Singida United yatinga fainali FA Cup

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Timu ya soka ya Singida United jana ilifanikiwa kuingia fainali baada ya kuilaza JKT Tanzania mabao 2-1 katika mchezo mkali wa nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup uwanja wa Namfua mkoani Singida.

Mchezo huo ulilazimika kuchezwa dakika 120 hasa baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa zimefungana bao 1-1, JKT Tanzania ilitangulia kupata bao la uongozi dakika ya 38 likifungwa na Hassan Matalema kabla ya Singida United hawajakomboa bao kupitia kwa Tafadzwa Kutinyu dakika ya 54.

Pambano hilo lilielekea katika muda wa nyongeza wa dakika 30 ambapo yule yule Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu aliiandikia timu yake bao la pili na la ushindi, kwa matokeo hayo Singida United imeingia fainali ambapo itaumana na Mtibwa Sugar Juni 2 mwaka huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta mjini Arusha

Singida United imeingia fainali ya FA Cup

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA