MAKALA: Kichuya kuvunja rekodi ya Omari Hussein Keegan?

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Rekodi ya mfungaji wa magoli matatu (Hat trick) inashikiliwa na King Abdallah Kibaden Mputa wa Simba Sc ambaye alifunga mabao hayo mwaka 1977 wakati Simba ilipoibugiza Yanga mabao 6-0 uwanja wa  Taifa Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu bara.

Lakini mshambuliaji wa Yanga Sc, Omari Hussein wengi walimpachika jina la utani Keegan wakimdananisha na mwanasoka wa kimataifa ulimwenguni, Kevin Keegan, Omari Hussein ni mchezaji wa Yanga yeye ameweka rekodi ya kuwa mfungaji wa muda wote wa mechi za watani Simba na Yanga.

Keegan amefunga jumla ya magoli sita ambayo ni mengi na mchezaji pekee anayekaribia kumfikia ama kuweza kuivunja rekodi hiyo ni kiungo mshambuliaji wa Simba Sc, Shiza Kichuya ambaye yeye amefunga mabao manne mpaka sasa.

Keegan alianza kufunga tangu Septemba 18, 1982 Yanga ilipoifunga Simba mabao 3-0, Keegan alifunga mabao mawili dakika ya 2 na 85 huku goli lingine likifungwa na Makumbi Juma dakika ya 62.

Keegan alifunga tena Aprili 16, 1983 Yanga ikiichapa tena Simba mabao 3-1, wafungaji wa Yanga walikuwa Charles Mkwasa dakika ya 21, Makumbi Juma dakika ya 38 na Keegan dakika ya 84 goli pekee la Simba lilifungwa na Musa Kihwelo dakika ya 14.

Machi 10, 1984 Yanga na Simba zilitoka sare ya kufungana bao 1-1, Omari Hussein Keegan akaifungia Yanga bao dakika ua 72 wakati bao la Simba lilifungwa na kipa Idd Pazi kwa mkwaju wa penalti dakika ya 20.

Mei 19, 1985 Yanga na Simba zilitoka tena sare ya kufungana bao 1-1 na Omari Hussein Keegan akaifungia Yanga bao dakika ya 6 na Simba wakapata bao kupitia Mohamed Bob Chopa dakika ya 30.

Agosti 23, 1986 safari hii Simba ikaifunga Yanga mabao 2-1 yaliyofungwa na Edward Chumila dakika ya 9 na Malota Soma dakika ya 51 wakati goli pekee la Yanga lilifungwa na Keegan dakika ya 5, jumla mshambuliaji huyo Omary Hussein Keegan anaweka historia ya kuwa mfungaji wa wakati wote wa mechi za watani wa jadi Simba na Yanga

Miamba hiyo inaumana siku ya Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam

Shiza Kichuya anakaribia kuvunja rekodi ya Omary Hussein Keegan wa Yanga

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA