Hanspoppe aunganishwa na Aveva, Kaburu kesi ya utakatishaji
Na Asher Maliyaga. Dar es Salaam
Mahakama mkazi ya Kisutu mjini Dar es Salaam imeliagiza jeshi la Polisi kumkamata haraka mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hanspoppe na kumuunganisha na viongozi wenzake katika kesi ya utakatishaji fedha inayowakabili na kughushi.
Hakimu mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba amelitaka jeshi la polisi kumkamata mara moja Hanspoppe kwani ameonekana kuhusika moja kwa moja kwenye kesi hiyo inayowakabili Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake Geofrey Nyange "Kaburu" ambao wanasota mahabusu hadi sasa.
Hanspoppe naye amehusishwa kwenye kesi hiyo ya utakatishaji fedha za klabu ya Simba zinazokadiliwa kufikia dola 300,000 za Kimarekani, kwa mujibu wa wakili wa Taasisi ya kupambana na rushwa nchini, (TAKUKURU) Leonard Swai amebadilisha hati ya mashitaka na kuliingiza jina la Hanspoppe pamoja na Franklin Lauwo ambapo wote hao watapelekwa na polisi na sasa wametakiwa kukamatwa