YANGA YATINGA MAKUNDI SHIRIKISHO, KULAMBA BILIONI MOJA SAAFI
Na Paskal Beatus. Hawassa
Klabu bingwa ya soka Tanzania bara na wawakilishi pekee waliosalia katika mashindano ya kimataifa, Yanga Sc jioni ya leo imefuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kufungwa bao 1-0 na wenyeji wao Welayta Dicha ya Ethiopia.
Mchezo huo wa marudiano uliofanyika katika uwanja wa kimataifa wa Hawassa uliopo mjini Hawassa wenyeji walifanikiwa kujipatia bao lao la kuongoza lililofungwa na mshambulizi wake raia wa Togo, Arafat Djako kunako dakika ya pili kipindi cha kwanza.
Baada ya kupata bao hilo Welayta Dicha waliendelea kulisakama lango la Yanga kama nyuki lakini kipa wa mabingwa hao wa soka nchini Mcameroon, Youthe Rostand alikuwa imara kuokoa hatari zote na timu hizo kwenda mapumziko matokeo yakiwa hayo.
Kipindi cha pili Yanga waliendelea kulilinda lango lao na shukrani ziwaendee mabeki wa kati Kevin Yondan na Abdallah Shaibu "Ninja" ambao walifanya kazi yao vizuri na kumaliza Yanga ikisonga mbele kwa jumla ya ushindi wa mabao 2-1 baada ya ushindi wa 2-0 waliopata jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo Yanga imejihakikishia kulamba jumla ya shilingi Bilioni 1 na ushee ambazo zitawafanya wajiandae vizuri ikiwemo kuimarisha kikosi chao