TAMBWE FITI KUIVAA SIMBA JUMAPILI
Na Saida Salum. Morogoro
Mshambuliaji wa kimataifa wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Yanga Sc, Amissi Joceylin Tambwe raia wa Burundi huenda akacheza dhidi ya Simba.
Watani wa jadi Simba na Yanga zinaumana Jumapili ijayo uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara na mtaalamu huyo wa vichwa ataungana na kikosi cha Wanajangwani kuhakikisha pointi tatu zinaenda Yanga.
Yanga imeweka kambi mjini Morogoro kujiandaa na mchezo huo na kwa mujibu wa daktari wa Yanga, Edward Bavu amesema Tambwe yuko fiti na anaweza kucheza bila wasiwasi huku kocha wa muda wa mabingwa hao Mzambia Noel Mwandila tayari ameanza kumshuhudia mazoezini na anakiri jamaa yuko fiti