KUELEKEA SIMBA NA YANGA JUMAPILI, REKODI YA KIBADEN YAWAUMIZA VICHWA OKWI, BOCCO NA CHIRWA

Na Paskal Beatus. Dar es Salaam

Mwaka 1977 Simba Sc almaarufu Wekundu wa Msimbazi au wana Lunyasi waliinyanyasa Yanga Sc kwa kuichapa mabao 6-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Taifa (Sasa Uhuru Stadium).

Mshambuliaji wa Simba wakati huo Abdallah Seif Athuman Kibaden aliifungia Simba mabao matatu katika mchezo huo huku mengine mawili yakifungwa na Jumanne Khamis Masimenti na goli lingine Yanga walijifunga.

Basi mpaka sasa imepita takribani miaka 39 hakuna mchezaji yeyote si wa Simba wala Yanga aliyeweza kumfikia Kibaden kwa kufunga mabao matatu kwenye mchezo mmoja wa watani.

Lakini Jumapili ijayo watani hao wa jadi wa soka la Tanzania wanaumana katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba wao wana washambuliaji watatu ambao wanaweza kufanya lolote katika mchezo huo kwa kuvunja rekodi ya Kibaden.

Simba wanaye Emmanuel Anord Okwi, John Raphael Bocco na Shiza Kichuya ambao wanaweza kumfikia Kibaden ingawa wafanye kazi kwelikweli kuupita ukuta wa Yanga ulio chini ya Kevin Yondan na Abdallah Shaibu "Ninja" au Andrew Vicent "Dante", na Yanga wanao watu hatari kama Obrey Chirwa, Raphael Daudi au Pius Buswita ambao kila mmoja anaweza kuvunja rekodi ya Kibaden.

Ukuta wa Simba una watu mahiri kama Salim Mbonde, Jjuko Murushid au Yusuph Mlipili ambapo unaweza usiamini kuwa huenda Kibaden akaendelea kutesa na rekodi yake ya Hat trick ndani ya Simba na Yanga "Derby"

Abdallah Kibaden (Pichani) rekodi yake huenda ikavunjwa Jumapili

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA