KOCHA WA DRC CONGO AJA KUMRITHI LWANDAMINA YANGA

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Kocha wa kimataifa aliyepata kuzifundisha timu mbalimbali barani Afrika na Ulaya, Mwinyi Zahera raia wa DRC Congo amewasili Dar es Salaam kujiunga na mabingwa wa soka nchini Yanga Sc na muda wowote kuanzia sasa atasafiri kuelekea Morogoro kuungana na kikosi hicho ambapo kimepiga kambi huko.

Taarifa zenye uhakika kutoka klabu ya Yanga zinasema Zahera kocha mzoefu kabisa la Afrika akiifundisha timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidwmokrasia ya Congo (Leopards) amekuja nchini kwa ajili ya kumrithi Mzambia George Lwandamina ambaye aliondoka klabuni hapo majuma mawili yaliyopita na kurejea nyumbani kwao Zambia ambapo inadaiwa amejiunga na timu yake ya zamani ya Zesco United.

Tayari Yanga iko kambini Morogoro ikitokea jijini Mbeya ambapo juzi Jumapili ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji wao Mbeya City uwanja wa Sokoine, na Jumapili ijayo inacheza na mtani wake Simba Sc hivyo kwa vyovyote pambano litakuwa gumu kwani timu zote mbili zinapigania ubingwa licha kwamba Yanga iko nyuma kwa tofauti ya pointi 11 dhidi ya mahasimu wao Simba Sc

Mwinyi Zahera anachukua mikoba ya George Lwandamina

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA