Simba yanusurika kichapo kwa Lipuli

Na Ikram Khamees. Iringa

Vinara wa Ligi Kuu bara, Simba Sc leo imenusurika kipigo kutoka kwa wenyeji Lipuli Fc ya Iringa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Samora mjini Iringa.

Timu hizo hadi zinaenda mapumziko tayari Lipuli walikuwa mbele kwa bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji wake Adam Salamba ambaye pia ndiye mchezaji bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu bara.

Laudit Mavugo raia wa Burundi ndiye aliyeinusuru Simba isifungwe katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 59 na mechi 25, watani zao Yanga leo wanacheza na Mbeya City uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na kama watashinda basi watapunguza gepu la pointi 12

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA