Makonda kuwa mgeni rasmi Simba na Yanga Jumapili

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Poul C Makonda anatazamiwa kuwa mgeni wa heshima kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Simba na Yanga utakaofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mchezo huo utakaopigwa siku ya Jumapili kuanzia saa 10:00 na kurushwa na Azam Tv, Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa soka watakaojitokeza kushuhudia mchezo huo wenye kuvuta hisia za wengi.

Makonda amewahi kuwa mgeni rasmi wakati klabu ya Simba ilipokuwa ikiadhimisha siku ya kuzaliwa kwake inayofahamika kama Simba Day mwaka jana katika uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, katika mchezo huo kiingilio cha chini kabisa jukwaa la mzunguko ni shilingi 7000

Mkuu wa mkoa Dar es Salaam, Poul Makonda (Kulia) atakuwa mgeni rasmi Simba na Yanga Jumapili

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA