Azam Fc yalipa kisasi kwa Mtibwa na kuishusha Yanga
Na Ikram Khamees. Morogoro
Mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Azam Fc jioni ya leo imefanikiwa kulipa kisasi baada ya kuichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Manungu Complex mjini Morogoro.
Bao pekee la Azam Fc limefungwa na mshambuliaji wake chipukizi Shabani Iddy Chilunda kunako dakika ya 43, ushindi huo unaifanya Azam Fc iliyocheza mechi 26 kufikisha pointi 49 na kuifanya ikamate nafasi ya pili na kuishusha Yanga Sc yenye pointi 47 na mechi 23.
Matokeo mengine mjini Songea katika uwanja wa Majimaji, mabingwa wa zamani wa Tanzania, Majimaji Fc imewalaza Ruvu Shooting mabao 3-1 na kuzidi kujinusuru na janga la kushuka daraja, Stand United imelazimishwa sare tasa 0-0 na majirani zao Kagera Sugar katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho lakini macho na masikio ni uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, watani wa jadi Simba na Yanga wataumana vikali