NINJA AIPIGIA HESABU KALI SIMBA
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Beki wa kati mwenye uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza cha mabingwa wa soka nchini, Yanga Sc, Abdallah Seif Shaibu "Ninja" , ameipigia mahesabu makali Simba na kusema wamekwisha.
Mlinzi huyo aliyecheza vizuri kwenye mechi tatu mfululizo alizobahatika kupangwa, mbili za michuano ya kimataifa dhidi ya Wolaika Dicha ya Ethiopia na moja ya Ligi Kuu bara dhidi ya Singida United amedai mechi dhidi ya Simba ndio njia yake ya kumtoa kimaisha.
Ninja aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea Taifa Jang' ombe ya Unguja, Zanzibar, hakuwa na mwanzo mzuri kwenye kikosi hicho kutokana na kushindwa kwake kuonyesha kile wanachotaka Wanayanga.
Lakini kwa sasa beki huyo ametokea kuwakosha mashabiki wa Yanga na sasa amekuwa kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa, Simba na Yanga zitaumana Aprili 29 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na beki huyo ameipigia mahesabu mechi hiyo, Jumapili ijayo Yanga itacheza na Mbeya City uwanja wa Sokoine mjini Mbeya