Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2018

Mama Kikwete amwambia Ali Kiba asipende kukagua simu ya mkewe

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mke wa Rais wa Awamu ya nne ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, mama Salma Kikwete amemtaka mwimbaji nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini Ally Saleh Kiba "Ali Kiba" kutopendelea tabia ya kukagua simu ya mkewe. Ally Kiba alifunga ndoa majuma mawili yaliyopita na mchumba wake Amina Khaleef, Mombasa, Kenya na sherehe yake inefanyika juzi katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam ambapo mama Kikwete alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika sherehe hiyo iliyoonyeshwa moja kwa moja na Azam Tv. Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mbunge maalum wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, alimtaka msanii Ally Kiba kulinda ndoa yake na kamwe asidiriki kukagua simu ya mkewe kwa kuangalia sms na simu zinazopigwa kwani zinaweza kuvunjika ndoa. Amedai ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu hiyo ya kutoaminiana, hivyo Kiba anapaswa kupuuzia sms ama simu anazopigiwa mkewe na anatakiwa kumuamini Ali Kiba ameambiwa na Mama Kikwete asipende ...

Mwadui yazidi kuichimbia kaburi Mbao Fc

Picha
Na Paskal Beatus. Shinyanga Timu ya Mwadui Fc ya mjini Shinyanga jioni ya leo imeweza kujinusuru katika janga la kutaka kushuka daraja baada ya kuilaza Mbao Fc ya Mwanza kwa bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Mwadui Complex. Ushindi huo unawafanya Mwadui kujiweka pazuri huku kipigo hicho kikizidi kuwachimbia kaburi vijana wa Mbao Fc ambao kwa sasa wako shakani. Goli pekee lililowapa ushindi Mwadui Fc lilifungwa na Charles Ilanfya kunako dakika ya 29 ambapo liliweza kudumu kwa dakika zote 90 za mchezo Mwadui Fc imeifunga Mbao Fc 1-0 leo

Yanga kupaa Alhamisi kuifuata USM Alger

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Baada ya jana kuchapwa bao 1-0 na mahasimu wao wa kandanda nchini Tanzania, Simba Sc, wawakilishi pekee kwenye michuano ya kimataifa nchini, Yanga Sc wanatarajia kusafiri Alhamisi ijayo kuelekea mjini Algiers nchini Algeria tayari kwa mchezo wa kwanza kundi D kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga Sc itaumana na USM Alger siku ya Jumapili mjini Algiers na safari yao itaanzia Alhamisi, mabingwa hao wa bara wamepoteza matumaini ya kutetea ubingwa wao hasa baada ya kuzidiwa pointi 14 na Simba wanaoongoza ligi wakiwa na pointi 62 huku wao wakiwa na pointi 48 wakishikilia nafasi ya tatu. Yanga ilifanikiwa kuingia hatua ya makundi kombe la Shirikisho baada ya kuitoa mashindanoni Welayta Dicha ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 2-1 ikishinda nyumbani 2-0 kabla ya kulala ugenini 1-0, hata hivyo Yanga imepangwa kundi moja na USM Alger ya Algeria, Rayon Sports ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya Yanga wanaondoka nchini Alhamisi kuifuata USM Alger

Hanspoppe aunganishwa na Aveva, Kaburu kesi ya utakatishaji

Picha
Na Asher Maliyaga. Dar es Salaam Mahakama mkazi ya Kisutu mjini Dar es Salaam imeliagiza jeshi la Polisi kumkamata haraka mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hanspoppe na kumuunganisha na viongozi wenzake katika kesi ya utakatishaji fedha inayowakabili na kughushi. Hakimu mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba amelitaka jeshi la polisi kumkamata mara moja Hanspoppe kwani ameonekana kuhusika moja kwa moja kwenye kesi hiyo inayowakabili Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake Geofrey Nyange "Kaburu" ambao wanasota mahabusu hadi sasa. Hanspoppe naye amehusishwa kwenye kesi hiyo ya utakatishaji fedha za klabu ya Simba zinazokadiliwa kufikia dola 300,000 za Kimarekani, kwa mujibu wa wakili wa Taasisi ya kupambana na rushwa nchini, (TAKUKURU) Leonard Swai amebadilisha hati ya mashitaka na kuliingiza jina la Hanspoppe pamoja na Franklin Lauwo ambapo wote hao watapelekwa na polisi na sasa wametakiwa kukamatwa Zacharia Hanspoppe anatakiwa kukamatw...

Kispoti: HAKUNA USHIRIKINA KWENYE SOKA

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam HATIMAYE ubishi wa mashabiki wa soka umemalizwa Jumapili ya Aprili 29, 2018 wakati Simba Sc ilipoizamisha Yanga Sc bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Goli pekee la Simba lilifungwa na Erasto Nyoni katika dakika ya 37 na ushindi huo moja kwa moja unawafanya wafikishe pointi 62 ikibakiza pointi 6 tu ili waweze kutwaa ubingwa wa bara kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne. Pia Jumapili ilikuwa siku nzuri kwa mashabiki wa Tanzania hasa baada ya timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kutwaa ubingwa wa kombe la Chalenji iliyofanyika nchini Burundi kwa kuilaza Somalia mabao 2-0, shukrani ziwaendee Edson Jeremiah na Jaffari Mtoo kwa mabao yao yaliyoipa kikombe Tanzania. Lakini mada yangu ya leo ni kuhusu Kamati ya Nidhamu na Maadili ya Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania, Tff kutoa maamuzi yake juu ya uendeshaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Kamati hiyo iliweza kutoa a...

SERENGETI BOYS YABEBA NDOO YA CHALENJI

Picha
Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, maarufu Serengeti Boys jioni ya leo imefanikiwa kunyakua ubingwa wa michuano ya Cecafa- Challenge Cup baada ya kuichapa Somalia mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Burundi. Ushindi huo wa leo ni dhahiri kwamba itawakilisha vema taifa katika fainali ya mataifa Afrika Afcon- U17 zitakazofanyika mwakani Tanzania ambapo Serengeti itakuwa mwenyeji. Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Edson Jeremiah na Jaffari Mtoo, Serengeti ilipenya hatua ya fainali baada ya kuilaza Kenya mabao 2-1 wakati Somalia iliiondosha Uganda kwa kuichapa bao 1-0 Serengeti Boys mabingwa Cecafa Challenge Cup

ERASTO NYONI APELEKA MAAFA JANGWANI

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Goli lililofungwa dakika ya 37 kipindi cha kwanza na mlinzi Erasto Nyoni limepeleka kilio mitaa ya Jangwani baada ya Simba Sc kuichapa Yanga Sc bao 1-0 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Huo ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara ambapo sasa Simba imefikisha pointi 62 na mechi 26 ikiiacha mbali Yanga yenye pointi 48 na mechi 24 ikishika nafasi ya tatu hasa baada ya Azam Fc jana kushinda 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar. Mpira wa leo Simba imeonekana kuutawala karibu vipindi vyote viwili,  huku Yanga ikishindwa kabisa kupeleka mashambulizi langoni kwa Simba na kumfanya kipa wake Aishi Manula kukaa likizo, mlinzi wa Yanga Hassan Kessy alitolewa nje kwa kadi nyekundu. Kituko kingine ni Yanga kushindwa kupata hata kona moja kitendo ambacho hakijawahi kutokea tangia watani hao wakutane Simba imeifunga Yanga 1-0 leo

TSHISHIMBI, AJIBU WAREJEA KUIANGAMIZA SIMBA LEO

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Kaimu kocha mkuu wa klabu bingwa ya soka Tanzania bara, Yanga Sc, Mzambia Noel Mwandila na msaidizi wake Shadrack Nsajigwa wakisaidiwa na kocha mpya raia wa DR Congo, Mwinyi Zahera wamewaanzisha Papy Kabamba Tshishimbi na Ibrahim Ajibu huku pia wakimrejesha Andrew Vincent Chikupe maarufu Dante kwenye eneo la ulinzi akisaidiana na Mhandisi Kevin Yondani kulinda ukuta wa Yanga. Yanga inashuka dimbani leo kusaka ushindi wake wa kwanza tangia alipoondoka kocha mkuu Mzambia George Lwandamina anayedaiwa kutimkia kwao Zambia kujiunga na timu yake ya zamani ya Zesco United. Kikosi kamili cha mabingwa hao kinatarajiwa kuwa hivi dhidi ya Simba Sc 1. Youthe Rostand 2. Hassani Kessy 3.  Gadiel Mbaga 4. Andrew Vicent 5. Kelvin Yondani 6. Saidi Juma 7. Yusufu Mhilu 8. Papy Tshishimbi 9. Obrey Chirwa 10. Rafael Daudi 11. Ibrahim Ajibu Benchi - Ramadhani Kabwili - Abdallah Shaibu - Juma Abdul - Juma Mahadhi - Maka Edward - Pius Buswita - Emanue...

KOTEI KUIMARISHA KIUNGO SIMBA, BOCCO, OKWI KUCHAPA LAPA

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Kocha mkuu wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba Sc, Mfaransa, Pierre Lechantre akisaidiwa na Masoud Djuma Irambona na Mohamed Hbibi wamempanga James Kotei kusimama kama kiungo wa kati yaani namba sita huku akiendelea kuwaanzisha Emmanuel Okwi, John Bocco na Shiza Kichuya kwenye safu ya ushambuliaji. Mchezo huo wa Ligi Kuu bara unatazamiwa kupigwa hii leo katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam huku kila timu ikihitaji ushindi ili kujiweka pazuri katika kutwaa ubingwa wa bara msimu huu wa 2017/18. Kikosi cha Simba kimepangwa hivi 1. Aishi Manula 2. Nicolaus Gyan 3. Asante Kwasi 4. Erasto Nyoni 5. Yusuph Mlipili 6. James Kotei 7. Jonas Mkude 8. Shomari Kapombe 9. John Bocco 10. Emmanuel Okwi 11. Shiza Kichuya Akiba 12. Said Mohamed 13. Poul Bukaba 14. Said Ndemla 15. Mohamed Tshabalala 16. Mzamiru Yassin 17. Laudit Mavugo 18. Rashid Juma Kotei (Kushoto) amepangwa katika kikosi cha kwanza leo

SIMBA NA YANGA LEO NANI ATALALA MAPEMA!

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Leo ndio leo asiyekuwa na mwana abebe jiwe ndivyo msemo wa kiswahili unavyoweza kutumika wakati watani wa jadi wa soka la Tanzania, Simba Sc na Yanga Sc watakapoumana jioni ya leo uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Katika kuelekea mchezo huo, Simba wanaonekana wako vizuri kuliko mahasimu wao Yanga ambao mashabiki wake wanaonekana wameikatia tamaa timu yao kutokana na matokeo wanayoyapata kwenye ligi, lakini kwa mujibu wa historia za timu hizo zinapokutana timu inayokuwa imeenea huwa inafungwa na ile inayoonekana dhaifu. Yanga inaingia uwanjani bila ya kocha wao mkuu, Mzambia George Lwandamina ambaye ameacha kazi na kurejea kwao Zambia na kuna taarifa amejiunga na timu yake ya zamani ya Zesco United, pia inaendelea kuwakosa nyota wake muhimu washambuliaji Donald Ngoma na Amissi Tambwe jambo ambalo linawanyima imani mashabiki wake huku sasa ikipanga kuwategemea Obrey Chirwa, Raphael Daudi, Yusuph Mhilu na Ibr...

Azam Fc yalipa kisasi kwa Mtibwa na kuishusha Yanga

Picha
Na Ikram Khamees. Morogoro Mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Azam Fc jioni ya leo imefanikiwa kulipa kisasi baada ya kuichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Manungu Complex mjini Morogoro. Bao pekee la Azam Fc limefungwa na mshambuliaji wake chipukizi Shabani Iddy Chilunda kunako dakika ya 43, ushindi huo unaifanya Azam Fc iliyocheza mechi 26 kufikisha pointi 49 na kuifanya ikamate nafasi ya pili na kuishusha Yanga Sc yenye pointi 47 na mechi 23. Matokeo mengine mjini Songea katika uwanja wa Majimaji, mabingwa wa zamani wa Tanzania, Majimaji Fc imewalaza Ruvu Shooting mabao 3-1 na kuzidi kujinusuru na janga la kushuka daraja, Stand United imelazimishwa sare tasa 0-0 na majirani zao Kagera Sugar katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Ligi hiyo itaendelea tena kesho lakini macho na masikio ni uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, watani wa jadi Simba na Yanga wataumana vikali Azam Fc imeichapa Mtibwa Sugar nyumbani kwao 1-0

Wanne kutua Yanga, yumo Salamba wa Lipuli

Picha
Na Asher Maliyaga. Dar es Salaam Wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa, Yanga Sc ambao pia ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, wamejipanga kujiimarisha kwa ajili ya hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika na msimu ujao. Taarifa ambazo hazina shaka kabisa zinasema mabingwa hao wamejipanga kunasa saini za wachezaji wanne ambao wataisaidia timu hiyo kwenye michuano hiyo pamoja na Ligi Kuu bara msimu ujao. Wachezaji ambao wanatajwa kujiunga na mabingwa hao ambao huenda msimu huu wakapokwa taji lao na mahasimu wao Simba Sc ni mshambuliaji wa Lipuli Fc ya Iringa, Adam Salamba ambaye hivi karibuni alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu Bara. Pia Yanga ina mpango wa kunasa saini ya mshambuliaji wa Welayta Dicha ya Ethiopia Arafat Djako na Mnigeria Quadri Kola Aladeokun na mzawa Habibu Kiyombo wa Mbao Fc, tayari Yanga imeshapata kocha mpya Zahera Mwinyi aliyechukua nafasi ya George Lwandamina raia wa Zambia Adam Salamba an...

Mtibwa Sugar na Azam Fc kumenyana leo Manungu Complex

Picha
Na Ikram Khamees. Morogoro Moja ya mechi kali na ngumu itapigwa jioni ya leo katika uwanja wa Manungu Complex, Turiani wilayaninMvomero mkoani Morogoro wakati wenyeji Wana tamtam Mtibwa Sugar watakapoikaribisha Azam Fc wana lambalamba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Mtibwa Sugar safari hii wanaonekana kuimarika zaidi hasa kutokana na matokeo mazuri wanayoyapata karibu katika mechi zake ilizocheza hivi karibuni ikiwemo kuingia fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup. Umahiri wa safu yake ya ushambuliaji ndiyo moja kati ya vitu vya kujivunia kwenye kikosi hicho kinachonolewa na mchezaji wake wa zamani, Zuberi Katwila, lakini Azam Fc nao wamekuwa wakifanya vibaya katika mechi zake za karibuni kiasi kwamba wanaelekea kuachana na kocha wake Mromania, Aristica Cioaba. Pia Azam Fc inakumbuka jinsi ilivyoondoshwa na Mtibwa Sugar katika michuano ya Azam Dports Federation Cup kwa mikwaju ya penalti 8-7 baada ya kumaliza dakika 90 bila kufungana, mechi nyingine z...

Makonda kuwa mgeni rasmi Simba na Yanga Jumapili

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Poul C Makonda anatazamiwa kuwa mgeni wa heshima kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Simba na Yanga utakaofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Mchezo huo utakaopigwa siku ya Jumapili kuanzia saa 10:00 na kurushwa na Azam Tv, Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa soka watakaojitokeza kushuhudia mchezo huo wenye kuvuta hisia za wengi. Makonda amewahi kuwa mgeni rasmi wakati klabu ya Simba ilipokuwa ikiadhimisha siku ya kuzaliwa kwake inayofahamika kama Simba Day mwaka jana katika uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, katika mchezo huo kiingilio cha chini kabisa jukwaa la mzunguko ni shilingi 7000 Mkuu wa mkoa Dar es Salaam, Poul Makonda (Kulia) atakuwa mgeni rasmi Simba na Yanga Jumapili

Njombe Mji yajinasua mkiani, Mbeya City nayo yabanwa

Picha
Na Mwandishi Wetu. Njombe Timu ya soka ya Njombe Mji ya mjini Njombe jioni ya leo imeutumia vema uwanja wa nyumbani baada ya kuilaza Ndanda Fc ya Mtwara mabao 2-0 uwanja wa Sabasaba mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Vijana wa Njombe Mji wakicheza mbele ya mashabiki wao wameweza kutakata kwa mabao hayo mawili yaliyowekwa kimiani na Notikeli Masasi na Ahmed Adwale na kuifanya timu hiyo kupanda kwa nafasi moja ikitoka nafasi ya 16 hadi ya 15 huku Majimaji Fc ya Songea sasa ikishikilia mkia, Njombe Mji iliyocheza mechi 25 imefikisha pointi 20. Nayo Singida United imenusurika kichapo toka kwa Mbeya City baada ya kulazimisha sare na wenyeji wao uwanja wa Sokoine mjini Mbeya jioni ya leo. Mbeya City walitangulia kupata bao lililofungwa na beki wake Haruna Shamte kabla ya Maliki Antiri kuisawazishia Singida United inayonolewa na Mholanzi, Hans Van der Pluijm Ligi hiyo inaendelea tena kesho kwa timu ya Majimaji ya Songea na Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar dhidi ya Azam Fc na Stand U...

MAKALA: Kichuya kuvunja rekodi ya Omari Hussein Keegan?

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Rekodi ya mfungaji wa magoli matatu (Hat trick) inashikiliwa na King Abdallah Kibaden Mputa wa Simba Sc ambaye alifunga mabao hayo mwaka 1977 wakati Simba ilipoibugiza Yanga mabao 6-0 uwanja wa  Taifa Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu bara. Lakini mshambuliaji wa Yanga Sc, Omari Hussein wengi walimpachika jina la utani Keegan wakimdananisha na mwanasoka wa kimataifa ulimwenguni, Kevin Keegan, Omari Hussein ni mchezaji wa Yanga yeye ameweka rekodi ya kuwa mfungaji wa muda wote wa mechi za watani Simba na Yanga. Keegan amefunga jumla ya magoli sita ambayo ni mengi na mchezaji pekee anayekaribia kumfikia ama kuweza kuivunja rekodi hiyo ni kiungo mshambuliaji wa Simba Sc, Shiza Kichuya ambaye yeye amefunga mabao manne mpaka sasa. Keegan alianza kufunga tangu Septemba 18, 1982 Yanga ilipoifunga Simba mabao 3-0, Keegan alifunga mabao mawili dakika ya 2 na 85 huku goli lingine likifungwa na Makumbi Juma dakika ya 62. Keegan alifunga tena Aprili 16, 1983 Y...

MBEYA CITY KUENDELEZA MOTO KWA SINGIDA UNITED LEO

Picha
Na Exipedito Mataluma. Mbeya Baada ya kuilazimisha sare bingwa mtetezi wa Ligi Kuu bara Yanga Sc ya bao 1-1, wakusanya kodi wa jiji la Mbeya, Mbeya City inatarajia kuikaribisha Singida United katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Sokoine. Ikumbukwe Singida United imeingia fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup na itacheza na Mtibwa Sugar Juni 2 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta mjini Arusha, hivyo mchezo wa jioni ya leo utakuwa mkali na wa kusisimua, lakini wagonga nyundo hao wa jiji la Mbeya wametamba kuibuka na ushindi. Ligi hiyo inaendelea tena leo kwa mchezo kati ya Ndanda Fc na wenyeji wao Njombe Mji katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, hiyo itakuwa mechi muhimu kwa timu hizo kwani kila moja inapigania kusalia Ligi Kuu, kesho Jumamosi ligi hiyo itaendelea tena pale Turiani katika uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro, wenyeji Mtibwa Sugar watawakaribisha Azam Fc "Wanalambalamba" wa Chamazi Dar es Salaam. Majimaji...

KUELEKEA SIMBA NA YANGA JUMAPILI, REKODI YA KIBADEN YAWAUMIZA VICHWA OKWI, BOCCO NA CHIRWA

Picha
Na Paskal Beatus. Dar es Salaam Mwaka 1977 Simba Sc almaarufu Wekundu wa Msimbazi au wana Lunyasi waliinyanyasa Yanga Sc kwa kuichapa mabao 6-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Taifa (Sasa Uhuru Stadium). Mshambuliaji wa Simba wakati huo Abdallah Seif Athuman Kibaden aliifungia Simba mabao matatu katika mchezo huo huku mengine mawili yakifungwa na Jumanne Khamis Masimenti na goli lingine Yanga walijifunga. Basi mpaka sasa imepita takribani miaka 39 hakuna mchezaji yeyote si wa Simba wala Yanga aliyeweza kumfikia Kibaden kwa kufunga mabao matatu kwenye mchezo mmoja wa watani. Lakini Jumapili ijayo watani hao wa jadi wa soka la Tanzania wanaumana katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba wao wana washambuliaji watatu ambao wanaweza kufanya lolote katika mchezo huo kwa kuvunja rekodi ya Kibaden. Simba wanaye Emmanuel Anord Okwi, John Raphael Bocco na Shiza Kichuya ambao wanaweza kumfikia Kibaden ingawa wafanye kazi kw...

KUTINYU WA SINGIDA UNITED AFUNGIWA KISA USHIRIKINA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Vitendo vya kuendekeza ushirikina vimeshamiri kwenye soka la Tanzania na safari hii limemsomba Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu anayekipiga timu ya Singida United. Mshambuliaji huyo aliyeibuka shujaa kwa kuifungia mabao mawili muhimu dhidi ya JKT Tanzania mchezo wa nusu fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup uwanja wa Namfua mjini Singida. Mchezaji huyo amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya shilingi 500,000 baada ya kutupa glovu za kipa wa Mtibwa Sugar kwa mashabiki wa Singida United na kukimbia nayo. Kitendo hicho kimesababisha kamati ya nidhamu ya TFF kumuadhibu nyota huyo ambaye amekuwa katika kiwango kikubwa, vitendo vya ushirikina vimeziponza pia timu za Mbao Fc na Simba ambazo zote zimepigwa faini ya shilingi laki tano Tafadzwa Kutinyu amesimamishwa mechi tatu na kupigwa faini ya Laki tano kisa ushirikina

MZUKA YANGA UMEPANDA BAADA YA KUREJEA NGOMA

Picha
Na Saida Salum. Morogoro Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc huenda wakawa na furaha baada ya kikosi chake kuimarika upya kufuatia nyota wake waliokuwa wakiunda kikosi cha kwanza na kuipa ubingwa wa bara mara tatu mfululixo kurejea uwanjani. Yanga imeweka kambi mjini Morogoro na Jumapili itaumana na mahasimu wake Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara utakaopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mabingwa hao watetezi wapo kambini Morogoro sawa na mahasimu wao lakini upepo unaweza kuwaendea poa baada ya mastraika wake hatari Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma kuanza mazoezi na kwa mujibu wa daktari wa timu Edward Bavu, nyota hao wanaweza kucheza mechi hiyo. Ngoma na Tambwe wamekuwa wakiitesa sana Simba na kama watapangwa huenda mchezo huo ukawa mkali na wa kusisimua, pia katika mazoezi yanayoendelea ya klabu hiyo, Ibrahim Ajib ambaye naye alikuwa majeruhi ameanza mazoezi na kuongeza mzuka wa mechi hiyo Donald Ngoma amerejea uwanjani

KIPA WA KIMONDO FC AVUNJIKA MGUU AJALINI

Picha
Na Ayubu Mhina. Chalinze Mlinda mlango wa zamani wa Kimondo Fc ya Mbeua na Polisi Moro, Azishi Simon amevunjika binaya mguu wake wa kuloa baada ya kupata ajali mbaya ya bodaboda maeneo ya Mdaula, Chalinze mkoani Pwani Junamosi iliyopita. Kwa mujibu wa mashuhuda ajali hiyo ilitokea wakati kipa huyo akiendesha pikipiki ndogo aliyopewa na mjomba wake ili airejeshe nyumbani kwao, mmoja kati ya mashuhuda hao amedai Azishi alikuwa amelewa na aliendesha pikipiki kwa mwendo kasi. Kipa huyo wa zamani wa timu ya mkoa wa Pwani iliyoshiriki michuano ya Taifa Cup alivunjika vibaya mguu wake baada ya kugongana uso kwa uso na roli lililokuwa likienda kwa mwendo kasi, ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Mdaula, barabara ya Kidugalo na inasemekana chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi na ulevi, kipa huyo amelazwa katika hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani Azishi Simon (Pichani) amevunjika mguu

SIMBA YAWEKA WAZI USHINDI KWAO NI LAZIMA J,PILI

Picha
Na Ikram Khamees. Morogoro Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba Sc wameahidi kuibuka na ushindi katika mchezo wao dhidi ya mahasimu wao Yanga Sc utakaochezwa Jumapili uwanja wa Taifa  jijini Dar es Salaam. Watani hao wa jadi wa soka la Tanzania watakutana katika mchezo wa Ligi Kuu bara huku Simba ikiwa kileleni ikifuatiwa na Yanga Sc hivyo kila moja inahitaji ushindi, Timu zote mbili zimejichimbia mjini Morogoro. Mkuu wa kitengo cha habaro na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema ushindi kwa klabu yake ni lazima na wala hakuhitaji nguvu kuupata, amedai kikosi chao kimeimarika idara zote hivyo wanazifuata pointi zao Taifa. Manara ameongeza kuwa msimu huu wanautaka ubingwa wa bara kwa hali yoyote ile na ili ubingwa unoge lazima umfunge Yanga Simba inaumana na Yanga Jumapili na wamesema watashinda tu hata kwa lazima

Kamera kufungwa kila kona uwanja wa Taifa, Simba na Yanga

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Katika kuhimarisha Usalama Ndani ya Uwanja wa Taifa katika Pambano la Watani wa Jadi Kati ya Simba SC Dhidi ya Yanga SC hapo Aprili 29,Shirikisho la Soka Nchini (TFF) limetangaza Kufungwa kwa Kamera 109 Uwanjani. Afisa habari wa Shirikisho hilo Clifford Ndimbo Amesema kuwa watu wa Usalama Wamejipanga kuhakikisha Wanazuia Vurugu zitakazojitokeza Uwanjani Hapo Siku ya Mchezo huo. Huku kwa Upande wa Jeshi la Polisi Wamesema kuwa Wamejipanga kuhakikisha Amani Inakuweoo Kuanzia Mwanzo wa Mchezo Mpaka Mwisho. Uwanja Utakuwa wazi Kuanzia Saa 2.00 Asubuhi. Yanga na Simba kuumana Jumapili

KISPOTI

Picha
SIMBA KUMTOA MO IBRAHIM KWA MKOPO NI JAMBO LA BUSARA SANA Na Prince Hoza SIMBA SC na Yanga Sc zinaumana Jumapili ijayo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, hiyo ni mechi kubwa hapa nchini ambapo wapenda soka watajitokeza kushuhudia mtanange huo. Lakini jina la Mo Ibrahim halimo katika kurasa za magazeti ya michezo hasa ya hapa nchini, Mo Ibrahim ni mchezaji wa Simba Sc ambao kwa sasa wanaongoza ligi, Simba wapo kileleni kwa pointi zao 59 wakiiacha nyuma ya pointi 11 mtani wake Yanga Sc. Kikosi cha kwanza cha Simba hata mtoto mdogo ukimpa akupangie atakutajia kuanzia mlinda mlango hadi winga wa kucheza namba 11, na pia atakutajia wachezaji wanaokaa benchi, kwa vyovyote Mohamed Ibrahim "Mo" atakuwa jukwaani akiufuatilia mpira huo. Siku nyingi sana sijamuona Mo Ibrahim akiwa ameuvalia ule uzi wa rangi nyekundu na micharazo meupe mabegani, Mo sijamuona hata benchi akisubiri kuchukua nafasi aingie, tayari mashabiki wameshamsahau. Ilikuwa ngumu mashabiki wa Simba kums...

TAMBWE FITI KUIVAA SIMBA JUMAPILI

Picha
Na Saida Salum. Morogoro Mshambuliaji wa kimataifa wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Yanga Sc, Amissi Joceylin Tambwe raia wa Burundi huenda akacheza dhidi ya Simba. Watani wa jadi Simba na Yanga zinaumana Jumapili ijayo uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara na mtaalamu huyo wa vichwa ataungana na kikosi cha Wanajangwani kuhakikisha pointi tatu zinaenda Yanga. Yanga imeweka kambi mjini Morogoro kujiandaa na mchezo huo na kwa mujibu wa daktari wa Yanga, Edward Bavu amesema Tambwe yuko fiti na anaweza kucheza bila wasiwasi huku kocha wa muda wa mabingwa hao Mzambia Noel Mwandila tayari ameanza kumshuhudia mazoezini na anakiri jamaa yuko fiti Amissi Tambwe ameanza mazoezi Morogoro

KOCHA WA DRC CONGO AJA KUMRITHI LWANDAMINA YANGA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Kocha wa kimataifa aliyepata kuzifundisha timu mbalimbali barani Afrika na Ulaya, Mwinyi Zahera raia wa DRC Congo amewasili Dar es Salaam kujiunga na mabingwa wa soka nchini Yanga Sc na muda wowote kuanzia sasa atasafiri kuelekea Morogoro kuungana na kikosi hicho ambapo kimepiga kambi huko. Taarifa zenye uhakika kutoka klabu ya Yanga zinasema Zahera kocha mzoefu kabisa la Afrika akiifundisha timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidwmokrasia ya Congo (Leopards) amekuja nchini kwa ajili ya kumrithi Mzambia George Lwandamina ambaye aliondoka klabuni hapo majuma mawili yaliyopita na kurejea nyumbani kwao Zambia ambapo inadaiwa amejiunga na timu yake ya zamani ya Zesco United. Tayari Yanga iko kambini Morogoro ikitokea jijini Mbeya ambapo juzi Jumapili ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji wao Mbeya City uwanja wa Sokoine, na Jumapili ijayo inacheza na mtani wake Simba Sc hivyo kwa vyovyote pambano litakuwa gumu kwani timu zote mbili zinapigania ubin...

Singida United yatinga fainali FA Cup

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Timu ya soka ya Singida United jana ilifanikiwa kuingia fainali baada ya kuilaza JKT Tanzania mabao 2-1 katika mchezo mkali wa nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup uwanja wa Namfua mkoani Singida. Mchezo huo ulilazimika kuchezwa dakika 120 hasa baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa zimefungana bao 1-1, JKT Tanzania ilitangulia kupata bao la uongozi dakika ya 38 likifungwa na Hassan Matalema kabla ya Singida United hawajakomboa bao kupitia kwa Tafadzwa Kutinyu dakika ya 54. Pambano hilo lilielekea katika muda wa nyongeza wa dakika 30 ambapo yule yule Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu aliiandikia timu yake bao la pili na la ushindi, kwa matokeo hayo Singida United imeingia fainali ambapo itaumana na Mtibwa Sugar Juni 2 mwaka huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta mjini Arusha Singida United imeingia fainali ya FA Cup

Yanga na Mbeya City ngoma inogile leo

Na Exipedito Mataruma. Mbeya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga Sc jioni ya leo wanaanza kucheza viporo vyao ambapo itaumana na Mbeya City uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Yanga iliyo katika nafasi ya pili na pointi zake 47 kwa vyovyote itataka kushinda mchezo huo ili kufikisha pointi 50 na kupunguza gepu lake la pointi na mahasimu wao Simba Sc wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 59. Lakini Simba jana imepunguzwa kasi na Lipuli Fc ya Iringa baada ya kuambulia sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Samora mjini Iringa na kujikuta ikifikisha pointi 59 na mechi 25 wakati Yanga wao wamecheza mechi 22 tu hivyo wanaweza kuikaribia zaidi Simba iwapo watapata ushindi mechi zao tatu zilizosalia. Yanga pia inachagizwa na ushindi wake ilioupata kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika hasa baada ya kufuzu hatua ya makundi hivyo itakuwa ikisaka upya tiketi ya kushiriki tena michuano ya kimataifa mwakani

YANGA YAANGUKIA MIKONONI MWA WAARABU CAF

Picha
Na Asher Maliyaga. Dar es Salaam Yanga Sc ya Tanzania imepangwa pamoja na timu za Rayon Sports ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya na USM Alger ya Algeria katika kundi D kombe la Shirikisho barani Afrika na itaanza kushuka uwanjani Mei 6 mwaka huu. Kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa jana saa nane mchana makao makuu wa Shirikisho la mpira wa miguu mjini Cairo, Misri, makundi manne yamepangwa ambapo Yanga Sc itaanza na waarabu hao wa Algeria. Kundi A lina timu za Asec Mimosas ya Ivory Coast, Raja Casablanca ya Morocco, AS Vita ya DR Congo na Aduana Stars ya Ghana, wakati kundi B lina timu za RS Berkane ya Morocco, El Masry ya Misri, UD Songo ya Msumbiji na El Hilal ya Sudan. Kundi C lina timu za Enyimba ya Nigeria, Williamsville ya Ivory Coast, CARA ya Kongo Brazaville na Djoliba ya Mali, wakati kundi D linajumuhisha mabingwa wa Tanzania bara Yanga Sc, USM Alger ya Algeria, Rayon Sports ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya

Simba yanusurika kichapo kwa Lipuli

Picha
Na Ikram Khamees. Iringa Vinara wa Ligi Kuu bara, Simba Sc leo imenusurika kipigo kutoka kwa wenyeji Lipuli Fc ya Iringa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Samora mjini Iringa. Timu hizo hadi zinaenda mapumziko tayari Lipuli walikuwa mbele kwa bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji wake Adam Salamba ambaye pia ndiye mchezaji bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu bara. Laudit Mavugo raia wa Burundi ndiye aliyeinusuru Simba isifungwe katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua. Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 59 na mechi 25, watani zao Yanga leo wanacheza na Mbeya City uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na kama watashinda basi watapunguza gepu la pointi 12

Busungu, Mwaisabula waiongezea mzuka Lipuli kuia Simba

Picha
Na Ikram Khamees. Iringa Kuwepo kwa kocha mzoefu na mchambuzi mahiri wa soka nchini, Kenny Mwaisabula "Mzazi" kwenye kikosi cha Lipuli Fc ya Iringa na uwepo wa mshambuliaji Malimi Busungu kunaiongezea mzuka Lipuli kuilaza Simba leo. Wawili hao wapo Iringa na kikosi cha Lipuli huku kila mmoja akiwa na jukumu lake, Mwaisabula yeye amewahi kuzinoa Bandari ya Mtwara, Cargo ya Dar es Salaam, Yanga Sc na JKT Tanzania zamani JKT Ruvu na anawajua vilivyo wachezaji wa Kitanzania. Wakati Busungu yeye amekuwa na rekodi nzuri ya kuitungua Simba kila timu anayojiunga nayo, amewahi kuiliza Simba alipokuwa Polisi Moro (Sasa Polisi Tanzania) pia amefanya hivyo akiwa na JKT Mgambo, Yanga Sc na sasa yupo Lipuli na leo wanakutana na Simba ngoja tuone kama atawalaza mapema Wekundu hao wa Msimbazi wanaokamata usukani wa ligi hiyo wakiwa na pointi 58 zikiwa ni nyingi mno kuliko anayefuatia Yanga mwenye pointi 47

Straika Welayta Dicha kumrithi Ngoma Yanga

Picha
Na Albert Babu. Dar es Salaam Mabingwa wa soka Tanzania bara na wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa, Yanga Sc wamemnasa straika hatari wa timu ya Welayta Dicha ya Ethiopia, Arrafat Djako raia wa Togo na kuna uwezekano mkubwa akasajiliwa. Yanga inaruhusiwa kufanya usajili mdogo hivi sasa kwa ajili ya kushiriki hatua ya makundi na Djako anatajwa kutua Jangwani kutokana na kuridhishwa na kiwango chake. Djako ni mshambuliaji lakini ana uwezo wa kucheza kiungo wa pembeni na ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, Yanga ilifungwa bao 1-0 na Welayta Dicha Jumatano iliyopita na goli pekee lilifungwa na nyota huyo. Kuna taarifa huenda Yanga ikaachana na Mzimbabwe Donald Ngoma ili nafasi yake kuchukuliwa na Mtogo huyo kwakuwa tayari Yanga imeshamaliza nafasi za wachezaji saba wa kigeni. Wachezaji ambao wa kigeni Yanga inao ni Youthe Rostand (Cameroon), Obrey Chirwa (Zambia), Thabani Kamusoko, Donald Ngoma (Zimbabwe), Fiston Kayembe, Papy Kabamba Tshishimbi (DR Congo) na Amissi Tambwe...

SIMBA KUSAKA USHINDI MWINGINE KWA LIPULI LEO

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu Bara Simba Sc jioni ya leo wanakuwa wageni wa Lipuli Fc katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Samora mjini Iringa. Kwa hakika Simba leo inahitaji ushindi mwingine muhimu ili kujiwekea matumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu baada ya kuhangaika kipindi cha miaka mitano bila mafanikio. Lipuli inayonolewa na kiungo wa zamani wa Wekundu hao wa Msimbazi, Seleman Matola ambaye inaonekana pia ameongezewa nguvu na kocha wa zamani wa Yanga, Kenny Mwaisabula "Mzazi" kwa vyovyote wanataka kuizuia Simba yenye safu kali ya ushambuliaji inayoongozwa na Emmanuel Okwi, John Bocco na Shiza Kichuya

AGNES MASOGANGE AFARIKI DUNIA

Picha
Na Asher Maliyaga. Dar es Salaam Video queen mwenye jina kubwa nchini, Agnes Gerald "Masogange" amefariki dunia leo baada ya kuugua kwa muda mfupi. Taarifa za kifo chake zimesambaa jioni hii ambapo inasemekana staa huyo amefariki katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge ambapo alikuwa akifanyiwa matibabu kufuatia kupatwa na presha ghafla. Masogange aliyejipatia umaarufu kwa uigizaji kwenye video za wasanii wa bongofleva akitamba na msanii Belle Nine na wimbo uliojulikana sana wa Masogange, pia msanii huyo alikuwa akiandamwa na kashfa ya utumiaji dawa za kulevya na aliwahi kukamatwa nchini China, tayari mwili wake umeshapelekwa hospitali ya Muhimbili. Mungu aiweke roho yake mahara pema peponi, Amina Agnes Masogange amefariki dunia leo

MTIBWA SUGAR HAWAKAMATIKI, WAILIPUA STAND UNITED NA KUTINGA FAINALI

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Timu ya Mtibwa Sugar ya Turiani, Manungu mkoani Morogoro jioni ya leo imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup baada ya kuilaza Stand United mabao 2-0 mchezo wa nusu fainali  wa CCM Kambarage mjini Shinyanga. Mchezo ulikuwa mkali kwa timu zote kushambuliana lakini Mtibwa Sugar inayonolewa na Zuberi Katwila ilionekana kuutawala mchezo huo kipindi cha kwanza na kufanikiwa kufunga mabao yote mawili kupitia kwa kiungo mshambuliaji wake Hassan Dilunga kwenye dakika za 30 na 38. Kipindi cha pili Stand United waliweza kulinda lango lao na kufanya mashambulizi mengi kwa Mtibwa lakini hawakuweza kupenya ukuta, Mtibwa sasa imetinga fainali ikisubiri mshindi kati ya Singida United na JKT Tanzania utakaopigwa Jumapili, bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika Mtibwa Sugar imeingia fainali ya FA Cup ikiifunga Stand United 2-0 leo

NINJA AIPIGIA HESABU KALI SIMBA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Beki wa kati mwenye uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza cha mabingwa wa soka nchini, Yanga Sc, Abdallah Seif Shaibu "Ninja" , ameipigia mahesabu makali Simba na kusema wamekwisha. Mlinzi huyo aliyecheza vizuri kwenye mechi tatu mfululizo alizobahatika kupangwa, mbili za michuano ya kimataifa dhidi ya Wolaika Dicha ya Ethiopia na moja ya Ligi Kuu bara dhidi ya Singida United amedai mechi dhidi ya Simba ndio njia yake ya kumtoa kimaisha. Ninja aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea Taifa Jang' ombe ya Unguja, Zanzibar, hakuwa na mwanzo mzuri kwenye kikosi hicho kutokana na kushindwa kwake kuonyesha kile wanachotaka Wanayanga. Lakini kwa sasa beki huyo ametokea kuwakosha mashabiki wa Yanga na sasa amekuwa kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa, Simba na Yanga zitaumana Aprili 29 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na beki huyo ameipigia mahesabu mechi hiyo, Jumapili ijayo Yanga itacheza na Mbeya City uwanja wa S...

Stand United na Mtibwa Sugar ni nusu fainali ya kisasi

Picha
Na Mwandishi Wetu. Shinyanga Leo inapigwa nusu fainali ya kwanza ya kombe la Azam Sports Federation Cup kati ya Stand United na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Stand United inaingia katika mchezo huo ikiwa nyumbani mbele ya mashabiki wake hivyo kila sababu ya kuweza kuchomoza na ushindi, lakini vijana wa Mtibwa Sugar ambao msimu huu wanaonekana kuimarika haswa, hawatataka kupoteza mchezo huo. Hivyo wanahitaji kushinda ili kuongia fainali ikisubiri mshindi mwingine kati ya Singida United na JKT Tanzania keshokutwa, Srand United leo itawategemea mshambuliaji wake Vitalis Mayanga na Mtibwa Sugar ina winga wake hatari Salum Kihimbwa Stand United na Mtibwa Sugar zinaumana leo

TFF yaimwagia misifa Yanga kwa kutinga makundi CAF

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Shirikisho la mpira wa miguu nchini, TFF limeimwagia salamu za pongezi klabu ya Yanga kwa kufanikiwa kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika. Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia ameisifu Yanga kwa kufanikiwa kuingia hatua hiyo ambapo amedai ni heshima kubwa kwa nchi. Karia amedai kitendo ilichofanya Yanga ni cha kuigwa na vilabu vyote nchini vitakavyopata nafasi ya kushiriki, "Yanga imetuletea heshima kubwa kwa kuingia makundi, naamini nchi yetu itaheshimiwa", alisema Karia ambaye amesisitiza Shirikisho lake litaendelea kushirikiana na Yanga. Yanga jana ilitinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika kwa kuiondoa Welayta Dicha ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 2-1 na itawasili nchini leo usiku wa saa 7:00 Yanga imepomgezwa na TFF

Hatimaye Ally Kiba afunga ndoa na mchumba wake Mombasa

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Staa wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ally Kiba asubuhi ya leo amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi Amina Khaleef katika msikiti uliojengwa na swahiba wake Hassan Joho ambaye ni Gavana huko Mombasa. Taarifa ambazo zimeifikia Mambo Uwanjani, zinasema kuwa staa huyo aliwasili pamoja na familia yake tangu Jumanne iliyopita tayari kwa kushiriki shughuri hiyo kubwa leo. Sherehe ya harusi hiyo itarushwa Live na kituo cha Azam Tv hii leo kutoka moja kwa moja kwenye ukumbi mkubwa wa kisasa wa Diamond Jubilee uliopo mjini Mombasa ambapo watu mashuhuri wanatarajia kuhudhuria akiwemo Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali nchini Kenya. Pia mwanamuziki staa Ommy Dimpoz naye ni miongoni mwa watu maarufu watakaoudhuria harusi hiyo, Ally Kiba anakuwa msanii wa kwanza nchini kufunga ndoa na kuonyeshwa live na runinga ambapo dunia itashuhudia tukio hilo Ally Kiba na mkewe Amina Khaleef wamefunga ndoa ...

Simba wazifuata pointi tatu Iringa

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba Sc wameondoka leo kuelekea mjini Iringa tayari kabisa kwa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya wenyeji wao Lipuli Fc katika uwanja wa kumbukumbu ya Samora Machel, Jumamosi ijayo. Mchezo huo ulikuwa uchezwe Ijumaa ya kesho lakini kwa mujibu wa Bodi ya Ligi mchezo umesogezwa hadi keshokutwa kwa madai uwanja huo wa Samora utakuwa na matumizi mengine ya kijamii. Kikosi cha Simba ambacho kimepania kutwaa ubingwa wa bara msimu huu kimeondoka leo mapema kuifuata Lipuli, Simba iko kileleni na pointi zake 58 zikiwa ni tofauti ya pointi 11 na hasimu wake Yanga Sc ambao wanashikilia nafasi ya pili Simba imeondoka leo kwenda Iringa

Zilizofuzu makundi kombe la Shirikisho Afrika hizi hapa

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara Yanga Sc jana iliungana na timu nyingine 15 kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika na kufanya jumla ya timu 16 zitashiriki hatua hiyo. Jumamosi majira ya saa 8;00 mchana mjini Cairo, Misri droo itachezeshwa na kutoa makundi manne ambapo kila timu itajijua kama itapangwa kucheza na timu gani, ukanda wa Afrika kaskazini ndio vinara kwa kuingia timu nyingi ikifuatiwa na Afrika magharibi, Afrika mashariki na mwisho Afrika kusini. Timu zilizotinga hatua hiyo kutoka Kaskazini mwa Afrika ni USM Alger ya Algeria, Al Masry ya Misri, RS Berkane na Raja Casablanca za Morocco, za Afrika ya kati ni AS Vita ya DR Congo, CARA ya Congo Brazaville na El Hilal ya Sudan. Zinazotokea Afrika mashariki ni Gor Mahia ya Kenya, Rayon Sports ya Rwanda na Yanga Sc ya Tanzania, za kusini mwa Afrika ipo UD Songo ya Msumbiji, zinazotoka Afrika masharibi ni Enyimba ya Nigeria, Aduana Stars ya Ghana, Williamsville ya Ivory Coast n...

Kuziona Yanga na Simba ni buku saba

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Shirikisho la soka Nchini Tanzania (TFF) limetaja Viingilio vya mchezo wa tarehe 29 mwezi wa nne, kati ya Vigogo wa soka Nchini Tanzania Simba Sc na Yanga Sc. TFF imetaja viingilio hivyo kuwa VIP A itakua Tsh 30,000/= VIP B&C  itakua Tsh 25,000/= Huku mzunguko ikiwa ni Tsh 7,000/= Tu. Tiketi hizo zinapatikana kwa njia ya Selcom. Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga na Simba zitaumana Aprili 29 mwaka huu

YANGA YATINGA MAKUNDI SHIRIKISHO, KULAMBA BILIONI MOJA SAAFI

Picha
Na Paskal Beatus. Hawassa Klabu bingwa ya soka Tanzania bara na wawakilishi pekee waliosalia katika mashindano ya kimataifa, Yanga Sc jioni ya leo imefuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kufungwa bao 1-0 na wenyeji wao Welayta Dicha ya Ethiopia. Mchezo huo wa marudiano uliofanyika katika uwanja wa kimataifa wa Hawassa uliopo mjini Hawassa wenyeji walifanikiwa kujipatia bao lao la kuongoza lililofungwa na mshambulizi wake raia wa Togo, Arafat Djako kunako dakika ya pili kipindi cha kwanza. Baada ya kupata bao hilo Welayta Dicha waliendelea kulisakama lango la Yanga kama nyuki lakini kipa wa mabingwa hao wa soka nchini Mcameroon, Youthe Rostand alikuwa imara kuokoa hatari zote na timu hizo kwenda mapumziko matokeo yakiwa hayo. Kipindi cha pili Yanga waliendelea kulilinda lango lao na shukrani ziwaendee mabeki wa kati Kevin Yondan na Abdallah Shaibu "Ninja" ambao walifanya kazi yao vizuri na kumaliza Yanga ikisonga mbele kwa jumla ya ushindi wa ma...

CHIRWA, BUSWITA WAANZA PAMOJA KUIANGIZA DICHA, NINJA, YONDAN KUJENGA UKUTA WA BERLIN

Picha
Na Paskal Beatus. Hawassa Kaimu kocha mkuu wa mabingwa wa soka nchini, Yanga Sc, Mzambia Noel Mwandila leo amewaanzisha pamoja washambuliaji Obrey Chirwa, Raphael Daudi na Pius Buswita, na bila shaka hao ndio watakaoleta kashikashi langoni kwa Wolayta Dicha mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho barani Afrika. Mwandila pia amemtupa benchi mlinzi wa kushoto Gardiel Michael na kumuanzisha Mzanzibar, Haji Mwinyi Mngwali ambao wataongoza katikati na Mhandisi Kevin Yondan na Abdallah Shaibu "Ninja". KIKOSI CHA LEO CHA YANGA SC DHIDI YA WOLAYTA DICHA 1. Youthe Rostand 2. Hassani Kessy 3. Mwinyi Haji 4. Abdallah Shaibu 5. Kelvin Yondani 6. Papy Tshishimbi 7. Yusufu Mhilu 8. Thabani Kamusoko 9. Obrey Chirwa 10. Rafael Daud 11. Pius Buswita Benchi - Beno Kakolanya - Juma Abdul - Gadiel Michael - Nadir Haroub - Saidi Juma - Juma Mahadhi - Emanuel Martin Yanga iko kamili kwa mchezo huo leo

STAND UNITED YATISHIA KUJITOA AZAM FEDERATION CUP

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Uongozi wa timu ya Stand United "Chama la wana" ya mkoani Shinyanga, umetishia kujiondoa katika mivhuano ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup ikidai haijalipwa fedha zao za ushiriki tangia raundi ya kwanza hadi sasa nusu fainali. Akizungumza leo, katibu mkuu wa klabu hiyo, Kennedy Mwangi amesema Shirikisho la mpira wa miguu nchini, TFF, halijawapa fedha zao tangu walipoanza kushiriki mivhuano hiyo na huenda wakashindwa kuingiza timu Aprili 23 mwaka huu watakapoumana na Mtibwa Sugar. Mwangi amedai Stand United itawakaribisha Mtibwa Sugar uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga hatua ya nusu fainali lakini anashangaa fedha zao kuliwa na watu wa TFF, hata hivyo kuna taarifa inasema kuwa Stand United inadaiwa fedha na wachezaji wake ambao walishitaki TFF na sasa klabu hiyo inakatwa ili kufidia madeni hayo Stand United imetishia kujitoa Azam Sports Federation Cup

YANGA NA DICHA NI VITA YA KUINGIA MAKUNDI AFRIKA

Picha
Na Paskal Beatus. Hawassa Hatimaye ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa imefikia ambapo mchezo wa marudiano kati ya wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Yanga Sc na wawakilishi wa Ethiopia, Welayta Dicha zitakaporudiana jioni ya leo. Miamba hiyo itarudiana katika uwanja wa Hawassa mjini Hawassa nchini Ethiopia huku Yanga Sc ikihitaji matokeo ya aina mbili yaani kutoka sare yoyote ama ifungwe si zaidi ya goli moja ili iweze kuingia hatua ya makundi na kujinyakulia kitita cha shilingi Bilioni 1 zinatolewa na Shirikisho la mpira wa miguu Afrika, CAF. Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam magoli yakifungwa na Raphael Daudi na Emmanuel Martin, kwa wenyeji Welayta Dicha watakuwa na kazi kubwa ya kuhitaji ushindi mkubwa wa magoli matatu kwa bila au zaidi yake ili isonge mbele. Na hiyo itakuwa ngumu kwani katika mchezo wa kwanza Yanga iliwakosa wachezaji wake wanne tegemeo...

YANGA NA MBEYA CITY KUPIGWA JUMAPILI, RATIBA INAWABANA KINOMANOMA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga Sc watakuwa na shughuri pevu Jumapili ijayo ya Aprili 22 watakaposhuka uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kucheza na wenyeji Mbeya City mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Yanga kesho wanacheza na Wolaika Dicha mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho barani Afrika uwanja wa Hawassa mjini Hawassa nchini Ethiopia, lakini mabingwa hao wanaosaka tiketi ya kufuzu makundi CAF watalazimika kurejea Alhamisi kwa ndege na Ijumaa wataanza safari nyingine kuelekea jijini Mbeya. Ina maana Yanga haitapata muda wa kupumzika kwani Jumamosi watafanya mazoezi ya mwisho kabla ya Jumapili kushuka uwanjani kuwania pointi tatu muhimu ili kuifukuzia Simba iliyo kileleni mwa msimamo wa ligi, wakati huo huo Bodi ya Ligi ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini, TFF, imeisogeza mbele mechi kati ya Lipuli Fc na Simba Sc iliyokuwa ichezwe Ijumaa na sasa itachezwa Jumamosi Yanga itaumana na Mbeya City Jumapili ijayo

MECHI YA LIPULI NA SIMBA YAPIGWA KALENDA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Bodi ya Ligi imeusogeza mbele mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya wenyeji Lipuli Fc na Simba Sc uliokuwa ufanyike siku ya Ijumaa katika uwanja wa Samora mjini Iringa sasa utapigwa Jumamosi ya Aprili 21. Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema wameamua kuusogeza mbele mchezo huo kwakuwa siku ya Ijumaa wamiliki wa uwanja wa Samora wameutoa uwanja huo kwa jamii hivyo kutakuwa na shughuri nyingine. Wambura amedai mechi hiyo itachezwa Jumamosi ikiwa ni siku moja baada ya kusogezwa mbele, tayari Simba wamesafiri leo asubuhi kuifuata Lipuli na mchezo huo inatazamiwa kuwa mkali na wa kusisimua, katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya 1-1 uwanja wa Taifa Dar es Salaam Lipuli na Simba sasa watakutana Jumamosi badala ya Ijumaa

Okwi bado hajavunja rekodi ya Tambwe

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba Sc, Mganda, Emmanuel Okwi kwa sasa ndiye kinara wa mabao Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoendelea akiwa amepachika magoli 19. Okwi anafuatiwa na John Bocco "Adebayor" mwenye magoli 14 na Obrey Chirwa mwenye mabao 12, Adebayor ni mchezaji wa Simba wakati Chirwa ni wa Yanga. Lakini tayari Okwi ameshavunja rekodi za baadhi ya wachezaji waliobahatika kuwa wafungaji bora kwa nyakati tofauti, Okwi amevunja rekodi za Simon Msuva na Abdulrahman Musa walioibuka wafungaji bora msimu uliopita kwa kufunga magoli 14 kila mmoja. Okwi pia ameweza kuzivunja rekodi zilizowekwa huko nyuma na wafungaji bora kama Simon Msuva aliyewahi kufunga magoli 17, Amissi Tambwe akiwa Simba aliwahi kufunga magoli 19. Rekodi ambayo Okwi hajaivunja ni ile ya kufunga magoli 21 ambayo yalifungwa na Tambwe akiwa Yanga, pia Okwi ana deni la kufikisha mabao 25 ya Mohamed Hussein 'Mmachinga" na Abdallah Juma aliyefunga magoli 3...

Yanga waipashia Dicha

Picha
Na Paskal Beatus. Hawassa Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga Sc jana walianza kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Welayta Dicha kesho Jumatano katika uwanja wa Hawassa mjini Hawassa nchini Ethiopia. Yanga ambao pia ni mabingwa wa soka nchini Tanzania, waliangukia michuano hiyo baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 2-1 na timu ya Township Rollers ya Botswana. Katika mchezo huo utakaopigwa kesho, mabingwa hao wa Tanzania bara wanahitaji sare yoyote ama kufungwa goli moja tu ili wafuzu hatua ya makundi hasa baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 2-0 zilipokutana jijini Dar es Salaam, lakini hata hivyo Yanga itakuwa na kazi ngumu hasa baada ya kuondokewa na kocha wake mkuu, Mzambia George Lwandamina Yanga wakipasha