas alimwandalia Digo Costa pasi ya juu juu iliyomwezesha kufunga goli la pili kunyamazisha Arsenal 2-0 katika uga wa Stamford Bridge na alitajwa kama mchezaji bora zaidi wa mechi hiyo baadaye. "Naheshimu Arsenal sana kwani walipatia fursa kubwa nikiwa chipukizi na bila wao, seingelikuwa hapa au kushinda mataji. “Najua wananipenda licha ya kejeli zao na ni kwasababu tulikuwa pamoja wakati mmoja. Lakini matukio wakati mwingine yanaongoza yale yalitendeka na ni hali ya mchezo,” kiungo huyo wa

KENYATTA AKUBALI KWENDA ICC

Picha
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema yuko radhi kwenda katika mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kikao maalum kuhusu kesi inayomkabili. Akiwahutubia wabunge mjini Nairobi,aliwaambia kuwa yuko tayarti kuhudhuria kikao maalum alichotakiwa kuhudhuria mjini Hague bila wasiwasi wowote. Kenyatta alitakiwa na majaji wa mahakama hiyo kufika ICC tarehe 8 mwezi huu kufafanua madai kuwa serikali yake imekataa kushirikiana na mahakama hiyo hasa upande wa mashitaka kwa kukataa kuipatia ushahidi unaohitajika katika kesi inayomkabili.