CHIRWA, BUSWITA WAANZA PAMOJA KUIANGIZA DICHA, NINJA, YONDAN KUJENGA UKUTA WA BERLIN
Na Paskal Beatus. Hawassa
Kaimu kocha mkuu wa mabingwa wa soka nchini, Yanga Sc, Mzambia Noel Mwandila leo amewaanzisha pamoja washambuliaji Obrey Chirwa, Raphael Daudi na Pius Buswita, na bila shaka hao ndio watakaoleta kashikashi langoni kwa Wolayta Dicha mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mwandila pia amemtupa benchi mlinzi wa kushoto Gardiel Michael na kumuanzisha Mzanzibar, Haji Mwinyi Mngwali ambao wataongoza katikati na Mhandisi Kevin Yondan na Abdallah Shaibu "Ninja".
KIKOSI CHA LEO CHA YANGA SC DHIDI YA WOLAYTA DICHA
1. Youthe Rostand
2. Hassani Kessy
3. Mwinyi Haji
4. Abdallah Shaibu
5. Kelvin Yondani
6. Papy Tshishimbi
7. Yusufu Mhilu
8. Thabani Kamusoko
9. Obrey Chirwa
10. Rafael Daud
11. Pius Buswita
Benchi
- Beno Kakolanya
- Juma Abdul
- Gadiel Michael
- Nadir Haroub
- Saidi Juma
- Juma Mahadhi
- Emanuel Martin