Stand United na Mtibwa Sugar ni nusu fainali ya kisasi
Na Mwandishi Wetu. Shinyanga
Leo inapigwa nusu fainali ya kwanza ya kombe la Azam Sports Federation Cup kati ya Stand United na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Stand United inaingia katika mchezo huo ikiwa nyumbani mbele ya mashabiki wake hivyo kila sababu ya kuweza kuchomoza na ushindi, lakini vijana wa Mtibwa Sugar ambao msimu huu wanaonekana kuimarika haswa, hawatataka kupoteza mchezo huo.
Hivyo wanahitaji kushinda ili kuongia fainali ikisubiri mshindi mwingine kati ya Singida United na JKT Tanzania keshokutwa, Srand United leo itawategemea mshambuliaji wake Vitalis Mayanga na Mtibwa Sugar ina winga wake hatari Salum Kihimbwa