YANGA YAANGUKIA MIKONONI MWA WAARABU CAF

Na Asher Maliyaga. Dar es Salaam

Yanga Sc ya Tanzania imepangwa pamoja na timu za Rayon Sports ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya na USM Alger ya Algeria katika kundi D kombe la Shirikisho barani Afrika na itaanza kushuka uwanjani Mei 6 mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa jana saa nane mchana makao makuu wa Shirikisho la mpira wa miguu mjini Cairo, Misri, makundi manne yamepangwa ambapo Yanga Sc itaanza na waarabu hao wa Algeria.

Kundi A lina timu za Asec Mimosas ya Ivory Coast, Raja Casablanca ya Morocco, AS Vita ya DR Congo na Aduana Stars ya Ghana, wakati kundi B lina timu za RS Berkane ya Morocco, El Masry ya Misri, UD Songo ya Msumbiji na El Hilal ya Sudan.

Kundi C lina timu za Enyimba ya Nigeria, Williamsville ya Ivory Coast, CARA ya Kongo Brazaville na Djoliba ya Mali, wakati kundi D linajumuhisha mabingwa wa Tanzania bara Yanga Sc, USM Alger ya Algeria, Rayon Sports ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA