Kamera kufungwa kila kona uwanja wa Taifa, Simba na Yanga
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Katika kuhimarisha Usalama Ndani ya Uwanja wa Taifa katika Pambano la Watani wa Jadi Kati ya Simba SC Dhidi ya Yanga SC hapo Aprili 29,Shirikisho la Soka Nchini (TFF) limetangaza Kufungwa kwa Kamera 109 Uwanjani.
Afisa habari wa Shirikisho hilo Clifford Ndimbo Amesema kuwa watu wa Usalama Wamejipanga kuhakikisha Wanazuia Vurugu zitakazojitokeza Uwanjani Hapo Siku ya Mchezo huo.
Huku kwa Upande wa Jeshi la Polisi Wamesema kuwa Wamejipanga kuhakikisha Amani Inakuweoo Kuanzia Mwanzo wa Mchezo Mpaka Mwisho.
Uwanja Utakuwa wazi Kuanzia Saa 2.00 Asubuhi.