YANGA NA MBEYA CITY KUPIGWA JUMAPILI, RATIBA INAWABANA KINOMANOMA
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga Sc watakuwa na shughuri pevu Jumapili ijayo ya Aprili 22 watakaposhuka uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kucheza na wenyeji Mbeya City mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga kesho wanacheza na Wolaika Dicha mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho barani Afrika uwanja wa Hawassa mjini Hawassa nchini Ethiopia, lakini mabingwa hao wanaosaka tiketi ya kufuzu makundi CAF watalazimika kurejea Alhamisi kwa ndege na Ijumaa wataanza safari nyingine kuelekea jijini Mbeya.
Ina maana Yanga haitapata muda wa kupumzika kwani Jumamosi watafanya mazoezi ya mwisho kabla ya Jumapili kushuka uwanjani kuwania pointi tatu muhimu ili kuifukuzia Simba iliyo kileleni mwa msimamo wa ligi, wakati huo huo Bodi ya Ligi ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini, TFF, imeisogeza mbele mechi kati ya Lipuli Fc na Simba Sc iliyokuwa ichezwe Ijumaa na sasa itachezwa Jumamosi