MZUKA YANGA UMEPANDA BAADA YA KUREJEA NGOMA
Na Saida Salum. Morogoro
Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc huenda wakawa na furaha baada ya kikosi chake kuimarika upya kufuatia nyota wake waliokuwa wakiunda kikosi cha kwanza na kuipa ubingwa wa bara mara tatu mfululixo kurejea uwanjani.
Yanga imeweka kambi mjini Morogoro na Jumapili itaumana na mahasimu wake Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara utakaopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabingwa hao watetezi wapo kambini Morogoro sawa na mahasimu wao lakini upepo unaweza kuwaendea poa baada ya mastraika wake hatari Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma kuanza mazoezi na kwa mujibu wa daktari wa timu Edward Bavu, nyota hao wanaweza kucheza mechi hiyo.
Ngoma na Tambwe wamekuwa wakiitesa sana Simba na kama watapangwa huenda mchezo huo ukawa mkali na wa kusisimua, pia katika mazoezi yanayoendelea ya klabu hiyo, Ibrahim Ajib ambaye naye alikuwa majeruhi ameanza mazoezi na kuongeza mzuka wa mechi hiyo