TFF yaimwagia misifa Yanga kwa kutinga makundi CAF
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Shirikisho la mpira wa miguu nchini, TFF limeimwagia salamu za pongezi klabu ya Yanga kwa kufanikiwa kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.
Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia ameisifu Yanga kwa kufanikiwa kuingia hatua hiyo ambapo amedai ni heshima kubwa kwa nchi.
Karia amedai kitendo ilichofanya Yanga ni cha kuigwa na vilabu vyote nchini vitakavyopata nafasi ya kushiriki, "Yanga imetuletea heshima kubwa kwa kuingia makundi, naamini nchi yetu itaheshimiwa", alisema Karia ambaye amesisitiza Shirikisho lake litaendelea kushirikiana na Yanga.
Yanga jana ilitinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika kwa kuiondoa Welayta Dicha ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 2-1 na itawasili nchini leo usiku wa saa 7:00