KIPA WA KIMONDO FC AVUNJIKA MGUU AJALINI
Na Ayubu Mhina. Chalinze
Mlinda mlango wa zamani wa Kimondo Fc ya Mbeua na Polisi Moro, Azishi Simon amevunjika binaya mguu wake wa kuloa baada ya kupata ajali mbaya ya bodaboda maeneo ya Mdaula, Chalinze mkoani Pwani Junamosi iliyopita.
Kwa mujibu wa mashuhuda ajali hiyo ilitokea wakati kipa huyo akiendesha pikipiki ndogo aliyopewa na mjomba wake ili airejeshe nyumbani kwao, mmoja kati ya mashuhuda hao amedai Azishi alikuwa amelewa na aliendesha pikipiki kwa mwendo kasi.
Kipa huyo wa zamani wa timu ya mkoa wa Pwani iliyoshiriki michuano ya Taifa Cup alivunjika vibaya mguu wake baada ya kugongana uso kwa uso na roli lililokuwa likienda kwa mwendo kasi, ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Mdaula, barabara ya Kidugalo na inasemekana chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi na ulevi, kipa huyo amelazwa katika hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani