YANGA NA DICHA NI VITA YA KUINGIA MAKUNDI AFRIKA

Na Paskal Beatus. Hawassa

Hatimaye ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa imefikia ambapo mchezo wa marudiano kati ya wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Yanga Sc na wawakilishi wa Ethiopia, Welayta Dicha zitakaporudiana jioni ya leo.

Miamba hiyo itarudiana katika uwanja wa Hawassa mjini Hawassa nchini Ethiopia huku Yanga Sc ikihitaji matokeo ya aina mbili yaani kutoka sare yoyote ama ifungwe si zaidi ya goli moja ili iweze kuingia hatua ya makundi na kujinyakulia kitita cha shilingi Bilioni 1 zinatolewa na Shirikisho la mpira wa miguu Afrika, CAF.

Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam magoli yakifungwa na Raphael Daudi na Emmanuel Martin, kwa wenyeji Welayta Dicha watakuwa na kazi kubwa ya kuhitaji ushindi mkubwa wa magoli matatu kwa bila au zaidi yake ili isonge mbele.

Na hiyo itakuwa ngumu kwani katika mchezo wa kwanza Yanga iliwakosa wachezaji wake wanne tegemeo ambao ni Obrey Chirwa, Papy Kabamba Tshishimbi, Said Juma Makapu na Kevin Yondan ambao walikuwa na kadi tatu za njano, lakini wote hao wamerejea na huenda wakacheza leo kitu ambacho kitawashangaza Dicha

Yanga inaumana na Welayta Dicha leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA