Straika Welayta Dicha kumrithi Ngoma Yanga

Na Albert Babu. Dar es Salaam

Mabingwa wa soka Tanzania bara na wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa, Yanga Sc wamemnasa straika hatari wa timu ya Welayta Dicha ya Ethiopia, Arrafat Djako raia wa Togo na kuna uwezekano mkubwa akasajiliwa.

Yanga inaruhusiwa kufanya usajili mdogo hivi sasa kwa ajili ya kushiriki hatua ya makundi na Djako anatajwa kutua Jangwani kutokana na kuridhishwa na kiwango chake.

Djako ni mshambuliaji lakini ana uwezo wa kucheza kiungo wa pembeni na ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, Yanga ilifungwa bao 1-0 na Welayta Dicha Jumatano iliyopita na goli pekee lilifungwa na nyota huyo.

Kuna taarifa huenda Yanga ikaachana na Mzimbabwe Donald Ngoma ili nafasi yake kuchukuliwa na Mtogo huyo kwakuwa tayari Yanga imeshamaliza nafasi za wachezaji saba wa kigeni.

Wachezaji ambao wa kigeni Yanga inao ni Youthe Rostand (Cameroon), Obrey Chirwa (Zambia), Thabani Kamusoko, Donald Ngoma (Zimbabwe), Fiston Kayembe, Papy Kabamba Tshishimbi (DR Congo) na Amissi Tambwe (Burundi) , pia kuna uwezekano wa kumuondoa Kayembe ambaye mpaka sasa hajaitumikia klabu hiyo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA