ERASTO NYONI APELEKA MAAFA JANGWANI
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Goli lililofungwa dakika ya 37 kipindi cha kwanza na mlinzi Erasto Nyoni limepeleka kilio mitaa ya Jangwani baada ya Simba Sc kuichapa Yanga Sc bao 1-0 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Huo ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara ambapo sasa Simba imefikisha pointi 62 na mechi 26 ikiiacha mbali Yanga yenye pointi 48 na mechi 24 ikishika nafasi ya tatu hasa baada ya Azam Fc jana kushinda 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mpira wa leo Simba imeonekana kuutawala karibu vipindi vyote viwili, huku Yanga ikishindwa kabisa kupeleka mashambulizi langoni kwa Simba na kumfanya kipa wake Aishi Manula kukaa likizo, mlinzi wa Yanga Hassan Kessy alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Kituko kingine ni Yanga kushindwa kupata hata kona moja kitendo ambacho hakijawahi kutokea tangia watani hao wakutane