Mama Kikwete amwambia Ali Kiba asipende kukagua simu ya mkewe

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Mke wa Rais wa Awamu ya nne ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, mama Salma Kikwete amemtaka mwimbaji nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini Ally Saleh Kiba "Ali Kiba" kutopendelea tabia ya kukagua simu ya mkewe.

Ally Kiba alifunga ndoa majuma mawili yaliyopita na mchumba wake Amina Khaleef, Mombasa, Kenya na sherehe yake inefanyika juzi katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam ambapo mama Kikwete alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika sherehe hiyo iliyoonyeshwa moja kwa moja na Azam Tv.

Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mbunge maalum wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, alimtaka msanii Ally Kiba kulinda ndoa yake na kamwe asidiriki kukagua simu ya mkewe kwa kuangalia sms na simu zinazopigwa kwani zinaweza kuvunjika ndoa.

Amedai ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu hiyo ya kutoaminiana, hivyo Kiba anapaswa kupuuzia sms ama simu anazopigiwa mkewe na anatakiwa kumuamini

Ali Kiba ameambiwa na Mama Kikwete asipende kukagua simu ya mkewe 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA