Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TSHISHIMBI, AJIBU WAREJEA KUIANGAMIZA SIMBA LEO

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Kaimu kocha mkuu wa klabu bingwa ya soka Tanzania bara, Yanga Sc, Mzambia Noel Mwandila na msaidizi wake Shadrack Nsajigwa wakisaidiwa na kocha mpya raia wa DR Congo, Mwinyi Zahera wamewaanzisha Papy Kabamba Tshishimbi na Ibrahim Ajibu huku pia wakimrejesha Andrew Vincent Chikupe maarufu Dante kwenye eneo la ulinzi akisaidiana na Mhandisi Kevin Yondani kulinda ukuta wa Yanga.

Yanga inashuka dimbani leo kusaka ushindi wake wa kwanza tangia alipoondoka kocha mkuu Mzambia George Lwandamina anayedaiwa kutimkia kwao Zambia kujiunga na timu yake ya zamani ya Zesco United.

Kikosi kamili cha mabingwa hao kinatarajiwa kuwa hivi dhidi ya Simba Sc

1. Youthe Rostand
2. Hassani Kessy
3.  Gadiel Mbaga
4. Andrew Vicent
5. Kelvin Yondani
6. Saidi Juma
7. Yusufu Mhilu
8. Papy Tshishimbi
9. Obrey Chirwa
10. Rafael Daudi
11. Ibrahim Ajibu

Benchi
- Ramadhani Kabwili
- Abdallah Shaibu
- Juma Abdul
- Juma Mahadhi
- Maka Edward
- Pius Buswita
- Emanuel Martin

Papy Tshishimbi (Katikati) amepangwa kuanza leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe